Wabunge na kaunda suti za vifua wazi

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
wakuu mimi sio mwanasiasa na kamwe sipendi kuwa mwanasiasa,
lakini kuna kitu kinanishangaza kuhusu wabunge wetu kuvaa kaunda suti na kuacha vifua wazi,jamani sioni kama ni jambo la busara kuvaa vile,hivi unajua nchi za wenzetu wakiona wanashangaa sana?
je ni halali kuvaa vile?je lile vazi linaitwaje?je kwa nini wasivae suti na tai kwa heshima?
 
Mi nadhani tukianza kufuatilia kila mtu avae nini bungeni haitakua sawa.. Wavae wanachopenda ili mradi mavazi yao yasiwe kinyume na sheria za bunge na zisitudhalilishe wananchi kwa njia yoyote ile. Mbona uingereza (kama nimekosea nisahihishwe) judges wao wanavaa kama "wigs o kofia" fulani hivi za ajabu watu tunawashangaa but ndio utamaduni wao!
 
mkuu nia yangu ni kuficha kifua hadharani,hata shati likivaliwa ofisini tunafunga mpaka kifungo cha mwisho
 
Kwa kweli mimi pia huwa zinaniboa! Hivi na zile vest huwa wanamuonyesha nani? Nijuavyo mimi vest ni nguo ya ndani...kama ch**i hivi itakuwa sawa kama Mbunge mwanamke mmoja akavaa blouse na kuacha vifungo wazi na kuonyesha bra yake au shingo ya nguo yake ikawa imekatiwa chini na hivyo kuonyesha Bra yake. Inatia kinyaaaa! sijui ni ushamba au zile fashion za kuigana? Ikiwa unataka kuvaa hivyo basi tafuta vest yenye mkato wa v ili iendane na mkato wa kijikaunda suti chako. Hivi viongozi huwa hawana sessions za dressing?
 
Tupozungumzia maadili ya kitanzania,hatuwezi kuyatenga mavazi na namna ya kuvaa.Kukaa kifua wazi kwenye hadhara ya watu ni ukiukaji mkubwa wa maadili ya kitanzania. Waheshimiwa hawa hawanabudi kuacha kuvaa mavazi hayo kama kweli niwasikivu na wenye nia njema na Tanzania yetu.
 
unakuta mbaba kavaaa sut/shat vifungo viwili waz ahhhh inaboa.....UNAONA MANYWELE TU yamechachamaaa kifuani pale...mengne yana mvi mengne yana rangi ya njano ...bluuu..ahh nataman niingize mkono niyavuteeeeeeeeee akome!!!!!!!
 
Jamani si garden love hizo wanawavutia wadada! muwapende zaidi
 
wakuu mimi sio mwanasiasa na kamwe sipendi kuwa mwanasiasa,
lakini kuna kitu kinanishangaza kuhusu wabunge wetu kuvaa kaunda suti na kuacha vifua wazi,jamani sioni kama ni jambo la busara kuvaa vile,hivi unajua nchi za wenzetu wakiona wanashangaa sana?
je ni halali kuvaa vile?je lile vazi linaitwaje?je kwa nini wasivae suti na tai kwa heshima?

Baadhi wanaacha vifua wazi ili uone mikufu yao ya dhahabu waliyovaa. Lakini hata mimi huwa sidhani kama ni sahihi kuvaa suti na kuacha vifua wazi.
 
Kwa kweli mimi pia huwa zinaniboa! Hivi na zile vest huwa wanamuonyesha nani? Nijuavyo mimi vest ni nguo ya ndani...kama ch**i hivi itakuwa sawa kama Mbunge mwanamke mmoja akavaa blouse na kuacha vifungo wazi na kuonyesha bra yake au shingo ya nguo yake ikawa imekatiwa chini na hivyo kuonyesha Bra yake. Inatia kinyaaaa! sijui ni ushamba au zile fashion za kuigana? Ikiwa unataka kuvaa hivyo basi tafuta vest yenye mkato wa v ili iendane na mkato wa kijikaunda suti chako. Hivi viongozi huwa hawana sessions za dressing?

Kwa ufupi kuvaa suti ukaacha vesti ionekana hakuna tofauti na vijana wa kileo wanaoning'iniza suruali zao na kuonesha nguo zao za ndani. Hii ina maana maadili nchi hii kwishney kuanzia kwa vijana wadogo mpaka kwa mibabu yenye umri mkubwa na ambayo ina nafasi za uongozi wa juu.
 
Ni ukosefu wa adabu. Licha ya kuvaa mivifua wazi , wewe anagalia hata wakila chakula mezani, na mabaya zaidi nyama choma. Kwa ufupi hawana elimu ...at equate, good manners, etc. Wengine wanatoka vijijini ati. Do not take them too serious
 
si ndo maana ikaitwa kaunda suit tai ya nn tena?
wakuu mimi sio mwanasiasa na kamwe sipendi kuwa mwanasiasa,
lakini kuna kitu kinanishangaza kuhusu wabunge wetu kuvaa kaunda suti na kuacha vifua wazi,jamani sioni kama ni jambo la busara kuvaa vile,hivi unajua nchi za wenzetu wakiona wanashangaa sana?
je ni halali kuvaa vile?je lile vazi linaitwaje?je kwa nini wasivae suti na tai kwa heshima?
 
....tuataishia kujadili tuvae nini bungeni wenzetu wanapiga hatua kimaendeleo.

Na mnapoongelea utamaduni wa kitanzania,ni nini hasa mnaongelea!Hivi,just wondering,kama mtu akiingia na vazi la kimasai bungeni,mtamwambiaje?Au akivalia msuli wa kiswahili je itakuwaje?Nini hasa huu utamaduni mnaoongelea?wa kuvaa suti?toka lini utamaduni wa kitanzania ukawa kuvaa suti?

Kama mtu hajaingia uchi,basi yote heri tu.kinachotakiwa ionekane kazi inayofanyika,na wala sio vazi alilovaa.Kazi hiyo tuwaachie uwazi.
 
Jamani tusilalamike sana. Watanzania wengi nguo tunazijuwa juzi juzi tu. Nakumbuka mwaka 78 nikipita njia ya Arusha kwenda Singida, vijana mpaka wa miaka 14-15 wako uchi kabisa wa mnyama.

Wengi wa wana JF, hususan wale waliotoka vijiji vya mbali na miji, sitoshangaa kusikia kuwa hata wao nguo wameanza kuvaa wakisha balehe.

Hawa Wabunge wetu wengi tu, na si wabunge pekee, hata maofisini, mitaani utakuta watu hawana kabisa sense ya nguo ipi ivaliwe wapi.

Tusijilaumu, utamaduni wa nguo ni wa watu wa Pwani, huwezi kumkuta Mbunge wa Pwani akavaa hovyo hovyo, huo ni ukweli usiopingika.

Hata Pinda siku anateuliwa kuwa Waziri Mkuu, alikuwa bungeni na ki Kaunda suit chake kifua wazi, mfulana wa ndani unaonekana. Inakera sana.
 
unakuta mbaba kavaaa sut/shat vifungo viwili waz ahhhh inaboa.....UNAONA MANYWELE TU yamechachamaaa kifuani pale...mengne yana mvi mengne yana rangi ya njano ...bluuu..ahh nataman niingize mkono niyavuteeeeeeeeee akome!!!!!!!
<br />
<br />
MMMM UYAVUTEEE AU UYAPAPASE? KUMBE NA HAWA KINA BABA WANAKAAGA NUSU U CHI EEE AF KILA MARA WANATUSEMA SIE LOOOL
 
Back
Top Bottom