Wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Pinda?

MOD unganisha na ile yangu sikuiona hii!
Ila haya mambo ya kis.........................ge INABIDI TUYAACHE huwezi toa bandari kubwa kama ile kipuuzi puuzi ivi jamani tunaenda wapi?
 
Jamani hii imetokea Tanzania!! Huwezi amini lakini ndio kilichofanyika! Serikali imebadilishana na Kampuni iliyokodisha ndege ya ATCL na Bandari ya Mtwara! Jamani hii nchi yetu tuna viongozi au tunaongozwa na M......ko?
 
Ni katika kuhitimisha hotuba za kamati zao bungeni jioni hii,zitto awapasha joto mawaziri wa JK,
wajiuzuru kama hawataki watamuondoa PM PINDA nao wafate.kesho zinakusanywa kura 70 za kutokua na imani na PM ili siwasilishwe J3.
kweli zitto umetukuna wa-tz wengi wazalendo.bigup.kaza buti
hakuna kulala mpaka kieleweke,
 
inabidi 2015 cdm tupate wabunge hata mia hivi ili haya mambo ya kura ya kutokua na imani na waziri mkuu tupige kura wenyewe tu...magamba wazushi sana.
Ilo neno..tutakuwa na control sasa ivi mpaka mapamba watusapoti kaazi kweli kweli
 
lakini je bado miez 3 tu bunge la bajeti likae sasa wakiwatimua leo hiyo bajeti itakuwaje? na watakao chaguliwa kweli watakuwa wameshaelewa mwenendo mzima wa ofisi hadi hiyo mwez wa 7?
 
Hizo sahihi zingetakiwa muda huu ambao wabunge bado wana munkari zingepatikana zaidi ya saini 200.
Kwakuwa ni mpaka kesho wabunge wa ccm lazima wakafanye kikao cha dharura ya kuwatosa wananchi na kuwalinda wezi, kwa maana ya kutoweka saini ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Ila Zitto tayari ana sahihi ya Deo na Zambi.
 
Ni ama waziri mkuu awajibishwe na bunge ili baraza zima livunjike au mawaziri wazembe na watendaji wao wawajibike au kuwajibishwa na JK.
Nail 'em Up
 
Deo Filikunjombe hakumung'unya maneno. Toa ushahidi anautoa papo kwa papo. Kweli Tanzania tunasonga mbele
 
Hizo sahihi zingetakiwa muda huu ambao wabunge bado wana munkari zingepatikana zaidi ya saini 200.
Kwakuwa ni mpaka kesho wabunge wa ccm lazima wakafanye kikao cha dharura ya kuwatosa wananchi na kuwalinda wezi, kwa maana ya kutoweka saini ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Ila Zitto tayari ana sahihi ya Deo na Zambi.



tena wafanye haraka sana
 
zito kazini anatafuta kura za wabunge 71

sababu bunge halina meno ya kuwawajibisha mawaziri ila wabunge wanauwezo wa kumwajibisha waziri mkuu

swali:

Wakina filikunjombe watatoa saini kumwajibisha wanaojiita mwanachama mwenzake?

Wananchi tuone wabunge wetu wapo kweli au ni kerere za chura

imani yangui kwa zitto imeongezeka maradufu.
Sasa naona ni jinsi gani anavyofaa kuwa rais wa tanzania.
Zitto wewe ni kiboko aisee.
 
Back
Top Bottom