Wabunge na wananchi kama wasanii na mashabiki wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge na wananchi kama wasanii na mashabiki wao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Jun 20, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nafananisha Wabunge wetu wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wapiga kura wao kama ilivyo kwa Wasanii wa filamu na Muziki kwa mashabiki wao.
  Kila Msanii ana mashabiki wake kwa sababu tu ya aina ya muziki/filamu anazocheza bila hata kujali athari za aina ya uigizaji huo katika jamii na Wasanii wamekuwa wajanja kweli, wanapakua kile ambacho wanajua kitajiuza. Bila kumumunya maneno, sababu kubwa ya wanamuziki wetu kujikita kutoa nyimbo za mapenzi ni kwa sababu mashabiki wao wengi ndizo wanazozipenda. Hivi kweli hakuna nyimbo au filamu za kuweza kuonya jamii, kuhamasisha uzalendo, kuhimiz matumizi ya lishe bora, kutunza mazingira?

  Tafakari yangu ya leo: Wabunge wetu wetu wamekwisha tusoma wananchi na kugungua kuwa tunachopendelea kusikia bungeni siyo tulichowatuma kusema kwa ajili ya maendeleo yetu, bali tunapendelea kusikia mbwembwe zao. Wameshatambua kuwa tunachopendelea kusikia ni jinsi gani leo Serikali imeshambuliwa hata kama hakuna hoja ya msingi. Kitendo cha wabunge kutoa lugha za matusi tena mbele ya chombo ambacho kimeundwa na kuongozwa na kanuni ambao wamezitunga wenyewe na wakati huo huo tunajiaandaa kuwapokea majimboni kwa maandamano ni dhahiri kabisa kwamba wanafanya hivyo makusudi ili kujipatia umaarufu wa kisiasa kwa vile wameshatambua kuwa hicho ndicho tunachokihitaji.
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  well said
   
Loading...