Wabunge mnaohama vyama kabla ya bunge kuvunjwa mnapoteza haki zenu

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,685
22,694
Kuna ujinga unaendelea kwenye siasa za Tanzania, kuhama hama vyama kwa sababu ya maslahi binafsi huku kule wanapokimbilia hawana hakika napo kama watapewa nyadhifa, kwa kifupi wanacheza kamari maana wanapoteza walichokitumikia kwa muda mrefu huku hawana uhakika na wanachokitarajia huko wanakohamia!
 
Wasingeweza kuhama wapoteze zaidi ya milioni 100 zilizotayari kuingia kibindoni kama siyo rushwa. Hili ni jambo linalokera sana kwenye utawala wa Pombe. Watu wanajiuliza iweje apigane na rushwa kwa nje wakati matendo yanayofanyika ndani yanaakisi rushwa iliyokubuhu?
 
Kuna ujinga unaendelea kwenye siasa za Tanzania, kuhama hama vyama kwa sababu ya maslahi binafsi huku kule wanapokimbilia hawana hakika napo kama watapewa nyadhifa, kwa kifupi wanacheza kamari maana wanapoteza walichokitumikia kwa muda mrefu huku hawana uhakika na wanachokitarajia huko wanakohamia!
hakika inatia aibu maana ujinga ni mwingi sana mpaka inasikitisha kuina mtu mzima na akili zake tena ana mke na watoto anavyotangatanga kisa pesa.
 
Kuna ujinga unaendelea kwenye siasa za Tanzania, kuhama hama vyama kwa sababu ya maslahi binafsi huku kule wanapokimbilia hawana hakika napo kama watapewa nyadhifa, kwa kifupi wanacheza kamari maana wanapoteza walichokitumikia kwa muda mrefu huku hawana uhakika na wanachokitarajia huko wanakohamia!

Mawazo yako yanaonekana hujui ulisemalo,, hakunaga mwanasiasa mjinga isipokuwa watawaliwa ndio huwa wajinga ama werevu.

Sasa jitathimini upo kundi gani (mjinga au mwerevu) ,,,japo kwa hoja yako ushajulikana upo kundi gani :)
 
Haha mkuu hajui mtawaliwa ndio bwege mwenzako anakula vinono kwa kura yako eti unamwmita mjinga kivipi unafikiri unahama tu bila faida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawazo yako yanaonekana hujui ulisemalo,, hakunaga mwanasiasa mjinga isipokuwa watawaliwa ndio huwa wajinga ama werevu.

Sasa jitathimini upo kundi gani (mjinga au mwerevu) ,,,japo kwa hoja yako ushajulikana upo kundi gani :)
mimi naweza kukubali kuwa mjinga lakini wewe nakuweka kwenge kundi la wapumbavu....
 
Ingekuwa sheria zinafuatwa wangekosa haki zao, ila siku hizi sheria zinaangalia rais anataka nini. Hivyo hao wabunge waliojiuzulu upinzani na kwenda ccm watalipwa mafao yao yote bila tatizo lolote. Sheria sasa hivi zina macho, kisha nashangaa eti Takukuru wanaitisha mkutano wa wanahabari kupiga porojo ili waonekane wanachapa kazi.
 
Kwa serikali hii lolote linawezekana huenda wamehakikishiwa kupata haki zote na nafasi ya kurudi tena
Kuna ujinga unaendelea kwenye siasa za Tanzania, kuhama hama vyama kwa sababu ya maslahi binafsi huku kule wanapokimbilia hawana hakika napo kama watapewa nyadhifa, kwa kifupi wanacheza kamari maana wanapoteza walichokitumikia kwa muda mrefu huku hawana uhakika na wanachokitarajia huko wanakohamia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasingeweza kuhama wapoteze zaidi ya milioni 100 zolizotayari kuwa kibindoni kama siyo rushwa. Hili ni jambo linalokera sana kwenye utawala wa Pombe
Hizo hela zinatoka mfukoni kwa nani na ni nani anawalipa....
 
Kuna ujinga unaendelea kwenye siasa za Tanzania, kuhama hama vyama kwa sababu ya maslahi binafsi huku kule wanapokimbilia hawana hakika napo kama watapewa nyadhifa, kwa kifupi wanacheza kamari maana wanapoteza walichokitumikia kwa muda mrefu huku hawana uhakika na wanachokitarajia huko wanakohamia!
Umeandika nini? Hivi hiki ulichoandika utamshawishi nani? By the way, hivi ile kauli mbinu yenu ya "Toroka Uje" iliishia wapi? Ahahahahaha!!
 
Wewe this is bongo bhana, kiinua mgongo cha after five years lazima wapokee. Ni kama wale madiwani tu , walijiuzuru na kuhamia chama baba lao lakni vkao vya bajeti wakauzulia.
 
Back
Top Bottom