Wabunge: Mitambo TANESCO ilindwe na JWTZ, JKT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge: Mitambo TANESCO ilindwe na JWTZ, JKT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 31, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMANNE, JULAI 31, 2012 06:25 NA MAREGESI PAUL, DODOMA

  *Yadaiwa mafisadi wanajipanga kukata umeme
  *Washtukia walinzi wa makampuni binafsi

  WABUNGE wamechachamaa. Kuanzia sasa wanataka mitambo ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na vyanzo vyote vya umeme, vilindwe na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na askari polisi.

  Mapendekezo hayo, yalitolewa bungeni jana na Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora (CCM) na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), baada ya kuwapo taarifa kwamba, kuna watu wanajipanga kuifanyia hujuma mitambo hiyo ili umeme usipatikane.

  Lugora na Mbatia, walitoa mapendekezo hayo walipoomba mwongozo wa Spika, kwa nyakati tofauti kuhusu usalama wa shirika hilo la umeme.

  Aliyekuwa wa kwanza kuomba mwongozo wa Spika ni Lugora, ambaye alisema kuna taarifa za mafisadi kuandaa mikakati ya kuihujumu TANESCO kama njia ya kukwamisha jitihada za Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na manaibu wake, Slyvester Masele na George Simbachawene.

  "Mheshimiwa Naibu Spika, nasimama hapa kwa kutumia Kanuni ya 68 (7) ambayo inaruhusu mbunge kusimama wakati wowote wakati ambao hakuna mbunge mwingine anayezungumza.

  "Mheshimiwa Naibu Spika, juzi Jumamosi wakati Waziri wa Nishati na Madini akihitimisha mjadala wa hotuba ya bajeti yake, alilihakikishia Bunge na Watanzania wote, kwamba mgawo wa umeme ambao tumekuwa tukikumbana nao ulikuwa ni wa kuumba.

  "Waziri alituhakikishia kuwa, kulingana na hatua alizochukua, kuanzia sasa mgao wa umeme utakuwa ni wa historia.

  "Lakini kwa kuwa suala la mgawo wa umeme ni zito na kwa kuwa uamuzi wa Spika wa kuvunja Kamati ya Nishati na Madini siyo suluhisho na kwa kuwa kuwasimamisha watendaji wa TANESCO pia siyo suluhisho na pia uamuzi aliosema Waziri atavunja bodi ya TANESCO siyo suluhisho.

  "Sasa ninazo taarifa kwamba, baada ya waziri na manaibu wake kuvunja mirija ya ulaji TANESCO, sasa mafisadi wanajipanga kufanya hujuma nje ya Bunge kwenye gridi ya taifa na mitambo yote ya TANESCO ili umeme wa uhakika usipatikane kama waziri na manaibu wake walivyoahidi.

  "Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mitambo ya TANESCO inalindwa na walinzi wa makampuni ya kawaida wenye filimbi na virungu na kwa kuwa nchi nyingine duniani wanajeshi na polisi ndio wanaolinda mitambo kama hiyo, kwa nini sasa na sisi tusiimarishe ulinzi kwa kuwatumia askari wa majeshi hayo?

  "Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mwongozo wako katika jambo hili kwa sababu baadhi ya vyanzo vingine vya umeme viko porini," alisema Lugora.

  Mbunge huyo, alipomaliza zamu yake, ilikuja zamu ya Mbatia ambaye aliunga mkono hoja ya mbunge mwenzake huyo, akitaka Bunge, liiagize Serikali ipeleke askari hao katika mitambo yote ya TANESCO.

  "Mheshimiwa Naibu Spika na mimi natumia Kanuni ya 68 (7) aliyotumia Mheshimiwa Mbunge wa Mwibara.

  "Mheshimiwa Naibu Spika, siku zote kinga ni bora kuliko tiba na tishio hili linafanya hali iwe tete kwa sababu ufisadi ni mfumo na kuufumua kwa kauli siyo suala jepesi.

