Wabunge: Kaza Buti

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
251
11
Wabunge wembe huo huo

Habari Zinazoshabihiana
• Wabunge hii ni changamoto kwenu 27.01.2008 [Soma]
• Cheyo, Ole Sendeka waungwe mkono 03.02.2008 [Soma]
• Rais Kibaki kafanya usanii? 10.01.2008 [Soma]

JUZI semina ya wabunge iliyokuwa ikijadili Muswada wa Sheria za Umeme na Biashara ya Mafuta, ilivunjika kutokana na wabunge waliokuwa wakishiriki kukataa kuendelea nayo baada ya kubaini ubabaishaji katika yaliyokuwa yakielezwa.

Wabunge hao walionesha dhahiri kukerwa na kinachoendelea ndani ya Wizara ya Nishati na Madini na kuona kuwa kuendeleza blah blah kama hizo ni hatari kwao na kwa wananchi, ambao ni wapiga kura kwa ujumla na kutaka wasubiri kikao cha Bunge ili kuyamaliza.

Tunachukua fursa hii kuwapongeza wabunge hao kwa ujasiri huo ambao kwa kweli una malengo ya kuhakikisha kuwa wananchi wanatetewa kwa maslahi yao na ya Taifa kwa ujumla.

Ni dhahiri wabunge hao wameonesha njia kwa wenzao, kwamba kinachotakiwa hivi sasa ni kuangalia maslahi ya nchi bila kujali itikadi ya vyama vyao ambayo hapo awali imekuwa ikiwapa fursa ya malumbano kwa maslahi binafsi.

Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikilalamikiwa kwa mambo mengi na kwa bahati mbaya pengine wanaoisimamia hawajaelewa kuwa ni Wizara muhimu kwa maisha ya wananchi na hivyo kila mwananchi anaguswa nayo kwa namna moja au nyingine.

Ukali waliouonesha wabunge katika semina hiyo, tunatarajia watauendeleza hata katika masuala mengine yanayohusu maslahi ya wananchi na Taifa lao na hatimaye kuona Bunge kweli ni mahali pa kulinda maslahi ya nchi.

Wabunge wakiendelea na ujasiri huu ambao ndiyo hasa majukumu yao, watakuwa wamemsaidia Rais Jakaya Kikwete katika kukabiliana na matatizo ya nchi na kumpa nafasi ya kushughulikia masuala mengine ya msingi.
 
Back
Top Bottom