Wabunge na Mawaziri kufundisha vyuoni: Hii imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge na Mawaziri kufundisha vyuoni: Hii imekaaje?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Ng'wanza Madaso, Apr 11, 2011.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Je huku si kutafuta posho za ziada?

  Mwakyembe aomba akafundishe

  Sunday, 10 April 2011
  Habel Chidawali, Dodoma


  NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, ameuomba uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), umpe vipindi ili aweze kutoa mchango wake katika kuboresha taaluma katika chuo hicho.

  Dk Mwakyembe alifanya hivyo juzi kufuatia ombi lililotolewa na Profesa Mark Mwandosya, la kuwataka wabunge na mawaziri wenye uwezo na nafasi ya kufundisha, wafanye hivyo.


  Mwandosya alimtaka Makamu Mkuu wa Udom, Profesa Idrisa Kikula kutumia nafasi ya wabunge wanapokuwa Dodoma kwa ajili ya vikao vyao, kuwaomba waende kufundisha, ili kupunguza pengo la wahadhiri.


  Waziri huyo alisema kwa upande wake, yuko tayari kufundisha katika chuo hicho.Kwa upande wake, Mwakyembe alisema na yeye yuko tayari na kuutaka uongozi wa chuo hicho umpangie vipindi na kwamba ataanza kufundisha Juni mwaka huu wakati Bunge la bajeti, ambapo alisema atakuwa Dodoma kwa muda mrefu.


  Dk Mwakyembe ambaye amekuwa akialikwa katika vyuo vikuu kadhaa duaniani kwa ajili ya kutoa mihadhara, ni mtalaamu aliyebobea katika sheria.


  Kulingana na maelezo yake, somo hilo ndilo atakalokuwa anafundisha Udom.Makamu Mkuu wa Udom Profesa Kikula, alimwagiza Mkuuu wa Idara ya Mafunzo katika Kitivo cha Sheria kuwasiliana mara moja na Dk Mwakyembe, ili kumpatia ratiba ya namna atakayofundisha.


  Kabla ya uteuzi wa nafasi ya Makamu wa rais mwaka jana, Dk Mohamed Bilali alikuwa akifundisha katika chuo hicho.Alikuwa anafundisha Fizikia na wanafunzi walikuwa wanamsifu kwa mbinu za ufundishaji.


  Kwa upande wake, Waziri wa Elimu na Mafunzoya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa alikemea tabia ya wahadhiri wa vyuo mbalimbali nchini, kuhubiri mambo ya siasa vyuoni badala ya kufundisha.


  Dk Kawambwa alisema tabi hiyo imekuwa ikiota mizizi siku hadi siku baadhi ya wahadhili wamekuwa wakidiriki kufundisha hata kwa kutumia mifano ya EPA,Richmond na Dowans.


  Source: Mwananchi
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kama wanajitolea tu (volunteer) haina mbaya
   
 3. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  I dont think if this people are real comrades mbona lwaitama na shivji wanafundisha natunaona impact yao kwenye society waache siasa warudi mavyuoni .ni kweli kuna deficiency na inasababishwa na wao kukimbilia siasa wakati taifa linawahitaji kuboresha elimu .mtazamo wangu tu.
   
 4. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  ni kweli sio mambo ya kulipana tena mishahara miwili miwili la sivyo wachague moja
   
 5. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suala la msingi siyo kulipana mara 2, hapa tuangalie mchango wao ktk kuinua elimu ya watz
   
 6. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  wangekuwa na nia ya dhati ya kuelimisha watanzania wangebaki vyuoni full stop siasa ya nini?
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Uthibitisho mwingine kuwa CCM iko mahututi. Wanaenda kueneza doctrine za u CCM tu hawana lolote.

  too late niggaz!!!
   
 8. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa kuwa hakuna la maana wanalofanya bungeni zaidi ya sanaa katika kipindi cha maswali na majibu, ni bora waende wakafundishe maana taaluma zao ni za ukweli; ilhali nafasi za kisiasa wamepeana bila kujali nani anaweza nini. Mfano Dr. Kawambwa ni mtu wa kubebwa tu, hana la maana analofanya serikalini.
   
 9. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Binafsi nafikiri kwa mbunge kujitolea(volunteer) kufundisha ni sawa,ila kwa waziri mwenye majukumu mengi ni bora akasimamia maendeleo ya Taifa na kusaidia kumshauri Rais. Kuna watu kama Mbunge wa Magu Dr.Festus Limbu, Yule Mbunge Professor wa CHADEMA na wengine wengi,Wakajitolea kufundisha.Na imani kwa ule Muda wawapo mjengoni Dodoma wanafunzi wataambulia walau kitu fulani.
   
