Wabunge jipumzisheni vya kutosha kuepusha aibu ya kulala Bungeni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge jipumzisheni vya kutosha kuepusha aibu ya kulala Bungeni!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rich Dad, Jul 3, 2011.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwili wa binadamu si sawa na mashine yenye uwezo wa kufanya kazi 24 hrs na bado efficiency yake ikawa maintained. Mwili pamoja na akili inatakiwa kupumzishwa vya kutosha, kinyume na hapo performance yaweza kushuka au kufanya mambo yasiyotakiwa kwa wakati huo.
  Picha za hivi karibuni zinazowaonesha baadhi ya wabunge wakiwa wamelala huku mijadala mbalimbali ikiendelea zina tafsiri tofautitofauti. Baadhi ya tafsiri zinaweza kuwa ni kama ifuatavyo;
  1) Wabunge wetu wanadharau,hawana umakini au hawajui wajibu wao; haiwezekani wewe ni waziri mwenye dhamana unalala huku mijadala yenye kuamua mustakabali wa taifa letu ikiendelea.
  2) Wabunge wetu wanatumika sana baada ya vikao vya bunge, na hasa nyakati za usiku. Usiniulize wanatumikaje, sitaweza kukujibu.
  3) Labda watakuwa wagonjwa, maana kuna ugonjwa wa malale ( sleeping sickness), ambao humfanya mtu kutaka kulala wakati wote.
  4) Au ukumbi wa bunge unajoto ambalo sio rafiki kwa baadhi ya wabunge? Unaweza kukuta ni sababu pia.
  5) Uhakika wa posho upo, kwa hivyo hata ukilala posho yako iko palepale.

  Mwisho kabisa niseme hivi; ukikopa usingizi jua ya kwamba utaulipa tu!!! Sasa ni aibu kulipa sehemu ambayo watu wapo serious wanajadili mambo ya kitaifa.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sababu zote 5 ulizotaja zinachangia sana walalelale hovyo lakini wale wanaolala mpaka udenda mrefu uteremke hadi kwenye shati mi nadhani no. 2 inawahusu zaidi
   
 3. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Unafikiri hawapati muda wa kutosha wa kupumzika? Tuonyesheni kama kuna mfano wowote wa mbuge kutoka vyama vya upinzani anayechapa usingizi bungeni? Ni aibu kubwa hata waziri kulala bungeni. Kama amechoka si bora tu akaondoka?

  Wakizinduka kutoka usingizini wanaanza kupiga makofi. Kila hoja za CCM lazima zipite. Wabunge kuwa sehemu ya serikali. Hii naisikia tz. Kuna dola 3 (Bunge , serikali na mahakama). Haziwezi kuwa Utatu Mtakatifu. lkn kwa tz bunge na mahakama ni sehemu ya serikali.

  Ajabu na kweli
   
Loading...