  "Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa JWTZ wapo na moja ya kazi yao ni kuwalinda wananchi, tusichelewe kuiagiza Serikali ianze kuwatumia wanajeshi na JKT.

  "Uamuzi huu, tuutoe sasa tusichelewe tena na pia Waziri wa Nishati na manaibu wake nao wapewe ulinzi, Mheshimiwa Spika naomba mwongozo wako tusingoje kesho," alisema Mbatia.

  Akizungumzia miongozo hiyo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema ataitolea ufafanuzi jioni (jana), baada ya kupata ushauri zaidi.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Unaona MAFISADI hawana MOYO na Rasilimali za NCHI YAO? Ndio Mapendekezo ni kuwa wewe FISADI Umeshikwa na

  UFISADI then USHAHIDI UPO - ADHABU ni KUNYONGWA.

  Tutaisitiri nchi yetu toka kwenye Makucha ya MAFISADI; Wamejipenyeza kila kona, hadi ndani ya sebule zetu...
   
 3. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kuwanyonga lazima warudishe senti ya mwisho waliyotuibia.

  "Kifo" cha Balali kwani kiliturudishia mali zetu? Death penalty just after 99% recovery.
   
 4. mito

  mito JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,624
  Likes Received: 2,012
  Trophy Points: 280
  Mkuu umekumbuka kuweka wazo lako hilo (in red) ktk orodha ya maoni yako kwenye tume ya kurekebisha katiba? mi nilishaweka hilo pamoja na la biashara ya madawa ya kulevya, kama wanavyofanya China
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  kwana mafisadi wanaiba hardware?
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi zama za Nyerere unaweza fanya huu us.................ngee!
  Ivi hawa watu ni timamu kweli mnataka subotage umeme wetu!
  Kheri China ambako hawa watu hunyongwa
   
 7. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Lakini tukiwa na watu ndani ya nchi tunawaogopa basi tuna tatizo kubwa. Tunayo sheria dhidi ya ugaidi, wakamatwe na washitakiwe chini ya sheria ya ugaidi. Au ugaidi ni mpaka uharibu mali za Marekani?
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Yeah, nitaweka hilo tume ikinifikia sababu hata Mwakilishi wa Zanzibar aligusia suala la hao MAFISADI ambao wako

  Serikalini wanajua siri za serikali yetu wanatumia hizo loopholes kuwazulumu wananchi Rasilimali zao kuwa ni

  KUWANYONGA sababu hawajali sasa angalia bado wanataka kudhuru mitambo ya UMEME ili tuwe na GIZA ili wapate

  Mamilioni ya pesa...
   
 9. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #9
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  tatizo haliko tanesco tatizo liko ikulu ni bora harakati zielekezwe huko kuilinda ikulu.mungu ibariki tanzania.
   
 10. mito

  mito JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,624
  Likes Received: 2,012
  Trophy Points: 280
  Mkuu huna haja ya kusubiria tume ikufikie, hiyo ya kufikiwa ni kwa wale wasio na access na internet, wewe na mimi (tunao-access internet) tunaweza kutoa maoni yetu kwa kutembelea hapa Tume ya Mabadiliko ya Katiba au unaweza kutuma kwa barua pepe kwenye maoni@katiba.go.tz
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Yeah, Nyerere pamoja na sisi kumuita mbaya alikuwa anatueleza mabaya yetu...

  sasa Rais Kikwete hatuambii mabaya yetu, anatuacha tunafanya tutakavyo hakuna sheria inayowalinda wananchi dhidi

  ya hao viongozi aliyewateua, na hao viongozi hawakemei hata kidogo; ndio Maana kila mtu sasa anadai haki zao kivyake

  Madaktari Wanagoma - Pesa zipo Viongozi hawajui Jinsi ya kuongea kinadharia; Waalimu Wanagoma; Waislamu - wa

  Pwani Wanagoma kuhesabiwa Sababu ya Kipengele cha DINI - Viongozi hawajui jinsi ya kuongea nao Kinadharia yaani

  Hii issue ni ya Miezi hatujasikia Rais akiongea nao kimya kimya; kuonyesha heshima... Ni Maredioni...

  Lakini tunasikia UTUMBO WA MAFISADI kila leo ya KUTISHA
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hivi serikali ya Tz imefikia kiwango chakuwaogopa mafisadi kwakuwachukulia hatua mpaka kuamua kulinda mitambo? Usalama wa taifa unafanya kazi gani isichunguze na kuwachukulia hatua hawa wanaotaka kulipua hiyo mitambo? Inamaana hao mafisadi wapo juu ya sheria? Nazidi kuamini hii serikali nh dhaifu, legelege na isiyojitambua na inajiendesha bora liende na liwe na liwalo
   
 13. D

  Davie Member

  #13
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni upuui wa hali ya juuu...kila siku serikali na mafisadi..hao mafisadi ni akina nani..?na kwanini wasikamatwe na wakawajibishwa..?
  umekuwa ni mchezo wa ajabu kila siku..mafisadi wamefanya hili...mafisadi wamefanya lile....nk..
  kama wanafahamika kwanini wasichukuliwe hatua..
  ni ujinga kila siku tunaongelea kitu hichohicho...

  tnapotezeana muda sana kwa hii kitu...watumishi hao wa serikali ndo mafisadi wenyewe..
   
 14. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Naona hii singo ya Muhongo na Maswi imekolea kweli kila mtu anaicheza!
  Ati hakuna mgao ila "mafisadi" wanahujumu...
  Ati tanesco inaingiza bil 60 kwa mwezi na matumizi bil 11 hizo nyingine wanakula..
  Wadanganyika tumeshasahau mabilioni yanayopotea kwa kuendekeza hii mikataba ya kijambazi ya umeme wa "majenereta"!!
  Subirini hilo wese la puma likiisha na kiangazi ndo hicho kinakuja mtera maji yanapungua....tuone kama hii singo yao itaendelea!
  Ama kweli sisi "miafrika ndio tulivyo"!
   
 15. m

  mharakati JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  udhaifu wa Amiri mkuu wetu umewafanya mafisadi na ufisadi kua adui namba moja wa usalam wa taifa letu..huu mi naona ni sawa na uhaini sasa, sabotage huduma za jamii na, au za kiuchumi kwa manufaa binfasi au kwa kumfanya rais aonekana ameshindwa zaidi kazi ni uhaini na ugaidi.
   
 16. African American

  African American Senior Member

  #16
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa rais wetu mpendwa Jakaya Mrisho Kikwete, ninaomba kwa heshima uniteue kuwa pm kwa muda wa wiki mbili tu!sitaki zaidi mkuu. Hakuna haja ya kuwasumbuwa walinzi wetu wa mipaka JWTZ. Ninakuahidi kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba kwa utii na uaminifu, nitawakamata mapapa wote wanaohujumu uhai wa taifa hili na kuwashughulikia ipasavyo. Asante Mh JK natarajia kwa maslahi ya taifa utanipa nafasi nikusaidie.

  Wako mtiifu
  AA
   
 17. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hata tukiwa na walinzi wanajeshi lakini kama mafisadi wana nia ya kuhujumu hiyo mitambo bado watafanya tu. Itakuwaje hao wanajeshi wakipewa oda na mkuu wao kuruhusu hujuma kufanyika?. Kwani pesa ya EPA ilichukuliwa kinguvu kwa kuvunja benki kuu?.

  Dawa pekee ni kwamba watanzania wote tunatakiwa kubadilika na kuipenda nchi yetu kwa dhati. Tuwe na uchungu na nchi yetu, tuwe wazalendo wa kweli.
   
Loading...