Wabunge kujengewa nyumba kama mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge kujengewa nyumba kama mawaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Na Ramadhan Semtawa

  WABUNGE sasa watakuwa na makazi yao maalumu mjini Dodoma maarufu kama Bunge Estate, sawa na ilivyo kwa mawaziri jijini Dar es Salaam na Dodoma, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuweka bayana mpango huo kwa wawakilishi hao.

  Mradi huo mkubwa na wa kisasa ambao umewakuna wabunge wanaohudhuria semina elekezi ya siku kumi, unatekelezwa kwa pamoja kati ya Ofisi ya Bunge na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), huku ukitarajiwa kuathiri biashara ya nyumba za kukodi na hoteli.

  Kwa mujibu wa duru za habari za kuaminika kutoka katika semina hiyo kisha kuthibitishwa na Makinda, zilifafanua kwamba hatua iliyofikiwa hadi sasa ni mchoro wa ramani ya eneo la mradi, huku shabaha ikiwa hadi katikati mwakani kuwe na nyumba zilizojengwa.

  "Ndiyo, huo mradi tulikuwa tukiujadili hapo ndani (ukumbi wa semina). Ni mradi ambao tutashirikiana na wenzetu wa NHC (Shirika la Nyumba)," alithibitisha Spika Makinda.

  Kwa mujibu wa Makinda, kitu cha kwanza kilichokuwa kikifanyiwa kazi ni kupata eneo na sasa kinachofanyika ni michoro.
  "Kuhusu gharama bado hatujapata kwa sababu ndio kwanza mradi uko hatua za awali," alisema.
  Aliendelea kuwa, NCH kazi yao ni kujenga nyumba hizo huku Ofisi ya Bunge ikijipanga kurejesha fedha hatua kwa hatua kipindi cha miaka isiyopungua sita.

  Spika Makinda alifafanua kwamba, wabunge watatozwa kiasi cha fedha kitakachoamuliwa kama sehemu ya kusaidia kurejesha deni hilo hapo baadaye.

  Makinda akithibitisha hayo, duru za ndani ya semina zilizidi kuweka hadharani mpango huo kwamba, zitakuwa nyumba 350 ambazo kati ya hizo 200, zitakuwa kwenye muundo wa ghorofa na nyingine 150 za chini na hautakuwa mbali na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

  Kwa mujibu wa chanzo hicho huru, ili kuhakikisha nyumba hizo zinabaki kuwa mali ya Bunge, kila mbunge atakaa kwa muda wa miaka mitano na kuongeza: "ikimalizika unaondoka na familia yako."

  Chini ya mpango huo, Makinda na Naibu wake, Job Ndugai, waliufafanua vema kwa wabunge kuhusu usimamizi wa mradi huo kuhakikisha unanufaisha wabunge wapya watakaokuwa wakiingia bungeni.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Huu ni ufisadi mwingine unakuja............................siyo kazi ya serikali kuwajengea nyumba watumishi wake...................................ila kazi ya serikali ni kuwalipa fedha zinazokidhi mahitaji yao ya kila siku na kuliachia soko huru kwatatulia matatizo yao ikiwemo la kujenga nyumba............................
   
 3. H

  Haika JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kwa kuwa miradi ya ujenzi ndio sehemu laini ya kula Tanzania hasa serikalini, lazima ofisi ya bunge iwe makini katika kufikiria wale wapi, sasa ujenzi wa jengo la bunge umekamilika unadhani wataweza kuwahamisha watoto shule? Wawapeleke shule za kata???

  No way, lazima kila kitengo chini ya serikali kiwe makini katika kuhakikisha miradi ya ujenzi ipo, baada ya hapo watapata tu kitu kingine.

  Mimi nahoji hiyo bajeti kwanini isitoke au isiwe chini ya mamlaka ya ustawishaji Makao Makuu, si ndio ilikuwa lengo la kuanzishwa kwake?
   
 4. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Iwapo kuna wabumge makini ambao wapo kwa ajili ya maslahi ya wananchi inabidi waupinge mpango huu kwa sababu ni ufujaji wa kodi za wananchi.

  Hizo pesa zitumike kununua vifaa vya maabara mashuleni na kununua reference books.

  Wabunge ni waajiriwa kama waajiriwa wengine hapa nchini. Hivyo jukumu la serikali ni kuwalipa mishahara na ni wajibu wa wabunge kutafuta makazi yao.

  Viongozi wa serikali ya ccm mbona wana matatizo vichwani mwao? Wameona hii ndio priority kweli?
   
Loading...