 10. k

  kuringe Member

  #10
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mtazamo wangu ni jambo zuri kwa hawa waheshimiwa kufundisha ila napata ukakas kwenye mambo matatu makubwa 1.isije ikawa ni mbinu ya kuuzuia huu moto wa demokrasia ambao kwa kias kikubwa umechochewa na chadema kwa kutumia wasomi wa vyuo 2.kujiongezea ama kujilimbikizia sources za income.3kutengeneza mitandao km iliyopo ambayo imesaidia watu fulan kufanikiwa kwenye malengo yao ya siasa.km haya hayatakua malengo yao basi wanaweza kuwa wazalendo wazuri na tukafaidi uwepo wao na kusomeshwa kwao na kodi zetu ambazo hawarudishi hata kidogo
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  na kama rais hapokei ushauri wao, anapokea wa sofia tu?
   
 12. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bora wakafundishe bure tufidie mishahara mikubwa tunayowalipa na kuishia kulala tu mjengoni....:disapointed::disapointed::disapointed:
   
 13. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  muda watutoa wapi?

  uwaziri ni full time

  ubunge wakati wa vikao ni kutwa nzima (achilia mbali vikao vya kamati mbalimbali na semina za wabunge). baadaya bunge wanatakiwa warudi majimboni kuhamasisha na kusimamia shughuli za maendeleo pamoja na kuhudhuria ratiba za vikao vya madiwani na bodi za maendeleo za mikoa yao

  sasa niambieni, kama sio kujigawa na kuiba muda wao muhimu na adimu, muda wa ziada watutoa wapi? kwa nini wasichague moja kati ya kufundisha au siasa,

  wahenga walisema mshika mbili moja humponyka
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Anaweza kuwa anafundisha.

  Hata kama mchana hana muda, basi anaweza kupanga vipindi hata saa 19hrs hadi saa 22hrs.

  Nakumbuka hata Mpinzani wake jimbo la Kyela, member mwenzetu hapa JF aitwaye Mtanzania AKA Mwakalinga, alishasema kabisa kuwa kama atashinda, basi atatumia muda mrefu anaokuwa Dodoma kama Mwalimu.

  Unaweza usiwe mwalimu Permanent ila ukawa unawaongezea vijana maneno mawili matatu na kuwa na vipindi vya maswali na majibu kwa wanafunzi kukupatia matatizo yao kwenye masomo hayo unayotaka wewe kufundisha. Inakuwa kama Masomo ya Tuitions ila ni for free.
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Ingekuwa vizuri aache kabisa na kuingia chuo, alikwa dar badae akaacha sasa anataka kurudi? Kazi ya siasa siiwezi. Tukumbuke kuwa wanafunzi wengi wa vyuo vikuu vya bongo wanakuwa likizo Juni Septemba. Labda kama watakuwa wameanzisha Trimester system Bongo!
   
 16. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mwaqndosya na kundi lake wanafanya siasa tu; kumbukeni hivi sasa hapo Dodoma watu wanahangaika kutaka kuchaguliwa kuingia kwenye cc ya mafisadi kwa hiyo kila mmoja wao anataka aonekane kuwa ni mzalendo kuliko wengine!! Hilo la kufundisha wanafanya siasa tu kwani wananchi hapo Dar [ pamoja na kule anakoishi Tegeta] bado wana malalamiko chungu nzima kuhusu wizara ya maji na waziri ameshindwa kutatua kero zao!!
   
 17. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Dk ameomba akafundishe UDOM
   
 18. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Wameshaona siasa zao zinaelekea ukingoni wanatafuta ajira ya hapo baadae watakapopigwa chini. SI walisema wanasiasa wasiwe wahadhiri kama niko sawa walimtosa Baregu kwa sababu ya siasa. Sasa wanakuja vyuoni wao kama kina nani. Wamalize biashara zao za siasa then waombe kazi upya wasahiliwe. Tunataka wahadhiri commited si hao walo busy na siasa
   
 19. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Sioni tatizo hata kama akilipwa, sia anafanya kazi mbili kwanini asilipwe?:hat:
   
 20. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mbunge hata kama kuna kikao cha bunge ila yeye ana jambo jingine muhimu anatakiwa kushughulikia muda ule huwa anatoa taarifa na kuruhusiwa kuondoka bungeni. Ndio maana sio wabunge wote huwepo bungeni wakati wa vikao. Hata bunge la uingereza lina viti vichache kuliko idadi ya wabunge na wameliacha hivyo makusudi.
  Hata mawaziri nao huwa mara nyingine wanawakilishwa na manaibu waziri.
  Suala la kuamua kufundisha sio kwamba watashndwa.
  Au kama mdau hapo chini alivyosema kwamba wanaweza wakapewa muda wa kwenda vyuoni wakawa wanajibu maswali ya wanafunzi kuhusiana na somo husika.
   
Loading...