Wabunge kutoka Zanzibar kwa nini wasipungue ili wawakilishe Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge kutoka Zanzibar kwa nini wasipungue ili wawakilishe Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Malaria Sugu, Jul 14, 2011.

 1. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zanzibar wanaowawakilishi wao katika baraza la wawakilishi. kazi kubwa ya wawakilishi hao ni kuwatetea katika maswala mazima ya maji safi, umeme, kilimo, afya na mambo mengine ya msingi katika majimbo wanayowakilisha.
  na kazi kubwa ya wabunge inalingana kabisa na kazi za wawakilishi sio kuwatumikia watz tu. malengo ni kuwatumikia wananchi wa Jimbo lao
  wabunge kutoka zanzibar siwasikii wakizungumzia maendeleo ya majimbo yao, hawaiombi serekali ya Muungano kuwachimbia visima, kuwapelekea nguzo za umeme. matrekta hata kujengewa shule na zahanati. Haya yote yanafanywa huko Baraza la wawakilishi.
  Machcahe huyasikia yanahusu majeshi, polisi na muungano tena huzungumziwa kiujumla.
  Fedha za Jimbo sijui kama zinatumika zanzibar. kwani kazi ya maendeleo ya Jimbo hufanywa na mwakilishi anaependekeza kufanyiwa barazani.
  Wabunge wa Zanzibar hawazungumziii umeme wa Jimbo, kisima wala mengine
  JEE hakuna haja ya Kupunguza lwabunge kutoka zanzibar ili kupunguza gharama? na kuchaguliwa wabunge wataokuja kuwalisha zanzibar na sio majimbo ?
   
 2. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sali hivi kunapokuwa kunajadiliwa bajeti za wizara ambazo si za muungano, je hawa waheshimiwa wanaingia majengoni? na kama wanaingia kufanya nini kulala? na wanalipwa vipi wakati kisheria hawatakiwi kuchangia maana hizo wizara haziwahusu. Sasa kama wanalipwa hawaoni kuwa ni wizi wa pesa za walala hoi wa Tanzania bara bila hata aibu?
   
 3. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kwani kila siku tukiwambia kua huu "muungano" ni feki, mnadhani tunatania?

  Huo ndio "muungano" ambao mnaulinda kwa nguvu za kijeshi ya uvamizi Zanzibar.

  Haja si kupunguza idadi ya Wabunge, haja ni kuachana nao kabisa.
   
 4. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kweli hapo kwenye red umesema jambo la maana-kama kuna vikao vya wizara amabvyo wizara si za muungano wabubge wa zanzibar wanatakiwa wasiwepo kabisa-maana kuwepo kwao bungeni kunawafanya wazidi kula hela za tanganyika-vikao hivyo vitumike kudiscuss matatizo ya watanganyika tu-si kutuletea habari zao zisizotuhusu-
  KITU KINGINE KINACHO NISHANGAZA NI HOJA ZA HAWA WABUNGE WA ZANZIBAR KUDAI USAWA WA KILA KITU,YAN PASU KWA PASU NA TANGANYIKA-HIVI KWELI WATU WASIOZIDI MILION MOJA,WANAWEZA KUPEWA VITU PASU KWA PASU NA WATU TAKRIBANI MILION 38?KAMA SI KUTAKA KUTONYONYA SISI WATANGANYIKA-
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nafikiri huo ni moja kati ya utata wa Muungano. Kila jimbo zanzibar linaleta mbunge na kisha Ndani ya baraza la wawakilishi wanachaguliwa wawakilishi watano kuliwakilisha baraza katika Bunge.

  Sasa ni wakti wenu muafaka kama kweli mna nia thabiti ya kuipenda nchi yenu mukiondoa kifungu hicho ili wapungue na wala sio kuleta kelele chooni.
   
 6. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Watz wengi ni kichwa cha wenda wazimu sisi si wachambuzi ndio maana utakuta mtu anashabia sisiem bila kufahamu makosa makubwa na matatizo yaliyosababishwa na sisiem kama hili la mdau!
   
 7. J

  Justine Kilasara Member

  #7
  Jul 15, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hao CCM bado wanang'ang'ania muungano wa serikali mbili, napendekeza uwe hivi, zile wizara zisizokuwa za muungano zikutane mapema na kupitisha bajeti zao sambamba na baraza la wawakilishi huko Zanzibar, baada ya hapo baraza la wawakilishi la zanzibar na wabunge wa wabara wakutane kama bunge la muungano, walofuata utaratibu huu wataondoa mkanganyiko wa mambo mawili, la kwanza ni hili la jimbo moja kuwa na wawakilishi wawili, la pili ni kuwa watu wenye mtazamo mmoja watajadili mambo kwa pamoja, tofauti na sasa hivi wabunge wa zanzibar wanaridhia jambo katika bunge wakienda kwao wawakilishi wanakuwa na mtazamo tofauti.
   
 8. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  pia ina maana wabunge wa zanzibar wanapokea fedha mara mbili mbili-kwenye vikao vya bunge huku tanganyika-na kwenye vikao vya baraza la wawakililshi-
   
Loading...