Wabunge mngejadili uwezekano wa kuwa na ukomo kwenye mikataba ya kazi kulingana na maslahi yanayopatikana

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
33,566
2,000
Ningependa siku moja nisikie mkijadili kuhusu kuleta miswaada ya jambo hili.

Katika mfumo wa ajira kuwe na ukomo kwenye mikataba ya kazi tu kulingana na maslahi yanayopatikana.

Wenye mishahara inayozidi 6M+ ndani ya miaka 5 wastaafishwe kwa manufaa ya umma wapishe intake nyengine. Wale wenye mishahara ya 2M-4M wapewe miaka 7!

Wenye mishahara chini ya hapo wapewe ukomo wa 10 years.

Hii itasaidia Graduates wakapate uzoefu katika taaluma zao na kujipatia mitaji katika miaka watakayokuwa kazini. Wakitoka ni aidha waunganishe mitaji waanzishe viwanda. Au kila mtu afanye uzalishaji binafsi.

Kwa mawazo yangu ndio naona ni namna pekee ya kufuta umaskini nchini na kuondosha tatizo la ajira.
 
Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
11,498
2,000
Haliniingii akilini kwa sababu kila mara kutakuwa na staff wapya ubobezi na uzoefu serikalini ungepotea.

WAJADILI NI NAMNA GANI SERIKALI ITABUNI MBINU ZA KUKUZA SECTOR BINAFSI ILI WAHITIMU WENGI WAPOKELEWE SECTOR BINAFSI.
 
Kelevra

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
1,057
2,000
Watakwambia ooh! si unajua mambo ya expirience na nini.
Halafu tutawajibu kila kitu kina first day.
 
DA HUSTLA

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
2,035
2,000
Ukianza na mshahara chini ya million 2 baada ya muda ukapata zaidi ya million nne, hapo calculation ya muda inakuaje...isije kuwa ukianza na kazi ya chin ya million 2 ,ile unapata kazi zaidi ya 6m unastaafu baada ya mwez
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
33,566
2,000
Haliniingii akilini kwa sababu kila mara kutakuwa na staff wapya ubobezi na uzoefu serikalini ungepotea.
WAJADILI NI NAMNA GANI SERIKALI ITABUNI MBINU ZA KUKUZA SECTOR BINAFSI ILI WAHITIMU WENGI WAPOKELEWE SECTOR BINAFSI.
Mkuu miaka 5 sindio ambayo inaandikwa kwenye job description nyingi tu! Iweje leo ionekane tena haitoshi kwa uzoefu?

Je, hawa graduates wanaoambiwa wakajiajiri kwao hio experience huwa mnaizingatia?
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
33,566
2,000
Ukianza na mshahara chini ya million 2 baada ya muda ukapata zaidi ya million nne, hapo calculation ya muda inakuaje...isije kuwa ukianza na kazi ya chin ya million 2 ,ile unapata kazi zaidi ya 6m unastaafu baada ya mwez
Unapataje ongezeko la ghafla namna hio? Ni kwa scale gani? Maana mshahara unaongezekaga kwa elfu 50/50 tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!

Anyways ukomo wako ni according na mshahara ulioanza nao tu! Sio increment.
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
33,566
2,000
Watakwambia ooh! si unajua mambo ya expirience na nini.
Halafu tutawajibu kila kitu kina first day.
Jibu lipo rahisi, wanapoandika job description zao wanataka 5 yrs, 7yrs ama zaidi sindio miaka hio hio ina correspond na ukomo!
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
33,566
2,000
Hili ni zuri sana kuwepo na ukomo katika kila sekta hata kwa wabunge piambunge akishatumikia wananchi kwa miaka 10 inatosha sana japo hapa watachukia sana :D :D :D :D
Hao hamuwaambii maana mkisema nao wawe na ukomo hawatakubali hata kupitisha huo mswaada!

Wao mnawaacha tu wakae free! Mnawaadhibu jimboni tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom