Wabunge kuunga hoja asilimia miamoja!

Rwabugiri

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
2,773
209
Nilikuwa nakisikiliza bunge jana usiku, nikasikia mbunge wa Karagwe Brandesi akiuliza swali la msingi kwamba kuna dispensary zaidi ya tano za kata tofauti jimboni kwake ambazo ziliomba dawa mbali mbali lakini katika bajeti hajasikia pesa ilo tengwa kwa shughuli hiyo, na kwa msingi huo ina maana mwaka wote huu hizo dispensary hazitapa hata asprini!

Jibu la waziri ilikuwa ni kweli barua ilifika March wakisha panga bajeti na hizo pesa hazipo kwahiyo hizo dawa hazitakuwepo kwa mwaka mzima!

Nilicho shangaa ni huyo huyo mbunge Brandesi aliye uliza hilo swali na kupewa jibu kwamba hakuna dawa hata moja itapelekwa kwa dispensary hizo alipo kuwa kati ya wabunge wote walio unga hoja asilimia mia moja. Ina maana anaridhika na kutopata dawa mwaka mzima? kama la kwanini aliunga mkono asilimia mia moja? Na vipi hatima ya hao watu wake kutokuwa na dawa mwaka mzima?

Je hilo jibu la waziri linajali maslahi ya walalahoi watakao kufa mwaka mzima kwa kukosa panado?
 
Hivi serikali haijui ina dispensary ngapi tanzania nzima na consumption ya dawa hiko je kwenye kila dispensary? hawa wataalamu wanasomeshwa kwa gharama nyingi wanafanya kazi gani kusubiri mpaka mtu ambaye sio mtaalamu wa material management aandike barua ya kuomba dawa.

Sasa hivi hizi Dispensary ziko kidogo sana je? kila kijiji kikiwa na dispensary kama mpango wa afya unaoanza kutekelezwa mwaka huu wa fedha unavyosema itakuwaje?

Hawa wabunge ni wanashangaza sana yaani dispensary za jimbo lako zinakosa dawa kwa mwaka mzima na wewe unapitisha budget bila hata kuakikisha serikali inalekebisha hilo, watu wangapi watakufa kwa kukosa dawa katika vijiji usika?
 
Huyo mbunge hawakilishi wananchi wa JIMBO lake bali anawakilisha chama chake BUNGENI cha CCM kuendelea kukandamiza wananchi hana hata uchungu mpaka anaamua kuunga mkono hoja kwa 100% hana uelewa yupo tu bungeni kama ushahidi tu.
 
usije ukashangaa ukisikia spika kafunga mjadala na ishu hiyo 'inashugulikiwa' na wizara husika.

maana siku yao hizi njia rahisi ya kukwepa kubanwa ni spika kufunga mijadala
 
mbunge alikuwa anategemea jawabu hilo.....ndio maana kauliza ili ajibiwe apate cha kuwaambia wananchi wake.

jibu halijamuuma hata kidogo......karidhika tu kuwa sasa wananchi waliomchagua atawaeleza kuwa alifikisha malalamiko yao lakini serikali haina pesa.

mambo mazuri kwake
 
Siku zote ninavyosikiliza bunge majibu mengi sana yanakuwa serikali itashughulikia. mwaka unaofuata wabunge wanarudi na situatutions worse than the previous ones, jibu linakuwa lile na cha kushangaza wanaunga mkono asilimia mia. Ni lini hawa wabunge wataamka waone wanafanya upuuzi huko bungeni?
 
nashukuru wote mlio changia hii hoja, nimegundua kumbe ndo maana hata watu wengine huona kupigia kura wabunge ni kupoteza muda wao, kwani kwa swala kama hili ni maigizo tu yanayo fanyika! Kuunga mkono asilimia mia moja ili watu wako wakose dawa mwaka mzima binafsi naona ni usanii wa hali ya juu.

Kama angekuwa mbunge makini hapo ndo angeonyesha makeke yake kwa kuelezea mapungufu yaliyopo katika mlolongo mzima wa kuwezesha dispensary kama hizo zipate dawa na kuhitimisha kutoa changamoto kwa kuitaka wizara ihakikishe dawa zinapatikana, lakini kwa usanii sijui? uoga? hata sielewi anaishia kuunga mkono hoja!

Bado tunayo safari ndefu sana, na hakika mapinduzi ya kifikra ina bidi yaelekezwe kwa wawakilishi wetu ambao ni wabunge wanao onekana kutojua wajibu wao kama wabunge.
 
Tuanzishe jukwaa maalum la KATIBA MPYA. Tumejiandaa vipi kwenye matayarisho ya kuwa na Katiba mpya? Kuwa na Katiba mpya ni swala lisiloepukika.

In the meantime, tutaendelea kuwa na 'viongozi' au wabunge wa aina hiyo hapo juu.




.
 
Ndugu yangu rwabugiri, bunge letu lina wasanii kwa asilimia tisini.Usifikiri watu wapo pale kwa interest za wananchi, la hasha.

Ukitaka kujua ukweli nenda Dodoma wakati wa kikao cha bunge la bajeti halafu tembelea maeneo maarufu ya kunywa na kula kama Rose Garden hivi utawaona mawaziri na manaibu, makatibu na maofia wa wizara ambazo bado hazija soma bajeti zao wakiwa faragha na wabunge fulanifulani wakiweka mabo sawa.

Asikwambie mtu, mawaziri wetu wanaongoza kwa kufanya 'lobbing' kwa wabunge kusudi wale wenye maswali mazito na hoja za kusimamisha bajeti walainishwe mapema.Wanatenga fungu la kuwaziba midomo wale wenye kusema sanaaaaa!
Chama tawala nacho kina utaratibu mbovu wa kubebana eti kuinusuru serikali.Wapo wabunge wanaotumika kuvuruga hoja za wenzao walio makini kwa kujifanya wanasema sana lakini hakuna chochote, upuuzi na kuteketeza nchi.

Ukiona mbunge anahoji mambo fulani kuwa yanakasoro kwenye bajeti halafu anaunga bajeti asilimia mia kwa mia usimwite mnafiki kuanzia leo, wewe piga goti kwa MUNGU wako uiombee Tanzania Mungu ainusuru na wabunge na viongozi kama hao.Hawatabadilika kamwe hata tukiwachoma moto, watakufa na unafiki wao.

Taifa linateketea.
 
Back
Top Bottom