Wabunge kwenda na familia zao bungeni. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge kwenda na familia zao bungeni.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Darwin, Jul 6, 2009.

 1. D

  Darwin JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tunajua kwamba wabunge wa Tanzania wanapewa pesa nyingi za walala hoi.
  Tunajua pia kwamba baraza la mawaziri wa TZ nikubwa hata kuzipita nchi za ulimwengu wa kwanza, ambalo ufanisi wake ni kama zero.

  Tunajua pia kwamba wapo wabunge wengi TZ wanaolipwa mamilioni ya pesa bila hata kuyajali majimbo yao kimaendeleo.

  Tunajua pia kwamba wabunge wa TZ wana makaazi zaidi ya mawili, yote haya yanalipiwa kutokana na pesa za walala hoi.

  Sasa hiki kitendo chakubeba familia zao nakuziingiza bungeni, waTZ tunaelekea wapi?

  Waziri mzima na heshima zako unaaza kuwanadi watoto wako bungeni, mke wako, na wanakwaya wako.

  Bunge sasa limekua kama hall la harusi,
  Nini maana ya Bunge takatifu?
  Oops nimesahau kuhusu bunge linalohudhuriwa na mafisadi, wazee wa vijisenti, wazee wa mikataba feki na wavunja sheria za nchi.
  Mwisho naishukuru TBC kuionyesha aibu hii hadharani.
  Na nchi nyingine zinaona Utanzania halisi.
   
 2. F

  FM JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kila mtu na haki ya kuingia bungeni, una wahukumu watoto wa waheshimiwa kwa vyeo vya baba za na mama zao? tunajua kabisa wengi wa wabunge kwa umri wao na kama afya zao nzuri lazima wana watoto. sasa kuna ubaya gani kujua mtoto wa mhe. fulani ndiyo huyu. Wageni hutambulishwa bungeni na sio kunadiwa. Jenga hoja unayokusudia hii mie nimegoma.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hili la kutambulishana nalipinga kwa nguvu zote..Mara nyingi miswada mingi bungeni hupelekwa mbiombio kutokana na kukosa muda wa kutosha wa kuijadili..sasa tunapojaribu kuwa taifa linalokwenda na spidi ya karne ya sasa..hatuwezi kupoteza muda wa kuuza sura kwa wageni ambao hatuwajui...

  Hizi dhana za kijinga za kutambulishana inabidi zipigwe chini.
   
 4. d

  dmatemu JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2009
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 591
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 60
  FM unakosea, jamaa ana hoja kabissa tena iko wazi. Bunge lina mambo mengi ya msingi ya kufanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Si vibaya kwa watoto wa wabunge kwenda bungebi but ubaya unakuja pale watakapoa nza kusema wajitambulishe, because mtu kama mm ambaye nafuatilia shughuli za bunge kupitia vyombo vya habari ntaona ni ushamba wa wabunge zetu ambao badala ya kuumiza vichwa kufikiria mamabo ya maendeleo wanawaza kwenda kutambulisha watoto. Wabunge wenyewe wako sijui 435 sas kwa mfano, mbunge mmoja ana watoto 2. sasa mda wpte si utaisha kutambulisha? si hivyo tu bali bunge litajaa wwatoto wa wabunge na wageni wengine kama wakurugenzi wenye shughli muhimu bungeni watokosa nafasi. HAKUNA HAJA YA KUPELEKA FAMILIA ZA WABUNGE BUNGENI KWANI NI SERIKALI ITAKAYOGHARAMIKA. kweli bunge letu limeishiwa.
   
 5. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #5
  Jul 6, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inamaana baba akishakua mbunge na mtoto shule haendi sababu ya kuhudhuria vikao vya bunge? mama hatafanya kazi nyingine sababu ya kikao cha bunge? In the long run hii ni counterproductive in the long run.
   
 6. D

  Darwin JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hata mimi mlalala hoi nina watoto, jamaa wanipendao, marafiki, sijui na kila nani tena.
  Kama nitawachukua ofisini kwangu itakua kitu chakueleweka hapo?

  Kwanini kama hao watoto wa wabunge kama wanataka kutalii kwenye ukumbi wa bunge wasisubiri siku ambazo sio za kikazi?

  Ila nimeamini,
  Wewe kama mmoja wao.
  Hii inawezekana tu nchini Tanzania.

  By the way unajua kiasi cha mshahara wa mbunge anapokua bungeni?
  Nipe mahesabu kwa saa tu.
   
Loading...