Wabunge, mawaziri Tanzania kuchagua uongozi au biashara

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,890
Ana nia kweli ya kulifanya hili au ni usanii mwingine? Karamagi, Mkono na mawaziri na wabunge wengine wengi wa CCM mpo?

Posted Date::1/31/2008
Wabunge, mawaziri Tanzania kuchagua uongozi au biashara
Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete amewataka wafanyabiashara ambao ni wabunge na mawaziri kujiandaa kuchagua kimoja kati ya biashara au uongozi serikalini

Akizungumza jana katika utaratibu wake wa kila mwezi jana, Rais Kikwete aliwataka kuchagua jambo moja kati ya uongozi au biashara ili wasiendelee kuondokana na mwingiliano wa kimaslahi.

"Viongozi wetu wachague kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ama biashara au ubunge na Uwaziri. Kwa ajili hiyo ni makusudio yangu kuanzisha mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Uongozi ili tuingize utaratibu huo," alisema kuongeza.

"Ni jambo lenye maslahi kwa nchi yetu na litasaidia sana kujenga heshima ya viongozi wa umma mbele ya macho ya wananchi. Nafurahi kwamba suala hili tumelizungumza katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM tulichofanya Dodoma juzi Januari 29 na tumeelewana."

Alisema upo ushahidi wa kutosha wa kuwapo migongano ya maslahi kwa baadhi ya viongozi hao wa kisiasa suala linalosababisha wananchi kukosa imani na serikali.

Akitoa mfano wa mataifa yaliyoendelea alisema kuwa mataifa hayo yanao utaratibu unaomtaka mtu mwenye shughuli za kibiashara anapokuwa Mbunge au Waziri kuacha kujishughulisha na biashara zake na kwamba unakuwepo utaratibu rasmi unaotambuliwa kisheria wa wadhamini wanaoendesha hizo shughuli bila ya yeye kujihusisha nazo.

Akizungumzia suala la uhamiaji haramu nchini alitoa siku sitini za kwa wahamiaji haramu kujisalimisha. Baada ya hapo hatua zipasazo za kisheria zitachukuliwa kwa wale ambao watakuwa hawa kufanya hivyo.

Alisema kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kushuhudia mambo yasiyokubalika yakitendeka wakati akiwa kwenye ziara ya siku kumi Mkoani Kagera ambapo alikuta ukiukwaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na uingizaji mifugo nchini.

Alisema kwa muda mrefu sasa, raia wa nchi jirani zinazopakana na Mkoa wa Kagera wamekuwa wakiingia na kuishi nchini kwa vibali vya viongozi na watendaji wa vijiji na kata. Baadhi ya watu hao pia wamekuwa wakiingiza mifugo kwa vibali vya viongozi hao hao.

Suala hilo alisema halikubaliki kwani kwa mujibu wa sheria na taratibu za uhamiaji zinatoa mamlaka hayo kwa Maafisa Uhamiaji tu na si vinginevyo na kuwa viongozi na watendaji wa vijiji na kata hawana mamlaka hayo.

Hivyo alisema, vibali vyote walivyotoa viongozi hao si halali na havitambuliki na akapiga marufuku kwa kiongozi au mtendaji wa ngazi yoyote ile nchini kutoa kibali cha mgeni kuingia au kuishi nchini kama siyo Afisa wa Uhamiaji.

"Nilipokuwa Mkoani Kagera niliwaagiza Mkuu wa Mkoa na wakuu wa wilaya kufuatilia utoaji wa vibali unaofanywa na viongozi na watendaji wa vijiji na kata katika maeneo yao.

Nimewataka wawachukulie hatua zipasazo za kinidhamu watumishi hao wa umma pamoja na kuwabana wahamiaji haramu kufuata sheria za uhamiaji za nchi yetu au warudi makwao. Napenda kusema kuwa maagizo hayo ni kwa wakuu wote wa mikoa na wilaya nchini," alisema.

Sambamba na hilo pia ameiagiza Wizara ya Maendeleo ya Mifugo kutoa mwongozo wa jinsi ya usafirishaji mifugo kwa kuwa uvushaji unaoendelea sasa unaweza kusababisha hatari kubwa ya magonjwa ya milipuko kwa mifugo.

Pia alizungumzia la upandaji wa bei ya mafuta duniani akataka wananchi kuwawaangalifu na hasa wabanifu katika matumizi ya mafuta na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.

Alitaka juhudi za kuzalisha nishati mbadala kutokana na mimea hususan miwa, mawese na mbono-kaburi (jatropha) ziongezwe ili kama zikifanikiwa zisaidie kupunguza mzigo wa mafuta yanayoagizwa kutoka nje.

"Nafurahi kwamba juhudi zetu zina muelekeo mzuri na katika miaka michache ijayo tutaanza kunufaika na matunda yake. Pamoja na hayo tunaendelea na juhudi za utafutaji wa mafuta na gesi asilia hapa nchini,"alisema.

Kuhusu Uchunguzi wa Akaunti ya EPA alisema Serikali imedhamiria kulifuatilia suala hilo mpaka mwisho wake ambao utakuwa na maslahi kwa taifa.

Akawashukuru Watanzania kwa kuunga mkono hatua alizochukua na anazoendelea kuchukua kuhusu suala la Benki Kuu. Hata hivyo, alieleza kusikitishwa na taarifa anazozipata kuhusu kuwepo uvumi mwingi unaoenezwa na baadhi yetu kuhusu suala hilo.

Hivyo akakemea wale wote wanaoeneza uvumi na uongo kuacha kufanya hivyo na akawasihi wananchi wawe watulivu na wavumilivu.

"Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe na subira. Naamini kazi hii itakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita tuliyowapa. Napenda kurudia ombi la Serikali kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia katika uchunguzi na hatua katika suala hili waisaidie kamati yetu hiyo," alisema.

Akizungumzia ziara ya Rais George W. Bush wa Marekani katikati ya mwezi Februari, 2008 aliwataka wananchi wampokee kwa mujibu wa desturi na ukarimu wa Kitanzania kwani ujio wake unakuja na neema nyingi tofauti na uvumi unaoenezwa kuwa anakuja kuanzisha Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Marekani katika Bara laAfrika.

Alisema wakati wa ziara yake hapa nchini, Serikali ya Marekani inatarajia kutiliana sahihi msaada mkubwa wa maendeleo unaoelekezwa katika kuboresha miundo mbinu ya barabara, umeme na maji.

Kwa upande wa hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi jirani ya Kenya alisikitishwa na jitihada zanazofanywa na jumuiya mbalimbali za kimatiafa kutozaa matunda hivyo kusababisha hali kuwa mbaya nchini humo kiusalama.

Alisema serikali inaiunga mkono Kamati ya Kofi Annan (Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa), Rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa na mke wa wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Graca Machel.
 
Mwinyi wakati anayaua maadili hakufanya mchakato, aliita kikao cha NEC Zanzibar na kuwatangazia "Ruksa..." JK kwanini afanye mchakato kwa kitu ambacho kina mgongano wa maslahi wa wazi kabisa. Ni suala la yeye kuandaa utaratibu, anayetaka kuingia serikali akubali kujikana mwenyewe na biashara zake na si vinginevyo. Hizi lugha za michakato ni misamiati ya kisanii, ambayo rais hapaswi kuitumia awaachie mawaziri wa maji, miundo mbinu na afya waitumie kutoa ahadi zisizotekelezeka kwa kutumia msamiati wa mchakato.
 
hili ni shairi lingine,ambalo limepambwa kwa vina na mzani tulivu.hivi mpaka leo jk hajui watanzania wanataka nini ?,Sisi tunataka action na sio tungo mbalimbali za mashairi.
 
Please the same topic inaendelea hapa:::::BREAKING NEWS: JK na maadili ya viongozi::::

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=9391 ;;;;

So pls ingekuwa vema ikaunganishwa.
JK HILI NI KAMA TAIFA LA ISLAEL PAMOJA NA MUNGU KUWATOA UTUMWANI MISRI BADO WALICHONGA SANAMU NA KUZIABUDU.KILA UNALOFANYA KWAO BADO WANAENDELEA KULALAMIKA NA KUKEJELI.ACHANA NAO FANYA KAZI ACHANA NAO NABII HATAMBULIKI NYUMBANI KWAO.
 
Ana nia kweli ya kulifanya hili au ni usanii mwingine? Karamagi, Mkono na mawaziri na wabunge wengine wengi wa CCM mpo?

Posted Date::1/31/2008
Wabunge, mawaziri Tanzania kuchagua uongozi au biashara
Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete amewataka wafanyabiashara ambao ni wabunge na mawaziri kujiandaa kuchagua kimoja kati ya biashara au uongozi serikalini

Akizungumza jana katika utaratibu wake wa kila mwezi jana, Rais Kikwete aliwataka kuchagua jambo moja kati ya uongozi au biashara ili wasiendelee kuondokana na mwingiliano wa kimaslahi.

"Viongozi wetu wachague kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ama biashara au ubunge na Uwaziri. Kwa ajili hiyo ni makusudio yangu kuanzisha mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Uongozi ili tuingize utaratibu huo," alisema kuongeza.

"Ni jambo lenye maslahi kwa nchi yetu na litasaidia sana kujenga heshima ya viongozi wa umma mbele ya macho ya wananchi. Nafurahi kwamba suala hili tumelizungumza katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM tulichofanya Dodoma juzi Januari 29 na tumeelewana."

Alisema upo ushahidi wa kutosha wa kuwapo migongano ya maslahi kwa baadhi ya viongozi hao wa kisiasa suala linalosababisha wananchi kukosa imani na serikali.

Akitoa mfano wa mataifa yaliyoendelea alisema kuwa mataifa hayo yanao utaratibu unaomtaka mtu mwenye shughuli za kibiashara anapokuwa Mbunge au Waziri kuacha kujishughulisha na biashara zake na kwamba unakuwepo utaratibu rasmi unaotambuliwa kisheria wa wadhamini wanaoendesha hizo shughuli bila ya yeye kujihusisha nazo.

Akizungumzia suala la uhamiaji haramu nchini alitoa siku sitini za kwa wahamiaji haramu kujisalimisha. Baada ya hapo hatua zipasazo za kisheria zitachukuliwa kwa wale ambao watakuwa hawa kufanya hivyo.

Alisema kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kushuhudia mambo yasiyokubalika yakitendeka wakati akiwa kwenye ziara ya siku kumi Mkoani Kagera ambapo alikuta ukiukwaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na uingizaji mifugo nchini.

Alisema kwa muda mrefu sasa, raia wa nchi jirani zinazopakana na Mkoa wa Kagera wamekuwa wakiingia na kuishi nchini kwa vibali vya viongozi na watendaji wa vijiji na kata. Baadhi ya watu hao pia wamekuwa wakiingiza mifugo kwa vibali vya viongozi hao hao.

Suala hilo alisema halikubaliki kwani kwa mujibu wa sheria na taratibu za uhamiaji zinatoa mamlaka hayo kwa Maafisa Uhamiaji tu na si vinginevyo na kuwa viongozi na watendaji wa vijiji na kata hawana mamlaka hayo.

Hivyo alisema, vibali vyote walivyotoa viongozi hao si halali na havitambuliki na akapiga marufuku kwa kiongozi au mtendaji wa ngazi yoyote ile nchini kutoa kibali cha mgeni kuingia au kuishi nchini kama siyo Afisa wa Uhamiaji.

"Nilipokuwa Mkoani Kagera niliwaagiza Mkuu wa Mkoa na wakuu wa wilaya kufuatilia utoaji wa vibali unaofanywa na viongozi na watendaji wa vijiji na kata katika maeneo yao.

Nimewataka wawachukulie hatua zipasazo za kinidhamu watumishi hao wa umma pamoja na kuwabana wahamiaji haramu kufuata sheria za uhamiaji za nchi yetu au warudi makwao. Napenda kusema kuwa maagizo hayo ni kwa wakuu wote wa mikoa na wilaya nchini," alisema.

Sambamba na hilo pia ameiagiza Wizara ya Maendeleo ya Mifugo kutoa mwongozo wa jinsi ya usafirishaji mifugo kwa kuwa uvushaji unaoendelea sasa unaweza kusababisha hatari kubwa ya magonjwa ya milipuko kwa mifugo.

Pia alizungumzia la upandaji wa bei ya mafuta duniani akataka wananchi kuwawaangalifu na hasa wabanifu katika matumizi ya mafuta na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.

Alitaka juhudi za kuzalisha nishati mbadala kutokana na mimea hususan miwa, mawese na mbono-kaburi (jatropha) ziongezwe ili kama zikifanikiwa zisaidie kupunguza mzigo wa mafuta yanayoagizwa kutoka nje.

"Nafurahi kwamba juhudi zetu zina muelekeo mzuri na katika miaka michache ijayo tutaanza kunufaika na matunda yake. Pamoja na hayo tunaendelea na juhudi za utafutaji wa mafuta na gesi asilia hapa nchini,"alisema.

Kuhusu Uchunguzi wa Akaunti ya EPA alisema Serikali imedhamiria kulifuatilia suala hilo mpaka mwisho wake ambao utakuwa na maslahi kwa taifa.

Akawashukuru Watanzania kwa kuunga mkono hatua alizochukua na anazoendelea kuchukua kuhusu suala la Benki Kuu. Hata hivyo, alieleza kusikitishwa na taarifa anazozipata kuhusu kuwepo uvumi mwingi unaoenezwa na baadhi yetu kuhusu suala hilo.

Hivyo akakemea wale wote wanaoeneza uvumi na uongo kuacha kufanya hivyo na akawasihi wananchi wawe watulivu na wavumilivu.

"Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe na subira. Naamini kazi hii itakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita tuliyowapa. Napenda kurudia ombi la Serikali kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia katika uchunguzi na hatua katika suala hili waisaidie kamati yetu hiyo," alisema.

Akizungumzia ziara ya Rais George W. Bush wa Marekani katikati ya mwezi Februari, 2008 aliwataka wananchi wampokee kwa mujibu wa desturi na ukarimu wa Kitanzania kwani ujio wake unakuja na neema nyingi tofauti na uvumi unaoenezwa kuwa anakuja kuanzisha Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Marekani katika Bara laAfrika.

Alisema wakati wa ziara yake hapa nchini, Serikali ya Marekani inatarajia kutiliana sahihi msaada mkubwa wa maendeleo unaoelekezwa katika kuboresha miundo mbinu ya barabara, umeme na maji.

Kwa upande wa hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi jirani ya Kenya alisikitishwa na jitihada zanazofanywa na jumuiya mbalimbali za kimatiafa kutozaa matunda hivyo kusababisha hali kuwa mbaya nchini humo kiusalama.

Alisema serikali inaiunga mkono Kamati ya Kofi Annan (Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa), Rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa na mke wa wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Graca Machel.

Naona Mkuu wa nchi amekosa cha kusema mwezi Januari na ni bora angenyamaza tu akatuambia hana cha kuzungumza bali kututaikia mwaka mpya wenye maisha bora!

JK anataka kutuambia kuwa hakujua kuwa Waziri wake Kiranja-Lowasa ni "Mfanyabiashara" "aliyekubuhu", Mramba na Karamagai to mention afew hakuwajua kuwa ni "Wafanyabiashara"? Tuache utani!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom