Wabunge na viongozi mbalimbali wachukue nafasi za ufundishaji katika shule za senti kayumba.

Jul 29, 2012
52
4
Ualimu ni kazi sio kama kazi nyingine rahisi rahisi inahitaji kupewa heshima kubwa sana, Wadau wa Elimu wakubwa ni Waalimu wanavyodai haki zao ijulikane kuwa mazingira ya kazi na stahili zao haziko shwari kabisa. Uwezo wa kutoa elimu ni fani isiyo elezeka kisaikolojia kwa maana Elimu ni ufunguo wa Maisha, na ni Mwalimu anae saidia kumfungua mwanafunzi husika kwa kidato au darasa aliopo au kwa elimu husika. Kwa aliye Serikalini wengi huwa hawana uelewa kutokana na kupata elimu isiyo boreshwa toka enzi hizo kupelekea kupoteza uzalendo ndani ya Nchi hii, kwa mfano Dr. JK anaweza kushika chaki na kumfundisha mtoto kusema "a, e, i, o, u" katika shule ya msingi darasa la kwanza huko chunya au sumbawanga ndani yani ndani zaidi Tanzania hapa? Uzalendo jamani upo kwa walimu tuamini hivyo. Mtu anae bisha nahisi hajui anakotokea na ni mtu asiyejielewa anakoelekea. Sio kosa lake, kwa maana baba wa Taifa alikuwa mwalimu na alikuwa mzalendo katika nchi yake. Je katika suala la madai ya walimu ungelifumbia macho laiti ungelikuwa wewe? Jamani nina sababu nyingi za kulalamikia serikali kiujumla lakini haisikii kama sikio la kufa. Kwa mwisho ninaomba kuwe na mbadilishano wa kazi. Wabunge na viongozi wa serikali wabadilishane kazi na walimu. Ili kujifunza ugumu uliopo katika hiyo fani nchini mwetu ili wawe wazalendo. Serikali haina uzalendo kabisa kwa maana wengi wangekuwa wanapitia fani ya elimu ili kuwa wazalendo zaidi, waajiliwe na kufundisha kwa miaka hata miwili na kujifunza hali halisi ya watanzania. Na walimu kutokana na hali ngumu ya maisha yao na ugumu wa mazingira ya kazi kutoboreshwa inawafanya kutoa elimu isiyo kuwa na uzalendo kabisaaaaaaa. Nchi zilizo endelea makutano katika ya mwalimu na mwanafunzi yanawafanya wajifunze uzalendo wao shuleni na kuifanya nchi yao ndo maana mmarekani ataitetea marekani,lakini mtanzania ataitetea familia yake na tumbo lake wengine kwake maadui, wasaliti, wagomvi, wagomaji na hawana maana. Wahenga hawakukosea samaki mkunje angali mbichi, je hata mzalendo mfanye mzalendo toka akiwa mtoto na afanyae haya ni Mwalimu na wala sio JK au Mbunge yoyote. Taifa la kesho ndo watoto na m2 muhimu wa kulifanya Taifa la kesho liwe la Uzalendo ni Mwalimu. Jamani daah!
 
sawa ila unachanganya lugha hatuelewi maana halisi ya neno hili ni senti ama saint tumia kiswahili kama hujui english
 
Back
Top Bottom