wabunge na posho zao na magari yao, kazi inafanyika kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wabunge na posho zao na magari yao, kazi inafanyika kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by limited, Feb 8, 2011.

 1. l

  limited JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  wana jf wasalaam. Hivi hawa wabunge tuliowachagua wanatekeleza majukumu yao kwa ufasaha?
  nimekuwa nikijiuliza unakuta mtu ni mfanyabiashara mkubwa(au mzuri) lakini anajiingiza kwenye ubunge, na anatumia hela nyingi kwa ajili ya kampeni, kwa mahesabu ya harakaharaka ni kama mtu anaenda bungeni kuongeza mtaji au jina la biashara na title ya mheshimiwa. sioni haja ya mbunge kulalama kwamba wanachi wana hali mbaya wakati anadai posho kubwa na jimboni kwake hakuna cha maana na akishapewa ukurugenzi, au hizi tume zisizokuwa na mbele wala nyuma basi anazubaa tu.
  Kuna kitu kinaitwa uzalendo kuna wabunge wangapi au hata madiwani wangapi wanajua Definition ya uzalendo sasa hivi?

  Kuna kitu kikubwa sana Kinataka kutokea tanzania hii yetu (mabadiliko ya katiba) Hivi kuna mbunge atakae enda kwenye jimbo lake na kuwaelimisaha wananchi wake kuhusu ili?(au watakaa waombe hela ya kuwaelimisha wananchi katiba) Tukumbuke hela wanayotumia ni sisi tunaolipa.
  mwaka jana Kikao cha bajeti nilitakakulia. waziri alikuwa akitaja nchi zinazotufadhili kwenye bajeti yetu, wabunge wetu walikuwa wanagonga meza kwa ufahari kama watoto wa O level SIKUWAELEWA. ina maana ni ujasiri kila mwaka kutumia hela ambayo huna alafu tunatamba kwamba uchumi umekua?
  Thanks
   
Loading...