Wabunge kumjadili Kikwete

MiratKad

JF-Expert Member
May 2, 2008
294
3
Shinikizo zuri, kutoka kwa wabunge. Zitto, Slaa nk fanyeni kweli. JK anatakiwa kuongoza nchi na kuchukua hatua ambazo hazitawafurahisha maswahiba wake sio kuleta usanii wa waziwazi.

Wabunge kumjadili Kikwete

na Salehe Mohamed



BUNGE la Jamhuri ya Muungano wiki ijayo litapata nafasi ya kujadili hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa juzi ambayo tayari imeibua maswali mengi ya chini chini.

Hatua hiyo ya Bunge kwa kiwango kikubwa inaweza kuirejesha upya hoja ya wizi wa shilingi bilioni 133 kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Uwezekano wa kurejeshwa kwa suala hilo unaonekana kuwa mkubwa kutokana na ukweli kwamba, tayari baadhi ya wabunge wamesikika chini chini wakisikitikia uamuzi wa rais kuamua kulimaliza kistaarabu.

Baadhi ya wabunge waliozungumza na Tanzania Daima kwa masharti ya majina yao kutotajwa hadi hapo watakapochangia mjadala wa hotuba ya rais wanasema, uamuzi wa Kikwete kutochukua mkondo wa kisheria dhidi ya makampuni 13 yaliyoiba shilingi bilioni 90 kupitia EPA kwa kutumia nyaraka za kughushi unaonekana kutaka kuwanusuru baadhi ya watu.

Wasiwasi huo wa baadhi ya wabunge unaweza kupimwa pia na kauli zilizotolewa juzi na jana na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambaye amemwagiza Katibu wa Bunge kupanga ratiba kwa ajili ya kuijadili hotuba hiyo ya rais.

Sitta ambaye alikiri kupokea maombi mengi ya wabunge wanaotaka kuchangia bajeti hiyo, alisema masuala mengi muhimu aliyozungumzia rais katika hotuba yake, hayana budi kujadiliwa na wabunge.

Alisema lengo la wabunge ni kumsaidia rais kuiendesha nchi ili waweze kuleta maendeleo kwa wananchi ambao wana kiu kubwa ya kuona viongozi wao wakipambana na mambo yanayokwamisha ukuaji wa maendeleo katika sekta mbalimbali.

“Nimepokea maombi mengi ya wabunge, wakitaka hotuba ile ya Rais Kikwete ijadiliwe na mimi kutokana na umuhimu wa yale yaliyosemwa, nimekubaliana nayo. Tutachapisha kitabu na pia nimemuagiza Katibu wa Bunge, apange ratiba na siku ya kuijadili,” alisema Sitta.

Alisema wameamua kuijadili katika mkutano huu unaoendelea wakati ikiwa motomoto, kwani wakisubiri mkutano ujao, wabunge wengi wanaweza wasichangie kwa kiwango kinachotakiwa kama ilivyo sasa ambapo kumezuka masuala mengi yanayohitaji njia madhubuti kukabiliana nayo.

Akizungumza kwa kujiamini, Sitta alisema katika hali ya kawaida wabunge wanapenda kuona watu wote waliohusishwa na tuhuma za kuhujumu mali za wananchi wakifikishwa katika vyombo vya sheria.

Alisema vinginevyo watuhumiwa hao wanaweza wakaanza kutembea vifua mbele barabarani na kuwadhihaki wale wote waliokuwa wakipiga kelele ya kutaka wawajibishwe.

Sitta alirejea kauli aliyoitoa juzi muda mfupi baada ya Kikwete kumaliza kuhutubia akisema rais anapaswa kuwa mkali kwa hivi sasa ili kurekebisha baadhi ya tabia za watendaji ambao wanafikiri hawawezi kuwajibishwa, kwa sababu ya nyadhifa walizonazo au uhusiano na watu mbalimbali na kusahau kuwa, nyadhifa hizo walipewa ili wawahudumie wananchi na si vinginevyo.

Alisema juzi wakati akitoa shukrani kwa rais, alimwambia, wabunge wapo tayari kumsaidia hasa kwa kurekebisha baadhi ya sheria ambazo kwa namna moja au nyingine zinawalinda watu waliohujumu rasilimali za nchi kwa kisingizio kwamba kuwashughulikia ni ukiukaji wa haki za ubinadamu na utawala bora.

