Wabunge na neno "Ndiyoo" ndio wametufikisha hapa

storyteller

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
1,165
2,000
Najiuliza sana maswali kuhusiana na wabunge waliohusika na kupitisha mikataba yenye ukakasi kwa kupiga kelele za "ndiyooooo"
Wengi wao(bila shaka) hupiga hizo kelele bila hata kujua yaliyomo ndani ya hiyo mikataba, sasa.....
1. Huwa wanaipitisha wakiwa wamepata maslahi binafsi(wamelipwa mmoja mmoja) au
2. Wanapitisha wakisimamia maslahi ya chama(faida ni kwa chama)

Kwa sababu leo tunaona chama kikitumia mwanya ule ule walioutengeneza wao kuji-repear na kuwateka "wapumbavu" wasiofikiri na kupembua ili kujipatia kura za 2020.
Najua wao hawaoni aibu wala kujisikia vibaya kwa kuwa "yeye" keshafaidika na mwizi ni mwizi tu, huwa hafeel chochote ili mradi ye apate anachotaka ndiyo maana hushangai kumuona kiongozi yule yule aloyesimamia upitishwaji wa mikataba hii ya hovyo akisimama na "kujitia" anasikitika kwamba mikataba ilikua ya hovyo.

Sasa kwa hawa wabunge wetu, huwa wanafaidikaje na hizi kelele za "ndiooooo"
 

Freeland

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
14,492
2,000
Eti Ndugai naye analalamika mikataba mibovu kweli..Sheria Mbovu kweli

Anyway wenye matatizo ya uelewa ni sisi wanachi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom