Wabunge kuunga hoja asilimia miamoja!


R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
2,776
Likes
16
Points
135
R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
2,776 16 135
Nilikuwa nakisikiliza bunge jana usiku, nikasikia mbunge wa Karagwe Brandesi akiuliza swali la msingi kwamba kuna dispensary zaidi ya tano za kata tofauti jimboni kwake ambazo ziliomba dawa mbali mbali lakini katika bajeti hajasikia pesa ilo tengwa kwa shughuli hiyo, na kwa msingi huo ina maana mwaka wote huu hizo dispensary hazitapa hata asprini!

Jibu la waziri ilikuwa ni kweli barua ilifika March wakisha panga bajeti na hizo pesa hazipo kwahiyo hizo dawa hazitakuwepo kwa mwaka mzima!

Nilicho shangaa ni huyo huyo mbunge Brandesi aliye uliza hilo swali na kupewa jibu kwamba hakuna dawa hata moja itapelekwa kwa dispensary hizo alipo kuwa kati ya wabunge wote walio unga hoja asilimia mia moja. Ina maana anaridhika na kutopata dawa mwaka mzima? kama la kwanini aliunga mkono asilimia mia moja? Na vipi hatima ya hao watu wake kutokuwa na dawa mwaka mzima?

Je hilo jibu la waziri linajali maslahi ya walalahoi watakao kufa mwaka mzima kwa kukosa panado?
 
J

Jamco_Za

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2007
Messages
1,321
Likes
35
Points
145
J

Jamco_Za

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2007
1,321 35 145
Hivi serikali haijui ina dispensary ngapi tanzania nzima na consumption ya dawa hiko je kwenye kila dispensary? hawa wataalamu wanasomeshwa kwa gharama nyingi wanafanya kazi gani kusubiri mpaka mtu ambaye sio mtaalamu wa material management aandike barua ya kuomba dawa.

Sasa hivi hizi Dispensary ziko kidogo sana je? kila kijiji kikiwa na dispensary kama mpango wa afya unaoanza kutekelezwa mwaka huu wa fedha unavyosema itakuwaje?

Hawa wabunge ni wanashangaza sana yaani dispensary za jimbo lako zinakosa dawa kwa mwaka mzima na wewe unapitisha budget bila hata kuakikisha serikali inalekebisha hilo, watu wangapi watakufa kwa kukosa dawa katika vijiji usika?
 
Francis the King

Francis the King

Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
16
Likes
0
Points
0
Francis the King

Francis the King

Member
Joined Oct 4, 2007
16 0 0
Hao ndio wawakilishi wa wananchi wa jamhuri ya muungano wa Wadanganyika
 
Fidel80

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Messages
21,970
Likes
140
Points
145
Fidel80

Fidel80

JF-Expert Member
Joined May 3, 2008
21,970 140 145
Huyo mbunge hawakilishi wananchi wa JIMBO lake bali anawakilisha chama chake BUNGENI cha CCM kuendelea kukandamiza wananchi hana hata uchungu mpaka anaamua kuunga mkono hoja kwa 100% hana uelewa yupo tu bungeni kama ushahidi tu.
 
T

Tuandamane

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2008
Messages
1,220
Likes
2
Points
135
T

Tuandamane

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2008
1,220 2 135
usije ukashangaa ukisikia spika kafunga mjadala na ishu hiyo 'inashugulikiwa' na wizara husika.

maana siku yao hizi njia rahisi ya kukwepa kubanwa ni spika kufunga mijadala
 
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2007
Messages
11,845
Likes
86
Points
0
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2007
11,845 86 0
mbunge alikuwa anategemea jawabu hilo.....ndio maana kauliza ili ajibiwe apate cha kuwaambia wananchi wake.

jibu halijamuuma hata kidogo......karidhika tu kuwa sasa wananchi waliomchagua atawaeleza kuwa alifikisha malalamiko yao lakini serikali haina pesa.

mambo mazuri kwake
 
Power to the People

Power to the People

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2007
Messages
1,200
Likes
253
Points
180
Power to the People

Power to the People

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2007
1,200 253 180
Siku zote ninavyosikiliza bunge majibu mengi sana yanakuwa serikali itashughulikia. mwaka unaofuata wabunge wanarudi na situatutions worse than the previous ones, jibu linakuwa lile na cha kushangaza wanaunga mkono asilimia mia. Ni lini hawa wabunge wataamka waone wanafanya upuuzi huko bungeni?
 
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,134
Likes
74
Points
145
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,134 74 145
Bunge la bongo lala hilo......
 
BabaH

BabaH

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2008
Messages
703
Likes
7
Points
35
BabaH

BabaH

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2008
703 7 35
Wabunge wengi hawajui wanafanya nini pale na wala hawajui wayafanyayo wanasubilia kupewa posho tu

Hivi ebu jiulizeni, watu kama Makamba, Komba, Rwakatale nao ni wabunge mnategemea nini!

Kwa sifa za hawa jamaa na jinsi walivyofika pale Bungeni, wala tusitegemee kama kuna kupata maendeleo na challenge kutoka bungeni jamani

na ndio maana serikali kupitia wizara zake haifanyi lolote na hizo bajeti kila mwaka, lakini utayasikia yanaitikia naunga mkono asilimia mia moja hata kama mijibarabara kwenye jimbo lake ni mibovu mpaka basi ataitikia tu ili mradi twende.

Haya ndio matunda ya mmea tuliopanda 2005 na bado tutaendelea kuvuna tu mpaka 2010 tena zaidi ya haya ya sasa.
 
R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
2,776
Likes
16
Points
135
R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
2,776 16 135
nashukuru wote mlio changia hii hoja, nimegundua kumbe ndo maana hata watu wengine huona kupigia kura wabunge ni kupoteza muda wao, kwani kwa swala kama hili ni maigizo tu yanayo fanyika! Kuunga mkono asilimia mia moja ili watu wako wakose dawa mwaka mzima binafsi naona ni usanii wa hali ya juu.

Kama angekuwa mbunge makini hapo ndo angeonyesha makeke yake kwa kuelezea mapungufu yaliyopo katika mlolongo mzima wa kuwezesha dispensary kama hizo zipate dawa na kuhitimisha kutoa changamoto kwa kuitaka wizara ihakikishe dawa zinapatikana, lakini kwa usanii sijui? uoga? hata sielewi anaishia kuunga mkono hoja!

Bado tunayo safari ndefu sana, na hakika mapinduzi ya kifikra ina bidi yaelekezwe kwa wawakilishi wetu ambao ni wabunge wanao onekana kutojua wajibu wao kama wabunge.
 
LazyDog

LazyDog

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Messages
2,478
Likes
17
Points
135
LazyDog

LazyDog

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2008
2,478 17 135
Tuanzishe jukwaa maalum la KATIBA MPYA. Tumejiandaa vipi kwenye matayarisho ya kuwa na Katiba mpya? Kuwa na Katiba mpya ni swala lisiloepukika.

In the meantime, tutaendelea kuwa na 'viongozi' au wabunge wa aina hiyo hapo juu.
.
 
Mzee wa Gumzo

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Joined
Apr 21, 2008
Messages
197
Likes
0
Points
0
Mzee wa Gumzo

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Joined Apr 21, 2008
197 0 0
Ndugu yangu rwabugiri, bunge letu lina wasanii kwa asilimia tisini.Usifikiri watu wapo pale kwa interest za wananchi, la hasha.

Ukitaka kujua ukweli nenda Dodoma wakati wa kikao cha bunge la bajeti halafu tembelea maeneo maarufu ya kunywa na kula kama Rose Garden hivi utawaona mawaziri na manaibu, makatibu na maofia wa wizara ambazo bado hazija soma bajeti zao wakiwa faragha na wabunge fulanifulani wakiweka mabo sawa.

Asikwambie mtu, mawaziri wetu wanaongoza kwa kufanya 'lobbing' kwa wabunge kusudi wale wenye maswali mazito na hoja za kusimamisha bajeti walainishwe mapema.Wanatenga fungu la kuwaziba midomo wale wenye kusema sanaaaaa!
Chama tawala nacho kina utaratibu mbovu wa kubebana eti kuinusuru serikali.Wapo wabunge wanaotumika kuvuruga hoja za wenzao walio makini kwa kujifanya wanasema sana lakini hakuna chochote, upuuzi na kuteketeza nchi.

Ukiona mbunge anahoji mambo fulani kuwa yanakasoro kwenye bajeti halafu anaunga bajeti asilimia mia kwa mia usimwite mnafiki kuanzia leo, wewe piga goti kwa MUNGU wako uiombee Tanzania Mungu ainusuru na wabunge na viongozi kama hao.Hawatabadilika kamwe hata tukiwachoma moto, watakufa na unafiki wao.

Taifa linateketea.
 

Forum statistics

Threads 1,250,303
Members 481,303
Posts 29,727,544