Wabunge kuuziwa nyumba wakijadili bajeti ya nyumba/ardhi, hongo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge kuuziwa nyumba wakijadili bajeti ya nyumba/ardhi, hongo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Aug 15, 2011.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Katibu kupitia kwa mkiti wa Bunge Jenister Mhagama ametangazia wabunge kuwa Shirika la Nyumba liko ktk maeneo ya viwanja vya Bunge tayari kuwauzia wabunge Nyumba zake. Wanaotaka nyumba hizo wakajaze fomu pale walipo ktk viwanja hivyo vya Bunge.

  Tangazo hilo limetoka kipindi ambacho wabunge wengi wa CCM tangu mchana hadi jioni hii wakiwa wameonesha msimamo wa kutoiunga mkono bajeti ya wizara ya Nyumba, Ardhi na makazi. Kwanini leo bungeni? Kwani sisi tusio wabunge hatutaki hizo nyumba?

  Je, hii haiwezi kuwa Rushwa? Ninauliza tu! Bado sijatoa conclusion.

  Nawasilisha.
   
 2. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hata mie kwa kweli ile kauli ya Mwenyekiti kuhusiana na huko kuuziana nyumba imenishangaza na kunisikitisha sana!!

  Hivi kazi ya Takukuru ni nini kimazingira hii ni Rushwa tayari kutaka kuwapoza wabunge kuisamamia serikali katika ishu nzima ya ardhi...just imagine baada ya kikao cha jioni mbunge atoke nakuwahona wahusika nakupewa uhakika wa nyumba ya mkopo kwa Bei chee nini kitatokea katika mchango wake siku inayofuata?

  Mimi masikini pangu pakavu: Mwalimu, polisi, mjasiriamali mdogo, Mkulima; hivi naweza kupata tu hata nafasi juu ya taarifa ya hizo nyumba zinazouzwa? Ukweli ni kwamba Nchi imefika pabaya na siku zinavyokwenda ndivyo tunavyozidi kupotelea gizani.
   
 3. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Wewe hujui kuwa wabunge hawana nyumba? Na hujui sheria iliyoyounda na kuidhinisha ujenzi huo ililenga zaidi wakuu? Ungekuwa wewe ungefanyaje? Hasa ukikumbuka siku unadraive huna leseni na trafiki anaomba lift, pitia ile mikopo ya matrecta (mfuko wa pembejeo) wizara ya kilimo wakopaji karibu 60% ni wabunge na wakuu wengine.

  Mimi naona tatizo hakuna kwani mfumo unaruhusu.
   
 4. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Penye uzia penyeza rupia,ndugu hali ni mbaya kwenye hii bajeti na nina uhakika kama wakifuata haki haipiti kabisa.hiyo ni rushwa.
   
 5. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hawa jamaa wako kwa maslahi yao tu, hizo nyumba mbona sijaona zinatangazwa popote zaidi ya bungeni, ina maana wabunge tu ndio wana haki ya kununua hizo nyumba?

  Hili bunge ni ujairo mtupu, tusiwategemee hawa masaburi, naomba 2015 iwe kesho, hawa magamba ni kuwaponda kichwa kabisa hakuna kuwavua magamba.
   
 6. p

  plawala JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna kilicho chema kinaweza kutoka kwa mfumo wa kimagamba kikaenda kwa walala hoi

  Siku nyingi nimesikia kuna nyumba zinajengwa Dodoma kwa ajli ya kuwauzia watu kwa mkopo wa bei nafuu

  Hata kama tangazo halijadhamiria kuwanyamazisha bunge kwa nini nchi hii wasikumbikwe askari waalimu na watu wengine wenye kipato cha chini?

  Wale waliozoea kufanya hiyo michezo watasema mbunge ana haki kama alivo mwananchi mwingine yeyote.
   
 7. NEW TANZANIA

  NEW TANZANIA Senior Member

  #7
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  keki ya nchi inagawanwa
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  This is unconstutional... Uuzaji wa nyumba hizo hauna tofauti na uuzaji wa nyuma za viongozi ulofanyika wakati wa Mkapa.
   
 9. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mmh, jamni!!!!
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Naomba ufafanuzi, hizi nyumba wanazouziana ndio zile Spika aliziita Bunge village?

  Kama ndiyo ina maana wabunge wanamiliki nyumba ni wabunge wa maisha au?
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  wabunge sio wahitaji sana wa hizo nyumba, kwa nini wasiende uswazi kuanza na zoezi hilo, kwa nini wasiende wakati wa bajeti ya kilimo, kwa nini sasa???
   
 12. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Namsikitikia Edward Hosea kwakuwa anabeba dhambi za wenzake kwa kuzifumbia macho (kwa staili hii mbingu sahau), kama ataendelea hivi yeye na mafisadi ni sawa tu kwani kwa jambo kama hili alipaswa kutoa tamko kali bila kujali nani ataumia.
   
