Wabunge na mavazi yao sio jambo katika Taifa la leo

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
108
500
Siku ya jana Spika Ndugai alimtoa nje Mbunge mmoja kwa kosa la kuvaa mavazi anayosema kuwa yapo kinyume na maadili ya Bunge , cha ajabu watanzania wengi wakashikilia hili jambo kama vile lina maslahi yoyote kwa taifa , ikifika mbele mpaka NGO moja ikaandika taarifa ya kulaumu kama vile watanzania wanaishi kwa kutegemea mavazi ya wabunge , social media na baadhi ya wanaharakati wameshikilia hilo jambo kama vile lina maana yoyote kwa maisha ya mtanzania wa leo.

Wengine wanasema ni haki za binadamu najiuliza yaani katika maisha ya mtanzania wa leo ndio wakumpelekea jambo juu ya mavazi ya mbunge ambaye halipi hata kodi katika mshahara wake wa ubunge , mbunge ambaye anapokea malupulupu kushinda hata mfanyakazi wa serikali anayefanyakazi miaka zaidi ya thelathini , yani leo mbunge mmoja aliyetamani matako ya mbunge mwenzake na kumsemea kwa spika wakati sio kazi yake yaani huu upumbavu wa wabunge leo hii ndio jambo la kutusumbua katika akili zetu , tunaacha kujadili mambo ya maana , tunajadili juu ya spika huyu huyu kigeugeu kumfukuza huyo , yani ndio tumechoka kiasi hichi.

Kwa maisha ya leo ya mtanzania mtu kama mbunge anafaida gani kwa mfano ambapo zaidi ya kutoa umbeya tu na kudemka kishambashamba , waandishi wa habari hacheni kujadili vitu visivyo na ajenda ya maana , tuwaulize nyie NGOs ina mana hakuna jambo la kujadili katika haki za binadamu mpaka kumpa kiki mbunge wa kupita tu anayeangalia maisha yake, aasiyelipa hata kodi huu ni ujinga.

Yaani watu wanakaa na kujadili mbunge aliyevaa suruali , yani kodi zetu tunazowalipa bila wao kulipa kodi alafu bado tunakaa kumjadili huyohuyo , ambaye hana faida yoyote katika maisha yetu.

Kweli tunafikia hapa.
 

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,532
2,000
Sawa kuanzia leo waende hata uchi poa tu. Kama huyu hapa.
IMG_20210526_195923.jpg
 

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,532
2,000
Au mleta uzi unataka wavae hivi? Hivi unajua akili za wadangaji kina Magige? Wataingia na bikini
IMG_20210521_102521.jpg
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,125
2,000
Wabunge vijana hujifunza kutoka kwa viongozi wao waonekanapo katika sehemu mbalimbali. Kama "dressing code" ipo katika kanuni za kibunge, Je! Kanuni hizo zipo kwa kutumia kigezo kipi kuhusu uvaaji mavazi ya staha kwa mbunge awapo bungeni ambazo ni tofauti na matumizi yake sehemu nyingine nje ya Bunge?
IMG-20210602-WA0040.jpg
 

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,098
2,000
Wabunge vijana hujifunza kutoka kwa viongozi wao waonekanapo katika sehemu mbalimbali. Kama "dressing code" ipo katika kanuni za kibunge, Je! Kanuni hizo zipo kwa kutumia kigezo kipi kuhusu uvaaji mavazi ya staha kwa mbunge awapo bungeni ambazo ni tofauti na matumizi yake sehemu nyingine nje ya Bunge? View attachment 1806153
Tusubiri muongozo wa Naibu Spika kama alivyoahidi.
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,254
2,000
What is your point exactly?

Mwanzo mwisho unalalamika tu na kulaumu watu wanaojadili halafu wewe huyo huyo unalianzishia mada jambo lilelile ili sisi washamba wako tujadili.

It's ridiculous, right?

Ungekuwa specific kwenye hoja yako badala ya kulalamika na kulaumu tu mwanzo mwisho, ingekuwa akili sana...

Umelaumu mpaka social medias kutumika kama medium of communication kujadili ishu hiyo na wewe huyo huyo unatumia social media kulijadili.

It's ridiculous, right?

Kwa hili, nakuuliza tena; what's your point exactly in this issue ili tujadili?

Au unataka watu waanze kutukana na kulalamika kama wewe?
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,210
2,000
Mkuu SOPINTO hongera kwa kuwakilisha hoja yako kwa ufasaha.

Tatizo la msingi, dunia ya sasa, ni nguvu ya kalamu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Dunia ya sasa kwa kiasi kikubwa inaongozwa (maamuzi ya viongozi wengi na wafuasi wao) na tasnia ya habari.

Suala la huyo Mbunge lilikuwa la Kikanuni za Bunge. Mtoa hoja na Spika walilizungumzia vizuri. Baada ya hapo likakuzwa maradufu na wanahabari na kudakwa kwenye mitandao ya kijamii. Pamoja na kwamba siyo mara ya kwanza Wabunge kutolewa nje kwa sababu mbalimbali ikiwa na hilo la mavazi, lakini kwa kuwa lilihusu vazi tena la Mbunge mwanamke, likapokelewa isivyo kawaida. Kilichomponza ni umbile lake na si vazi - evil minds
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,078
2,000
Huwezi kumtazama mbunge wa kike kama upo na watoto wako kwenye Tv maana watoto na mama watoto wataacha kuangalia TV wakuangalie wewe unangalia nini kwenye TV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom