Wabunge na wanasiasa wa Zanzibar ni sitaki nataka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge na wanasiasa wa Zanzibar ni sitaki nataka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kalunguine, Aug 26, 2011.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mwenendo wa jana wa wabunge wa Zanzibar wakati wakichangia hotuba ya waziri kivuli wa kambi ya upinzania unaonyesha jinsi wanasiasa wa Zanzibar walivyokuwa sitaki nataka. Mara nyingi wameigiza kana kwamba hawautaki muungano. Lakini wameshindwa jaribio alilowapa waziri kivuli pale wa wizara ya sheria na mambo ya katiba walipoweweseka alipowasilisha hotuba yenye mapendekezo kuwa wazazinbar washiriki katika mchakato wa katiba huku bara kwa mambo yanayohusu muungano tu na si vinginevyo. Sasa waliweweseka nini huku kauli zao wameonyesha kujinasibu kuwa wao hawautaki muungano?.

  Wamekula matapishi yao. Nawashauri wasijidai tena kuonyesha kuwa hawana haja na muungano.
   
 2. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.  Wabunge kutoka Zanzibar wameishambulia hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Katiba na Sheria, wakisema Zanzibar si koloni la Tanganyika.
  Walitoa kauli hiyo wakati wakichangia hotuba ya kambi hiyo kuhusu makadiro ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2011/2012.
  Hotuba hiyo iliwasilishwa bungeni juzi na Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.
  Mbunge wa Magomeni (CCM), Muhammad Amour Chomboh, alisema maneno yaliyotolewa na Lissu ni ya ufedhuli.
  “Napenda kumfahamisha yeye (Lissu) pamoja na wengi walio humu ndani wenye mawazo mgando kama yeye na waliokuwapo nje ya jumba hili, Zanzibar sio koloni la Tanganyika na halitakuwa hata siku moja koloni la Tanganyika. Na mheshimiwa Lissu Agosti 8 mwaka huu, alizungumza huyu kuhusiana na mambo ya Muungano kuchangia katika hotuba ya Muungano akajaribu kuwataja viongozi, ambao ni victim (waathirika) wa Muungano, ambao ni muongo na mnafiki,” alisema.
  Aliongeza: “Nataka kumwambia kuwa Wanzanzibari hawatakubaliana na mpuuzi yoyote na uozo wowote, ambao umezungumzwa hapa kwa minajili ya kutaka kutugombanisha,” alisema.
  Alipotaka kuendelea, alikatishwa na Lissu aliyekuwa akiomba utaratibu.
  Kwa mara nyingine, Lissu alisimama akitaka kutoa taarifa hata hivyo, lakini Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliingilia kati na kuwataka wabunge wote kuwa wavumilivu na kisha kumruhusu Chomboh kuendelea kuchangia.
  Mbunge wa Tumbe (CUF), Rashid Ali Abdallah, alisema kauli aliyoitoa Lissu wakati akisoma hotuba hiyo, inaonyesha kuwa haelewi maana ya taifa.
  “
  Haelewi historia ya Zanzibar. Na kwa maana hiyo, mwelekeo wa Kambi ya Upinzani umepotea njia. Nadhani haya ni maoni yake. Unaposema Rais wa Zanzibar atolewe katika mambo yanayohusiana na Muungano una maana gani? Ipo serikali ya Tanganyika kujadili mambo ya Tanganyika hapa?” alihoji.
  Aliongeza: “…Nazungumza hili kwa uchungu kabisa. Huyu ni msomi, lakini sijui amehitimu vipi usomi wake…jambo la msingi ni kuimarisha taifa letu liwe na nguvu lenye utawala bora na misingi ya uwajibikaji. Mawazo haya ya mheshimiwa waziri kivuli wa katiba na sheria ni mawazo funyu, yamepitwa na wakati na hayatapewa nafasi.”
  Naye Mbunge wa Donge (CCM), Sadifa Juma Khamis, alisema mazungumzo yaliyotolewa na Lissu juzi yamevunja hata Katiba iliyopo hivi sasa.
  Aliwataka kuangalia kifungu namba nane na namba tisa vya Katiba, vinavyomtaka mwananchi kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yanayohusu nchi yake ya Tanzania.
  Alisema kungekuwa na Serikali ya Tanganyika wasingeingilia mambo yanayohusu serikali hiyo.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, alisema Lissu katika hotuba alitoa maneno ya uchochezi.  CHANZO: NIPASHE
   
 3. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani hawa wabunge wa nzanzibar wana matatizo makubwa sana. Hivi wanaweza kusema Tundu Lisu kavunja katiba ya jamuuri ya muungano ihali wao ndio wamevunja na bado wanaendelea kuivunja katiba ya jamuuri ya muungano wa tanzania. Hivi katiba ya JAMUURI YA MUUNGANO WA TANZANIA INA SEMAJE KUUSU ZANZIBAR. KUTAKUWA NA RAIS NA WAZIRI KIONGOZI aisemi Makamu wa kwanza na wapili hapa wamevunja. pia aisemi kuwa zanzibar ni NCHI. Napata shida sana kuwaelewa hawa Mungu wetu tuurumie maana kuna watu wana mawazo mgando sana katika bunge letu ila wapinzani wa kweli wakisema kitu tu basi shida utasikia hapana na SPIKA Wetu na ye kimya jamani.
   
 4. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwanza huyo mbunge wa Tumbe kalidanganya Bunge, ni wapi ambapo Lissu amesema kuwa rais wa zanzibar atolewe ktk mambo yanayohusu muungano?! Anajua kusoma huyo kweli?!
   
 5. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  We acha tu, Lissu katoa hoja za maana lakini spika anawaachia hao wazenji waendelee kutoa pumba zao. Halafu wakati bunge linaahirishiswha anasema yote yanayofanyika bungeni hakuna mwenye lengo la kumkomoa mtu. Akaomba msamaha kwa watu waliokwazwa jinsi bunge lilivyoendeshwa.Anauma hulu anapulizia. Kitu ambacho hajui, ni kujitambua. Mawazo ya kukitetea chama chake CCM yapo kwenye conscious na sub-conscious yake.
   
 6. e

  emrema JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanajijua wazi kuwa wao ni koloni letu waacheni wajifariji. Kama sio kolini waulize FIFA.
   
 7. e

  emrema JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kolini = KOLONI
   
Loading...