 13. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Kila Wizara ina matatizo na bajeti yake, ndio kazi ya copy n paste hiyo khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hii kwakweli ni rushwa/hongo na nitashangaa sana kama wabunge wa chadema watapretend hawajui nini kinaendelea
   
 15. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,650
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  Kwa hali ilivyo sasa katika Tanzania, wananchi wa kipato cha chini wanatakiwa kuanza mapambano ya kujikomboa kama walivyoanza enzi za kudai uhuru. Siyo rahisi tena wapate utetezi wa kuinua hali zao za maisha kupitia mfumo uliopo.
  Viongozi walio wengi wanajifikiria wenyewe, familia zao pamoja na marafiki zao.
  Wananchi wa vipato vya chini na vya kati mfumo wa utawala hauwajali na uzalendo hakuna tena na matokeo yake ni;
  1. Wageni wanamiliki uchumi wa nchi kwa kupitia viongozi wasiowadhibiti nidhamu ya uwekezaji.
  2. Wageni kufanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na wenyeji.
  3. Wageni kulipwa mishahara mikubwa kuliko wenyeji hata pale ambapo mwenyeji ana ujuzi na ufanisi kuliko mgeni.
  4. Wageni kumilikishwa ardhi kirahisi tu kwa kuwanyang'anya wenyeji.
  5. Kuanzishwa kwa mamlaka kama EWURA, SUMATRA etc ambazo hazimsaidii mwananchi wa kawaida zaidi ya kuongeza urasimu na gharama za huduma kupitia tozo.
  6. Viongozi kujilimbikizia mali, kujiuzia nyumba za serikali na sasa NHC, kujimilikisha njia kuu za uchumi etc.

  Kuondoa hali hii, wananchi wa kawaida wanatakiwa kuelewa kuwa viongozi na wanaofaidi mfumo huu ni wachache na hivyo kuwashughulikia ni rahisi sana. Tukiamua kubadilisha hali hii inawezekana tena kwa ufanisi na muda mfupi kutokana na wingi wetu.
  Viongozi wanatumia ujinga wa wananchi walalahoi kuwanyonya na kuwadhibiti. Vyombo vya dola vinavyotumika vinaundwa na walalahoi wanaonyonywa kwa asilimia kubwa na wao wanahitaji kushiriki kujikomboa.
  Polisi, jeshi la wananchi na hata mgambo wengi ni walalahoi kabisa ambao hawafaidiki na mfumo uliopo na hiyo tukiamua kurekebisha mfumo huu usiowasaidia wananchi walio wengi inawezekana, ni swala la kuamua ili kupata mustakabali mwema kwa watoto wetu na vizazi vijavyo.
  Mashujaa tunaowakumbuka siku hizi walijitoa kwa ajili ya wengi na yatubidi kujenga mawazo kwa wananchi kujitoa kwa ajili ya vizazi vijavyo kwa kuwa ukombozi lazima uwe endelevu.
  Viongozi wengi wamejisahau wakifikiri kuwa uhuru ulilenga kukomboa wao wenyewe, familia zao na marafiki wachache, lakini ukweli ni kwamba maana ya uhuru ni ukombozi kwa wananchi wote ambao ni zaidi ya milioni 40 kwa sasa na vizazi vijavyo.
   
 16. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Insikitisha kwa kweli

  Kwanini wasitanguliwa kuwapa kipumblene wakazi na wananchi wa dodoma kama walimu, menesi na wafanyakazi wengi be wanunue nyumba hizo.

  Au wabunge wanauziwa nyumba zizilzoko mikoa na wailaya wanazowakilisha.?


  Yaani Hiii nchi inakosa mwelekeo

  NSSF wanajenga nyumba za mawaziri
  JKT au JWTZ nao wakimua miradi ya nyumba ni ya wakubwa .

  Hivi hii mipango miji tunayotaka kwa mshahara gani mwalimu au mfanyakazi wa KCC atapata nyumba au japo chumba cha kaiwada lakini chenye hadhi na miundombinu ya maana inayotaiwa na binadamu.

  Hakuna anyejaribu kuteteta maslahi ya mwananchi wa kwaida iwe ni kuishi, usafiri, afya nyumba, mikopo

  Ndio hapo sasa kabl y wabunge tujiulize ni walimu wangapi wameambiwa wajaze fomu hizo. madaktari wangapi. Yaani wabunge wasio wakazi wa dodoma ndio wanapewa proority. Watu ambao kukaa kwao Dodoma wanakula Per diem bado wanataka kuwauzia nyumba.
   
 17. S

  Safre JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Bado meng yanakuja
   
 18. n

  ngoko JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MJ usishangae huo ndo mfumo wenyewe na unabaraka zote za angalau 2/3 kama siyo 3/3 ya mihimili unayoijua.
   
 19. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Wanaosema ndio waseme..'ndiyoooooooooo'...wanaosema sio 'siooooooooooooooooooooooooooooo!!
  Waliosema ndio wameshinda, bajeti imeungwa mkono!!
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hapa tukumbuke wahanga wa Gongo la Mboto bado wanaishi kwenye mahema!
   
Loading...