“Nilishamwambia kuwa hakuna maana kama utawala bora unatoa haki kwa mtu mmoja mmoja na kuwasahau walio wengi na kama kikwazo ni hizo taratibu, azilete hapa tuzifanyie marekebisho ili tuweze kuwabana zaidi.

Nchi zilizoendelea ziliweza kufika hapo zilipo kwa kuangalia haki za wengi na si za mtu mmoja mmoja ambaye anahujumu rasilimali za taifa kwa masilahi binafsi,” alisema Sitta, kauli ambayo baadhi ya wabunge waliozungumza na Tanzania Daima wameitafsiri kuwa kielelezo cha kutoridhishwa kwake na hatua za Kikwete kuliweka kando suala zima la wizi katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA).

Matamshi hayo ya spika kwa kiwango kikubwa yanakumbusha kauli iliyopata kutolewa katika Bunge hili la bajeti na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, ambaye alisema iwapo wezi wa EPA wasiporudisha fedha walizoiba, basi bungeni pasingetosha.

Kilango ambaye alikuwa akichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2008/09 aliitaka serikali kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kuwa shilingi bilioni 133 zilizoibwa Benki Kuu (BoT) kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) zinarejeshwa.

Kilango ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge na mmoja wa wabunge waliokuwa mstari wa mbele kulaani ufisadi katika kashfa ya Richmond, Februari mwaka huu, aliitaka serikali kuhakikisha wale wote waliokopa kiasi kinachofikia shilingi bilioni 216 kupitia mpango wa uagizaji bidhaa (Import Support) mwaka 1992 wanazirejesha fedha hizo mara moja.

Katika hatua ambayo haikutarajiwa, Kilango alirejea tena kauli aliyopata kuitoa siku zilizopita pale aliposema kuwa alikuwa yuko tayari kupoteza maisha ili kuhakikisha kuwa fedha hizo zinarudishwa.

“Mwanafalsa wa Kigiriki, Socrates siku moja alipokuwa sokoni, alihubiri kuwa, watu wengi makini duniani huwa wako tayari kufa kwa ajili ya kile wanachokiamini, ukweli na haki. Alipotakiwa kuikana kauli yake, halisema hawezi, wakampa sumu, akanywa, akafa kwa kusimamia ukweli.

“Mheshimiwa Spika, tumebaki kulalamikia ufinyu wa mapato ya ndani, lakini tumesahau kuwa, fedha nyingi zinaliwa na kikundi cha watu wachache.

‘‘Watu wameiba fedha za EPA, Rais anataka fedha hizo zirejeshwe na mimi nasema siogopi vitisho, fedha hizo zisiporudishwa, hapa patachimbika, patakuwa hapatoshi hapa, Mheshimiwa Spika.

“Fedha hizo ni mali ya wananchi wa jimbo la Same, Igunga, Kigoma Mjini na majimbo mengine yote. Lazima zirejeshwe. Mimi sitakata kauli ya kutaka fedha hizo zirudi, wananchi huko nje tulieni, wabunge tufanye kazi,” alisisitiza Kilango Juni 19, mwaka huu.

Wakati akitaka fedha hizo zirejeshwe, mbunge huyo aliilalamikia serikali kwa kuachia mianya iliyosababisha wajanja wachache kuchota mabilioni hayo, huku ikiacha mamilioni ya Watanzania wakiwa katika lindi kali la umaskini.

Alisema mianya ya ufisadi ipo pia kwenye sekta ya madini, mbunga za wanyama na misitu.

Akitoa mfano wa nchi zinazolinda na kujivunia rasilimali zake, Kilango alisema Libya inajivunia gesi yake na Falme za Kiarabu zinajivunia mafuta ya petroli ambayo leo kila kona ya dunia inalia kuhusu kupanda kwa bei ya malighafi hiyo.

Katika hilo alisema ni jambo la ajabu kwamba hapa nchini madini kama tanzanite, almasi na rasilimali zingine, hazimnufaishi Mtanzania kwa kiasi cha kumfanya ajivunie.

Mbali ya Kilango, siku hiyo hiyo Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazue (CCM) alitaka mafisadi wa EPA watajwe kwa majina bungeni ili kujenga imani kwa wananchi.

Alisema wananchi hawawezi kudanganywa kila siku na wakishajua wanadanganywa, watakosa imani na serikali yao.

Aidha, katika hatua nyingine jana, Spika Sitta, alisema utoro bungeni hivi sasa unaelekea kushika kasi na yupo mbioni kuwataja wabunge wote ambao hawashiriki kikamilifu kwenye vikao vya Bunge na hawajali kama jambo hilo lina athari kwa Bunge na wapiga kura wao.

Alisema kuna wabunge ambao hawashiriki katika vikao vya kamati mbalimbali lakini pia hawahudhurii kwa kiwango kinachotakiwa katika Bunge hilo.

“Jamani sasa naona hali ya utoro inazidi kushamiri na nimevumilia kwa muda mrefu sasa inabidi niliseme hadharani, kwani kuna wabunge hawaonyeshi kujali, nina mpango wa kuanza kutaja majina ya wabunge ambao hawashiriki kikamilifu katika Bunge,” alisema Sitta.

Sitta, pia aliwataja mawaziri ambao wanashiriki kikamilifu katika shughuli za Bunge kuwa ni Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Celine Kombani na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Mary Nagu.
 
Usiwe ni mkakati wa kutaka kufukia mashimo yaliyoachwa na muungwana[/QUOTE

......yawezekana ikawa hivyo,

Je, itakuwa katika muelekeo gani hasa? Naomba iwe katika muelekeo wa kutufurahisha wananchi. Vinginevyo ni mchezo ule ule wa ndio mzee.
 
'Itifaki ikizingatiwa' sioni namna ambavyo wale wa CCM watakavyosimama na kumponda bosi wao
 
Usiwe ni mkakati wa kutaka kufukia mashimo yaliyoachwa na muungwana

Sidhani kama itakuwa hivyo ila naamini kwanza kitendo cha Spika kusema wazi immediatelly baada ya prezidaa kuhutubu kwamba awe mkali na asiwasamehe mafisadi kwa kusemea haki za binadamu kinatupa picha ya wazi kwamba hata Spika sasa anapiga vita mafisadi. Nadhani ni kutokana na ukweli kwamba hata yeye sasa yuko kwenye list ya kuhujumiwa na mafisadi hao hao na anaona hatari pale prezidaa anapowaacha waendelee kumwaga unga bungeni, safari ile ilibuma lakini wasiposhughulikiwa sasa wanaweza kumwaga unga mwingine wa hatari zaidi na ukafanya kazi. Sio hivyo tu, kambi nzima ya wanaojijua wameumuka tumbo zao na nywele kuwa nyeupe sana kwa ufisadi wanafanya kila wawezalo kuzima huu moto kwa kupambana na wahusika na wasimamizi. Mmojwapo ni Spika ambaye anaruhusu mijadala kuhusu mafisadi badala ya kuizima kama Msekwa yule mbabe wa zamani bungeni.
 
'Itifaki ikizingatiwa' sioni namna ambavyo wale wa CCM watakavyosimama na kumponda bosi wao

Hii inaweza kuwa kweli, "collective responsibility"...! Lakini kama hawajaikubali hotuba ya mkuu wao maongezi yao yataonyesha. Hawataponda moja kwa moja, wataipongeza kisha watatoa ushauri hasa kwa minajili ya kumsaidia zaidi Bwana Mkubwa kwamba mahala fulani akifanya hivi yawezekana pia mambo yakawa mazuri zaidi. Hiyo hata protocol inakubali, reference ni kwa Sitta ambaye alitoa ushauri on the spot.
 
Usiwe ni mkakati wa kutaka kufukia mashimo yaliyoachwa na muungwana

Mpita Njia,

Labda haujamuelewa Sitta, nadhani sita anataka kukufua hoja hii, na hii ndilo litakuwa jambo likalodhohofisha uelekeo wa CCM. Nadhani hapa ndipo vyama vya upinzani tungejipanga na kufanaya mageuzi ya kweli kwa kutumia huo udhaifu wa CCM.
 
'Itifaki ikizingatiwa' sioni namna ambavyo wale wa CCM watakavyosimama na kumponda bosi wao

..siasa zimebadilika, wanaweza kumponda [kiaina] vilevile!

..nadhani spika na wabunge kadhaa hawakuridhika na ile hotuba.

..watu wanahamu ya damu ya mtu!
 
Kikwete ameonyesha tena kutojua kusoma alama za nyakati kwa kuwakumbatia mafisadi wakati nchi nzima inazizima kwa habari za kusikitisha za mafisadi. Kisingizio cha haki za binadamu ni danganya toto kwani ukitaka kufuata haki za binadamu kweli itabidi umfungulie kila mfungwa Tanzania kwani hamna gereza linalofikia standards za kimataifa kumfunga mtu kwa misingi ya haki za binadamu. Kwa hiyo mheshimiwa kama unapenda sana haki za binadamu waachie wafungwa wote Tanzania, tujenge magereza yenye standards then tutaanza process upya.


