Wabunge Kushindwa Kuielewa Misuada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge Kushindwa Kuielewa Misuada

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichankuli, Apr 4, 2009.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Katika habari zilizorushwa na Kituo cha ITV jana toka kwenye semina ya Wabunge, wabunge walieleza kuwa na wakati mgumumu kuielewa misuada inayowasilishwa kwao kabla ya kuipitisha. Hali hii imenishangaza na kunishitua. Imenishangaza kwa sababu Bunge la serikali ya awamu ya tatu limejaa ma DR. wengi kweli kweli. Sasa sijui MaDr. hao ni wa aina ya Remmy!. Lakini kilichonishitua ni kwamba inamaana muda wote huu wamekuwa wakipiga makofi kwenye meza na kuunga mkono kupitisha vitu ambavyo hawavielewi. Je wadau wa JF hali hii itatufikisha wapi/ Natoa hoja kwa mjadala
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kauli hiyo ilitolewa na mwakyembe, nadhani kuna watu alikuwa anawalenga
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nilipoanza kusoma hiyo habari nilishutuka hayo maneno ya Dr. Lakini ukisoma vizuri unagundua mawazo ya Dr. yalikuwa mazuri tu. Ushauri wake kwamba misuada iandikwe kwa Kiswahili nafikiri ni sahihi kabisa. Pia wanaweza kuwa wanatafsiri kwenye lugha zote mbili. Nafikiri Mwandishi wa hii habari katumia vibaya hilo neno kuwaumbua. Ukisoma ndani unakuta lengo lilikuwa sio kuumbua wengine.

   
 4. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Siyo Mwakyembe pekee, bali wengi ambao walipata fursa ya kuonekana kwenye Runinga ya ITV walikiri kuwepo udhaifu huo na wakawa wanawsema kuna haja misuada hiyo kupelekwa kwa wataalamu wa fani husika na wadau kabla ya kuwasilishwa Bungeni. Mimi naona kuna udhaifu wa uelewa miongoni mwa wanasiasa wetu. Ukiangalia wabunge wengi ni Askari Wastaafu, na katika Tanzania hii watu wengi waliokuwa wakiingia Jeshini wakati ule walikuwa ni wale waliokuwa na matokeo dhaifu darasani. Pitia kwa harakaharaka wakuu wa wilaya na mikoa waliopo uone walivyojaa maaskari. Wakishatoka huko wanaingia kwenye Ubunge.

  Lakini lingine ambalo nadhani linaletas hali hii ni ubunge kutokuwa na ukomo wa kiumri. Hali hii inafanya Bunge kujaa watu ambao uwezo wa akili zao katika kufikiria ukoo katika stage ya kudimishish. Mfano Mzee Kingunge alishatangaza kustaafu, lakini kwa mshangao JK akamteua tena. Nafasi kama hizo anazopewa Rais kuteua angekuwa anazitumia kuwateua vijana wanaomazilza vyuo vikuu ili kuwa na mchanganyiko mzuri wa kifikra. Angalia changamoto anazotoa Zito, je wangekuwepo hao kumi wa aina yake hali ingekuwaje? Lakini badala yake tunapeleka bungeni wazee wanaenda kulala, Mke (Viti Maalumu) na Mume na Kufanya Bunge kuwa familia
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hivi majukumu ya mbunge ni yepi?

  Yanahitaji elimu gani?

  Naomba kuelimishwa hapa.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Jukumu kubwa la Mbunge ni kuisimamia serikali katika utekelezaji wake. Anatakwia ajue kuandika na kusoma
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Shukran,

  Jukumu la bunge kwa ujumla nadhani ndilo hilo, tukilichukulia kwa mapana yake, yaani kuisimamia serikali. Kwa jinsi inavyofahamika, na kwa jinsi ulivyoweka hayo mahitaji ya mtu kuwa mbunge, yaani kujua kusoma na kuandika, sioni ni kwa jinsi ipi huyu mbunge, au wabunge (tukizungumza kwa mapana) wanawezaje kuisimamia serikali yenye wataalamu. Serikali ina wataalamu, bunge halina..

  Sasa huu si mchezo wa kuigiza? Au nipo bado kizani?

  Ningependa kueleweshwa kwa undani kidogo zaidi,kuhusu mbunge as an individual member of parliament, day to day, anatarajiwa afanye nini kuisimamia serikali, na kama hafanyi hivyo, anachukuliwa hatua gani.(Maana kuna wabunge sijawahi kuwasikia hata sauti zao zinasound vipi)
   
 8. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Kwa mujibu wa katiba (kifungu sikikumbuki) jukumu kuu la Bunge ni kutunga sheria. Lakini jukumu lingine la msingi la bunge ni kupitia, kujadili na kuidhinisha bajeti ya serikali; na baada ya hapo kuhakikisha kwamba serikali inatekeleza yale yaliyoainishwa kwenye bejati za wizara ambazo zimeidhinishwa na Bunge kwa ajili ya kutekelezwa.

  Sasa kama ulishawahi kuona vitabu vya bajeti za wizara unaweza kupata picha kiwango cha elimu (lakini pia na umri) ambacho kinastahili mtu kuweza kuyapitia makabrasha yale na kupembua mchele na chuya. Ndiyo maana wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu alipotoas tamko la kufuta semina pamoja na ununuzi wa Mashangingi mimi nilishangaa kwa sababu hayo yalitakiwa kufanyika katika mchakato wa kujadili bajeti za wizara kabla ya kuziidhinisha. Lakini wakati ule Wabunge hawakufanya hivyo ila waliunga mkono hoja kwa asilimia mia moja na kufanya bajeti zile kuwa na azimio la Bunge ambalo wabunge wenyewe wanasema kisheria haliruhusiwi kuhojiwa badala yake linahitaji utekelezaji tu.
   
 9. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Plain and clear kuwa wabunge wengi ni maimuna, ninakumbuka one time wakati bunge linaanza la mshikaji wenu kikwete, kuna mbunge alimponda Mzee Kabuye(Ex- MP) kuwa hajui kiingereza the reason behind ni kuwa atakwenda kusema nini akiwakilisha bunge nje ya nchi, naye mzee wa watu akatoa mfano kuwa amewasomesha watu wa nje wa kumwaga na kumalizia kumshukuru kwa kiingereza. It was a total humiliation lakini inaonyesha kasumba ya watu kujifanya wanaijua sana lugha ya malkia na kisha kupitisha contract kibao zenye utata.
   
Loading...