Shinikizo zuri, kutoka kwa wabunge. Zitto, Slaa nk fanyeni kweli. JK anatakiwa kuongoza nchi na kuchukua hatua ambazo hazitawafurahisha maswahiba wake sio kuleta usanii wa waziwazi.
Wabunge kumjadili Kikwete
na Salehe Mohamed
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wiki ijayo litapata nafasi ya kujadili hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa juzi ambayo tayari imeibua maswali mengi ya chini chini.
Hatua hiyo ya Bunge kwa kiwango kikubwa inaweza kuirejesha upya hoja ya wizi wa shilingi bilioni 133 kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).
Uwezekano wa kurejeshwa kwa suala hilo unaonekana kuwa mkubwa kutokana na ukweli kwamba, tayari baadhi ya wabunge wamesikika chini chini wakisikitikia uamuzi wa rais kuamua kulimaliza kistaarabu.
Baadhi ya wabunge waliozungumza na Tanzania Daima kwa masharti ya majina yao kutotajwa hadi hapo watakapochangia mjadala wa hotuba ya rais wanasema, uamuzi wa Kikwete kutochukua mkondo wa kisheria dhidi ya makampuni 13 yaliyoiba shilingi bilioni 90 kupitia EPA kwa kutumia nyaraka za kughushi unaonekana kutaka kuwanusuru baadhi ya watu.
Wasiwasi huo wa baadhi ya wabunge unaweza kupimwa pia na kauli zilizotolewa juzi na jana na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambaye amemwagiza Katibu wa Bunge kupanga ratiba kwa ajili ya kuijadili hotuba hiyo ya rais.
Sitta ambaye alikiri kupokea maombi mengi ya wabunge wanaotaka kuchangia bajeti hiyo, alisema masuala mengi muhimu aliyozungumzia rais katika hotuba yake, hayana budi kujadiliwa na wabunge.
Alisema lengo la wabunge ni kumsaidia rais kuiendesha nchi ili waweze kuleta maendeleo kwa wananchi ambao wana kiu kubwa ya kuona viongozi wao wakipambana na mambo yanayokwamisha ukuaji wa maendeleo katika sekta mbalimbali.
Nimepokea maombi mengi ya wabunge, wakitaka hotuba ile ya Rais Kikwete ijadiliwe na mimi kutokana na umuhimu wa yale yaliyosemwa, nimekubaliana nayo. Tutachapisha kitabu na pia nimemuagiza Katibu wa Bunge, apange ratiba na siku ya kuijadili, alisema Sitta.
Alisema wameamua kuijadili katika mkutano huu unaoendelea wakati ikiwa motomoto, kwani wakisubiri mkutano ujao, wabunge wengi wanaweza wasichangie kwa kiwango kinachotakiwa kama ilivyo sasa ambapo kumezuka masuala mengi yanayohitaji njia madhubuti kukabiliana nayo.
Akizungumza kwa kujiamini, Sitta alisema katika hali ya kawaida wabunge wanapenda kuona watu wote waliohusishwa na tuhuma za kuhujumu mali za wananchi wakifikishwa katika vyombo vya sheria.
Alisema vinginevyo watuhumiwa hao wanaweza wakaanza kutembea vifua mbele barabarani na kuwadhihaki wale wote waliokuwa wakipiga kelele ya kutaka wawajibishwe.
Sitta alirejea kauli aliyoitoa juzi muda mfupi baada ya Kikwete kumaliza kuhutubia akisema rais anapaswa kuwa mkali kwa hivi sasa ili kurekebisha baadhi ya tabia za watendaji ambao wanafikiri hawawezi kuwajibishwa, kwa sababu ya nyadhifa walizonazo au uhusiano na watu mbalimbali na kusahau kuwa, nyadhifa hizo walipewa ili wawahudumie wananchi na si vinginevyo.
Alisema juzi wakati akitoa shukrani kwa rais, alimwambia, wabunge wapo tayari kumsaidia hasa kwa kurekebisha baadhi ya sheria ambazo kwa namna moja au nyingine zinawalinda watu waliohujumu rasilimali za nchi kwa kisingizio kwamba kuwashughulikia ni ukiukaji wa haki za ubinadamu na utawala bora.
Nilishamwambia kuwa hakuna maana kama utawala bora unatoa haki kwa mtu mmoja mmoja na kuwasahau walio wengi na kama kikwazo ni hizo taratibu, azilete hapa tuzifanyie marekebisho ili tuweze kuwabana zaidi.
Nchi zilizoendelea ziliweza kufika hapo zilipo kwa kuangalia haki za wengi na si za mtu mmoja mmoja ambaye anahujumu rasilimali za taifa kwa masilahi binafsi, alisema Sitta, kauli ambayo baadhi ya wabunge waliozungumza na Tanzania Daima wameitafsiri kuwa kielelezo cha kutoridhishwa kwake na hatua za Kikwete kuliweka kando suala zima la wizi katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA).
Matamshi hayo ya spika kwa kiwango kikubwa yanakumbusha kauli iliyopata kutolewa katika Bunge hili la bajeti na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, ambaye alisema iwapo wezi wa EPA wasiporudisha fedha walizoiba, basi bungeni pasingetosha.
Kilango ambaye alikuwa akichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2008/09 aliitaka serikali kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kuwa shilingi bilioni 133 zilizoibwa Benki Kuu (BoT) kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) zinarejeshwa.
Kilango ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge na mmoja wa wabunge waliokuwa mstari wa mbele kulaani ufisadi katika kashfa ya Richmond, Februari mwaka huu, aliitaka serikali kuhakikisha wale wote waliokopa kiasi kinachofikia shilingi bilioni 216 kupitia mpango wa uagizaji bidhaa (Import Support) mwaka 1992 wanazirejesha fedha hizo mara moja.
Katika hatua ambayo haikutarajiwa, Kilango alirejea tena kauli aliyopata kuitoa siku zilizopita pale aliposema kuwa alikuwa yuko tayari kupoteza maisha ili kuhakikisha kuwa fedha hizo zinarudishwa.
Mwanafalsa wa Kigiriki, Socrates siku moja alipokuwa sokoni, alihubiri kuwa, watu wengi makini duniani huwa wako tayari kufa kwa ajili ya kile wanachokiamini, ukweli na haki. Alipotakiwa kuikana kauli yake, halisema hawezi, wakampa sumu, akanywa, akafa kwa kusimamia ukweli.
Mheshimiwa Spika, tumebaki kulalamikia ufinyu wa mapato ya ndani, lakini tumesahau kuwa, fedha nyingi zinaliwa na kikundi cha watu wachache.
Watu wameiba fedha za EPA, Rais anataka fedha hizo zirejeshwe na mimi nasema siogopi vitisho, fedha hizo zisiporudishwa, hapa patachimbika, patakuwa hapatoshi hapa, Mheshimiwa Spika.
Fedha hizo ni mali ya wananchi wa jimbo la Same, Igunga, Kigoma Mjini na majimbo mengine yote. Lazima zirejeshwe. Mimi sitakata kauli ya kutaka fedha hizo zirudi, wananchi huko nje tulieni, wabunge tufanye kazi, alisisitiza Kilango Juni 19, mwaka huu.
Wakati akitaka fedha hizo zirejeshwe, mbunge huyo aliilalamikia serikali kwa kuachia mianya iliyosababisha wajanja wachache kuchota mabilioni hayo, huku ikiacha mamilioni ya Watanzania wakiwa katika lindi kali la umaskini.
Alisema mianya ya ufisadi ipo pia kwenye sekta ya madini, mbunga za wanyama na misitu.
Akitoa mfano wa nchi zinazolinda na kujivunia rasilimali zake, Kilango alisema Libya inajivunia gesi yake na Falme za Kiarabu zinajivunia mafuta ya petroli ambayo leo kila kona ya dunia inalia kuhusu kupanda kwa bei ya malighafi hiyo.
Katika hilo alisema ni jambo la ajabu kwamba hapa nchini madini kama tanzanite, almasi na rasilimali zingine, hazimnufaishi Mtanzania kwa kiasi cha kumfanya ajivunie.
Mbali ya Kilango, siku hiyo hiyo Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazue (CCM) alitaka mafisadi wa EPA watajwe kwa majina bungeni ili kujenga imani kwa wananchi.
Alisema wananchi hawawezi kudanganywa kila siku na wakishajua wanadanganywa, watakosa imani na serikali yao.
Aidha, katika hatua nyingine jana, Spika Sitta, alisema utoro bungeni hivi sasa unaelekea kushika kasi na yupo mbioni kuwataja wabunge wote ambao hawashiriki kikamilifu kwenye vikao vya Bunge na hawajali kama jambo hilo lina athari kwa Bunge na wapiga kura wao.
Alisema kuna wabunge ambao hawashiriki katika vikao vya kamati mbalimbali lakini pia hawahudhurii kwa kiwango kinachotakiwa katika Bunge hilo.
Jamani sasa naona hali ya utoro inazidi kushamiri na nimevumilia kwa muda mrefu sasa inabidi niliseme hadharani, kwani kuna wabunge hawaonyeshi kujali, nina mpango wa kuanza kutaja majina ya wabunge ambao hawashiriki kikamilifu katika Bunge, alisema Sitta.
Sitta, pia aliwataja mawaziri ambao wanashiriki kikamilifu katika shughuli za Bunge kuwa ni Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Celine Kombani na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Mary Nagu.