Hizi habari, ukitilia maanani kauli za that rookie PM Mizengo Pinda kwamba hawa mafisadi ni watu wakubwa na wenye nguvu sana, zinaonyesha hata Kikwete mwenyewe anagwaya.Huenda anahusika moja kwa moja au watu wake wa karibu sana wanahusika. Sasa hivi watatfuta bangusilo wawili watatu wa katikati, kuwapa option ya kulipa au kufungwa ki Pablo Escobar kwenye vi "Penthouse jail cells" zinazoandaliwa sasa hivi.

Halafu hapo hapo Speaker Sitta naye amepata pa kutokea, anajua kusoma signs za nyakati na kama mwanamuziki anayetaka kufurahisha wapenzi kwa kutunga nyimbo yenye maudhui yanayokwenda na wakati, Speaker Sitta amem-slam rais wake live live.

JK asipoangalia CCM wenyewe wanaweza kumfanyia mkakati wa kumtoa na kumuweka bwege mwingine kama Sitta, admittedly far fetched for the morose and top down CCM, lakini kama watu wanataka kuijadili hotuba yake - unprecedented, up to now the president's speech was final- then sitashangaa watu wakianza kampeni za chini chini kumuondoa muungwana 2010.
 
..siasa zimebadilika, wanaweza kumponda [kiaina] vilevile!

..nadhani spika na wabunge kadhaa hawakuridhika na ile hotuba.

..watu wanahamu ya damu ya mtu!

Hakuna kitu hilo bunge afadhali na BUNGE la DARUSO

wananchi wangekua wanataka maendeleo wala hakuna haja ya kuwasikiliza hao jamaa,mnapoteza mda tu kujaribu kupata matumaini kutoka kwa WABUNGE wasanii wote kwa pamoja ccm na wapinzani.

Ukombozi haupatikani kwa kuongea sana ,unatafutwa kwa vitendo.Wananchi lazima tuamke tushinikize mambo ya ufisadi tuyaachane nayo tuangalie kwanza katiba.

Huu uhuni ili ukome mimi ningeomba mambo haya yafanyike.

1.Rais agombee kupata urais.
2.waziri mkuu naye agombee kupata uwaziri mkuu.
3.mawaziri nao wateuliwe na waziri mkuu na wasiwe wabunge.
hapo mimi nadhani ndipo tutaweza kuwajibishina.
 
Mpita Njia,

Labda haujamuelewa Sitta, nadhani sita anataka kukufua hoja hii, na hii ndilo litakuwa jambo likalodhohofisha uelekeo wa CCM. Nadhani hapa ndipo vyama vya upinzani tungejipanga na kufanaya mageuzi ya kweli kwa kutumia huo udhaifu wa CCM.


Sitta raised a star siku ile kwa uchache wa maneno yake ambayo yaliifunika kabisa hotuba nzima ya JK ya masaa makadhaa .It is about time sasa Wabunge wasimame na hasa wale wa Upinzani .Wananchi kazi kubwa ni kusimama nyuma ya wabunge wenye nia ya Utaifa na maendeleo ya Nchi .Hoja hii isife kwa ujanja tu .Watu kama Zitto , Slaa kupitua hoja hi na Richmond walipata shida nyingi na sisi sasa lazima kusimama na kusema Upinzani unaweza na kupunguza idadi ya wana CCM mwaka 2010
 
Mie naona mzizi wa fitina ukatwe prof. mkandara aitishe economic forum jk slaa na lipumba kila mmoja afanye presentation, then tuone kichwa ni kipi. Mbowe hatumhitaji is the oldest undergraduate student in uk hana cha kutueleza.

Mie nadhani presentation ya jk bado ninzuri, jk katuonesha njia kuwa tunahitaji tuwe na arbitration and mitigation round tables hasa kwa masuala yaliyokaa kibiashara zaidi. Nyie! sio kila ndoa yenye mgogoro inahitaji taraka, zingine zinahitaji usuluhishi tu.

Jamani Kibaki alimtia korokoroni ketan somaia yule bwana akaishi maisha raha mustarehe huko jela na fedha hazikurudi. Sokoine aliweka korokoroni wafanyabiashara nchi nzima wala nafuu ya maisha haikupatikana.
 
Back
Top Bottom