Wabunge na Polisi ndio wanaoongoza duniani kwa vitendo vya rushwa, wote wakiwa na 36

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Messages
7,322
Points
2,000

Francis12

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2016
7,322 2,000
Wabunge na Polisi ndio wanaoongoza duniani kwa vitendo vya rushwa, wote wakiwa na 36%, uchunguzi wa Jukwaa la Uchumi wa Dunia (WEF) umebainisha.

Kwa mujibu wa jukwaa hilo, rushwa hugharimu uchumi wa dunia TZS trilioni 8.4 kila mwaka, na rushwa hiyo huja katika mifumo mbalimbali.

Katika uchunguzi wa mwaka 2017 ilibainika kuwa, kati ya kila mtu 1 kati ya watu 4 alikiri kutoa rushwa ili kupata huduma ndani ya miezi 12 iliyopita katika mwaka huo.

Mbali na hao, asilimia 56 ya waliohojiwa walisema serikali zao hazifanyi vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa, ambayo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN) ni moja ya kikwazo kikubwa kufikia malengo ya 2030, ambayo ni kuondoa umasiki, njaa, kuboresha elimu na miundombinu.
FB_IMG_1551278477306.jpg
 

Forum statistics

Threads 1,381,368
Members 526,066
Posts 33,797,453
Top