Wabunge, Mawaziri na wakurugenzi mbona kimya kuhusu kukatwa mishahara?

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,803
8,795
Tumeshuhudia Waziri Mkuu akipokea mamilioni ya pesa ikiwa msaada wa kupambana na gonjwa la Corona.
Bwana Mkubwa mwenye jiji akaja na moja ya maelekezo vioja kuhusu wapangaji walipe kodi nusu kisha akaja na jipya la kutokaa ndani wafanyekazi. YEYE MPAKA LEO HAJASEMA ANATOA GAWIO KATIKA MSHAHARA WAKE. ila wengine biashara zao anazipangia majukumu.

Kenya karibia watendaji wakubwa katika serikali ya Uhuru wamepunguziwa asilimia fulani kwenda kuchangia vita ya corona huku kimyaaaaa kama hakuna jambo.

Sio akina Zitto sio mbowe sio Ndugai na wala sio Lusinde na kelele zake kaweza kunyanyua mdomo na kutoa pato lake la siku akachangia vita ya Corona.

Mitimu mikubwa ya ulaya wachezaji wao baadhi wameshajitolea kukatwa kwa mishahara yao kuchangia gonjwa la Corona. Timu tajiri na timu ya wananchi wapo kimya.

Natamani hili zogo lingeanza na wajuu ambao ni wabinafsi sana. Hakuna hata wakurugenzi wa mashirika ya umma hawa Maded na RAS na DAS nao wamepiga kimya kama hakuna janga.
Viongozi wetu wapo kuchumia mitumbo yao na wala sio kupigania ustawi wa pamoja . Yaaani hata wewe Mama Jenista Mhagama umeshindwa kutoa mkato katika mshahara wako uunge na uumie na wafanyakazi wengi ambao wamekaa majumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom