Wabunge hili la Utamaduni laweza kuwa Bomu la Atomic! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge hili la Utamaduni laweza kuwa Bomu la Atomic!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMBOTA, Apr 6, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mbili mtu.jpeg

  …kambi ya upinzani inaona umefika muda wa vyombo vya habari kutangaza kwa lugha za asili….

  Haya ni maneno ya mbunge wa Mbeya mjini (CHADEMA) Bw Joseph Desmund Mbilinyi ambaye pia anafahamika kama Sugu huyu ni mwasisi wa muziki wa HipHop nchini, Mbilinyi aliyasema haya jana kwenye kikao cha bunge huko Dodoma wakati akisoma taarifa ya kambi ya upinzani , bilashaka ni moja kati ya taarifa iliyokuwa ya kusisimua sana miongoni mwa wabunge kiasi kwamba naajihoji kwanini iliwasisimua?
  Haya yanafuatia kile kinachoitwa kuridhia mkataba wa kimataifa unaolenga kulinda tamaduni za watu ambayo Tanzania ilikuwa bado haijaridhia lakini hata hivyo dalili zishaanza kuonekana kuwa muda si mrefu tutaridhia na kuanza jukumu la kulinda tamaduni zetu. Hili la kulinda tamaduni linaniibulia swali moja la msingi kwani watanzania hatulindi tamaduni zetu? , hata hivyo inatosha kusema kuwa kuna udhaifu mkubwa sana katika swala hili ili nieleweke katika uchambuzi wangu huu nitajadili na kupembua mambo kwa misingi ya hoja ili hata ikibidi nijibiwe iwe pia kwa misingi ya hoja na mantiki.
  Kwanza kabisa katika hali ya kawaida huwezi kujadili mambo ya baadaye bila kuangalia ulipotoka na ulipo hivyo kwa mantiki hiyo nilitegemea wabunge wetu wajadili utamaduni wetu umetoka wapi na upo wapi? Hii ingewasaidia kubaini kwanini mwasisi wa taifa hili hayati baba wa taifa Mwallimu Julius Kambarage Nyerere alihimiza sana matumizi ya Kiswahili na kuwataka watu wengi wazungumze Kiswahili kuliko lugha zao za asili, haya ni maswali ambayo hayapaswi kutolewa majibu rahisi rahisi, badala yake nimeona wabunge wakijikita tu kwenye hoja ya kulinda tamaduni zetu pasipo kuichambua hoja hiyo kiundani,haina ubishi hili ni tatizo!
  Ikumbukwe kuwa watanzania wanalinda tamaduni zao tena wanazipenda sana, kwa jinsi hali ilivyo watanzania waishio vijijini wengi wao wanafahamu tamaduni zao hivyo kwangu mimi nilitegemea mkakati huu uwe maalumu kwa vijana wanaoishi mijini lakini nishaanza kuona mapungufu tayari, najaribu kujiuliza swali jepesi kuwa mbona mkakati huo naona hauwagusi vijana wa mijini, hivi serikali inamkakati gani wa kuhakikisha kuwa vijana wa mijini wanafahamu tamaduni zao na hapa wasije kujibu tu kuwa watasoma darasani kama mbunge mmoja jana alivyosema bungeni, kusoma ndio nini? wengi wanasoma hoja ni jinsi ya kuzifanya kwa vitendo mila na tamaduni hizo pia kuziishi kila siku, vinginevyo tutakuwa na wasomi wengi wa utamaduni wetu halafu wanaoufahamu kwa vitendo huo utamaduni hakuna! Na hoja ya pili nayojiuliza mbona wahindi wao hata wakizaliwa posta au kariakoo wanajua tamaduni zao? Iweje sisi tushindwe? Kumbe hoja sio kukaa mjini wala vijijini basi hoja ni nini hapa?
  Hoja iko wazi nitasema hata kama waheshimiwa watachukia potelea mbali ila ukweli lazima usemwe tu, hoja ni kupotea kwa roho ya uzalendo miongoni mwetu ndiyo sasa hivi uzalendo hakuna kabisa hata mzee Kingunge Ngombare Mwiru analifahamu hili! Hakuna uzalendo hata kidogo, vijana wetu wamekata tamaa hawaoni thamani yao kwenye nchi yao, wanaranda mchana kutwa juani watakuwaje wazalendo wakati hawapendwi? Na hili la uzalendo kupotea halijanyesha kama mvua bali lina mwanzo wake na hapa bila kupindisha maneno ni kulegalega kwa uongozi kwa maana kuwa viongozi wenyewe baadhi yao hawana uzalendo wanahusika kwenye ufisadi, je iwapo viongozi hawana uzalendo wanaoongozwa watautoa wapi? Au wataununua wapi huo uzalendo?
  Viongozi wenyewe hawapendi kuvaa nguo za asili wao ni mabingwa wa kuvaa suti za gharama huku wakizungumza kwa madaha wakichanganya kiingereza na Kiswahili hivi kweli wanataka kukuza utamaduni au wanatutania tu? Hawakumbuki mwenzao Nyerere hadi vitabu vya Kiswahili aliandika, hawakumbuki alivyomlilia Shaaban Robert alipofariki mwaka 1968 waende wakasome utenzi wa mwalimu kwa Shaaban Robert labda wataguswa kwa dhati, Mh Joseph Mbilinyi alikuwa ni mwanamuziki wa kizazi kipya hii inatia hamasa sana hasa anapozungumza swala la kukuza utamaduni kwa sauti ya ukakamavu ikizingatiwa kuwa yeye aliwahi kuwa mwanasanaa lakini pia labda swali moja rahisi hivi haya mapigo ya muziki wa Bongo flava au hayo ya Hiphop aliyokuwa anapiga yeye yana utanzania ndani yake? Ukiacha matumizi ya lugha ya Kiswahili? Ikumbukwe hata Michael Jackson amewahi kuingiza kionjo cha Kiswahili katika kile kibao chake cha "Liberian girl" anaposema….nakupenda pia nakutaka pia wawaaa….. maswali ya msingi waliyopaswa kujibu wabunge hivi kwanini mpaka leo wizara ya utamaduni imeshindwa kusimamia vazi la taifa? Mbona wenzetu Nigeria wameweza? Ilihali wako wengi milioni150 ukilinganisha na sisi wachache tu milioni42?
  Halafu hilo la vyombo vyetu vya habari kutangaza kwa lugha za asili hivi kweli tutaliweza? Kwa maana leo hii tunazungumza Kiswahili kuna redio mbalimbali zina matangazo yanayosikitisha tena ya kubomoa kabisa kama sio yenye chembe ya uchochezi hata mwandishi mkongwe Maggid Mjengwa amewahi kulisema hili kuhusu matangazo ya redio moja ya taasisi ya kidini huko mkoani Morogoro, sasa nadhani unaweza kupata picha hali ya mambo itakavyokuwa kama tutaruhusu vyombo vya habari vitangaze kwa lugha za asili, je serikali ina chombo imara kitakacholisimamia hili la uadilifu kwenye kurusha matangazo mpaka redio za huko mikoani na wilayani? Tusije tukachochea ukabila kwa kigezo cha kukuza utamaduni! Hakika tunacheza na moto! Mungu atuepushie mbali kabisa. Najaribu kujiuliza hivi itakuwaje siku wamiliki wa vyombo vya habari Dar es salaam wakiamua kurusha matangazo kwa lugha zao za asili au magazeti yao yakifanya hivyo? Je wasiaofahamu lugha hizo za asili itakuwaje? Watakosa haki yao ya kupata habari! Au itakuwaje siku kabila Fulani likinogewa na matangazo ya kilugha na kutaka TBC1 irushe maatangazo kwa kilugha? Au gazeti la serikali Daily News na Habari Leo yaandike kwa kilugha, tunacheza na moto!
  Mimi naona tuanze na mambo ya msingi kama kuhimiza vijana wengi wawe waandishi wa vitabu vya fasihi kwa lugha ya Kiswahili ikizingatiwa sasa hakuna kina Shaaban Robert wala Ben Mtobwa, tuwe na vazi la taifa, tuanze kufundisha kwa kiswali kuanzia shule za awali mpaka vyuo vikuu, tuhimize wanamuziki wetu kufanya kazi zenye vionjo vya asili, waheshimiwa wabunge waachane na suti wavae vazi la taifa, tuandike fasihi na tamaduni za kila kabila tena kila lugha ya kila kabila ihifadhiwe kwenye maandishi na tufundishe kwa vijana wetu kwa ustaarabu na uadilifu mkubwa.
  Mwishowe nihitimishe kwa kusema kuwa watanzania tumeishi kwa amani kwa zaidi ya nusu karne sasa , tukaoana watu wa dini tofauti na makabila tofauti , tena tumeishi kwa utangamano mkubwa kwa miaka yote hii, ikumbukwe kuwa kuanza kuongelea makabila yetu kwa sauti zenye ubinafsi ndani yake ni hatua ya kwanza ya maangamiz,i kwa taifa lenye makabila 126 yenye tamaduni tofauti ni hatari kuzungumza mambo ya makabila pasipo ustaarabu wala uadilifu tuwe macho mimi naona wabunge wetu mtuache watanzania tuendelee na utani wetu wakati wa misiba inatutosha na kama mnataka kujenga huo utamaduni kwanza acheni suti rudini kwenye vazi la taifa vinginevyo hatupo tayari kujitegea bomu la Atomic!...Tafakari!

  Nova Kambota mwanaharakati
  Tanzania, East Africa,
  Jumatano 06 April, 2011.
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Nova, ungei edit vizuri post yako ili iweze kusomeka vema.....'matusi' mengine yatatokana tu na hasira za msomaji kuwa kumsumbua kusoma kwa mpangilio wako mbaya wa sentensi na aya (kama zipo)!
   
 3. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I thnk hujackiliza kwa makini na kutafakari hotuba ya mh. sugu. Hebu itafakar kwa kina ndio utabain alichokisema sicho unacho maanisha wewe!
   
 4. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye red: Why are you so defensive?
   
 5. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Una pointi lakini la kusema kwamba tunacheza na moto liache kama lilivyo! Nitokako mimi hata mkuu wa wilaya anaishi katika nyumba iliyojengwa na wajerumani, ofisi yake ilijengwa na wajerumani, makao makuu ya polisi ni msikiti wa waarabu waliojenga wakati wa biashara ya utumwa. Wilaya yenyewe ina ukubwa wa eneo sawa na eneo la nchi ya Rwanda. Lakini ina Banki moja ya NMB! Barabara zote ni vumbi tena zinapitika kwa misimu. Kwa bahati mbaya tumepitiwa na barabara kuu ya kutoka Capetown mpaka Cairo. Ni eneo la wilaya yetu tu katika barabara kuu ambalo bado ni vumbi, yaani kutoka Bondeni hadi kwa Farao. Kwa hoja hii kuna haja gani ya kuendelea kuongea Kiswahili ili tuunganishwe na Watanzania wengine wakati Watanzania wametukataa? Kuna shida gani kama sisi tutajitenga na kuwa na redio zetu na kutangaza kwa lugha yetu? Watanzania mtapata shida gani na nyinyi mmekula kodi zetu tangu uhuru bila hata ya kutujengea ofisi ya mkuu wa Wilaya tu? Hakuna haja. Bora moto uweke na sisi tuendelee kuliko kuwa na utamaduni wa kifisadi na ujinga. Kuwa na utamaduni wa pamoja ni kukuza ufisadi tu!
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  mkuu hata sijakuelewa..
  Wewe utamaduni wako ni upi?
   
 7. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,535
  Likes Received: 2,116
  Trophy Points: 280
  Hoja ya Mh. Mbilinyi kuhusu kuwepo vituo vya redio na televisheni za kilugha nafikiri ameteleza vibaya ila kosa ni kurudia kosa hivyo kwa nguvu zote inabidi tumfahamishe Mh. Mbilinyi madhara ya kuwepo vituo vya habari kama redio/tv za kilugha.

  Jirani zetu Kenya wana utitiri wa redio za kilugha kama KASS, Kameme n.k. Na mtangazaji wa kituo cha KASS FM Joshua Sang naye yupo ktk kundi la 'Ocampo 6 '' ambapo wameitwa The Hague kwa kuchochea machafuko Kenya baada ya uchaguzi.

  Tanzania pia ni nchi ya kiafrika na tusikatae kuwa tunaweza kutumbukia ktk kuigawa nchi kikabila kwa kuruhusu vyombo vya habari kurusha rasmi matangazo yao kwa 'kilugha'.

  Ni kweli inabidi kutunza lugha za kikabila na tamaduni kama unyango, jando au matambiko lakini shughuli hizo tuziachie ktk ngazi ya kifamilia ndani ya maboma yetu au uwa za nyumba zetu.

  Mawimbi ya Radio ni 'public good' hivyo ni vyema kuyatumia kwa lugha ambayo wote tunaifahamu na kwa Tanzania ni Kiswahili. Taasisi nyingi Tanzania zimeshaona umuhimu wa Kiswahili kiasi miaka mingi iliyopita mfano madhehebu mbalimbali ya kidini Tanzania kutumia Kiswahili kama ndiyo lugha rasmi ya shughuli zao na kuendeleza muendelezo wa kuijenga Tanzania kama Taifa moja.

  Sasa hatuhitaji kurudi nyuma kwa kubomoa utaifa wetu kwa kutaka 'kilugha' tunachoongea kipenyezwe na kutumia ktk vituo vya redio kwa ajili ya midahalo ya kisiasa na kijamii, kutumiana salaam au kusomea taarifa za habari n.k.

  Kufanya kosa si kosa ila kurudia kosa ni kosa, hivyo Mh. Mbilinyi suala la kutumia kilugha kurushia matangazo kupitia masafa ya vituo vya redio Redio haikubaliki Tanzania. Ila kilugha ndani ya uwa wa nyumba/maboma yetu inakubalika.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa anaingia chaka baya sana , badala aya kuongeza shule na kuimarisha shule za kata kwenye jimbo lake yeye bado anatetea lugha nza kiutamaduni? hii inamaanisha kuwa watu wengi wa kwenye jimbo lake hawajasoma kwa hiyo hata kiswahili hawaelewi.Mbilinyi kuwa makini sana ndugu yangu natumai chadema hawajakutuma kwa hili
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  Kwa nafasi yake ni waziri kimvuli wa wizara husika, kuhusu redio za kiluga mimi sioni tatizo, kwani tunazo Redio zinazotangaza kiswahili na zinaongoza kwa uchochezi, mfano Redio Imaan ya Morogoro na Redio Uhuru ya CCM hizi ni redio zinazoongoza kwa uchochezi, kwahiyo ndugu mtoa mada, mimi binafsi naona hoja yako haina mashiko.
   
 10. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  good observation..Mbilinyi anataka kuturudisha nyuma
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..kwa wale ambao Kiswahili tumejifunza shuleni, lugha zetu za asili ni muhimu.
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  nxhi nyingi zinatumia lugha zao nigeria kenya,uganda ruanda burundi malawi zambia lesotho swazi southafrica na hakuna uchochezi ,uchochezi unaweza kuja hata kwa kutumia kiswahili iruhusiwe tuu ili lugha zisipotee
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hadi hapo tu ni kwamba ningeomba vyombo vya habari vya kikabila na visione jua ya siku inayofuatia katika taifa hili. Ukabila, udini na ukanda hapana!!!!
   
 14. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  Mkuu nadhani unakosea kidogo. Kama taifa lazima tuangalie vitu kwa 'holistic approach'. Kitu anachokiongea huyu mkuu ni kitu cha muhimu sana. Makabila yetu ndo identity yetu and thats a fact not an opinion. Hata asingesema Mh. Mbilinyi, someone is bound to say it at some point. Kwa hiyo as a nation lazima tujue kwamba matatizo siyo ufisadi na umasikini tuu. Wewe na mimi inawezekana kesho tusiwepo. Lakini Tanzania itakuwepo na watanzania wengine watakuwepo. Hatuna budi kulienzi taifa letu kwa vizazi vijavyo. Sisi kama tumeshindwa kuliendeleza na kujiendeleza haina maana kwamba watanzania watakotufuata miaka mia ijayo watakuwa kama sisi. Na lugha ni kitu muhimu sana ndo maana mashirika kama UNESCO wanajitahidi kuhakikisha kwamba 'endangered languages' zinathaminiwa na kuhakikisha hazifi. Nina imani mchango wa huyu Mh. Umelenga katika muktadha huu.

  Masanja
   
 15. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hii hoja haifai kabisa na italeta vurugu.Hivi kila kabila hapa Tanzania kwa mfano lianzishe radio yake ya kikabila patatosha hapa kweli?Lugha ya kwanza niliyofunzwa na wazee wangu ni Kiswahili na shuleni nilifundishwa Kiswahili pia,lakini nikafanya jitihadi,mpaka nikaijua vizuri lugha yangu ya asili.Lugha za asili haziweki kufa na bado zinatumika sana hasa maeneo ya vijijini.Kama huijui lugha yako ukategemea radio ije ikufunze basi utakuwa na matatizo
   
 16. m

  malimamalima Member

  #16
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kweli sugu umechemka vibaya sana tulikuwa na matumaini makubwa sana na wewe kama waziri kivuli lakini umekosea...vile vile mzee wa mistari haukuwa na mvuto hata kidogo wakati unasoma maoni ya kambi ya upinzani..there was no body language..nilitegemea makubwa sana kutoka kwako lakini badala yake ni kama vile ulikuwa unasoma ulichoandikiwa na kambi yako....jifunze kuongea kwenye jukwaa hasa unapoandaliwa hotuba baba...ila najua wewe ni mzuri sana kwa kuongea maneno yanayotoka mdomoni mwako bila kuandikiwa ndio maana umepata shida sana kusoma maoni ya kambi yako...sugu moto chini...eti wanamwita nani??? :redfaces:
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ENJOY YOUR DEMOCRATIC RIGHTS BY KEEPING YOUR TRIBAL CULTURAL PRIDE & IDENTITY
  AS PRIVATE & LOCAL AS POSSIBLE AS WE AGITATE THE MORE FOR WHAT
  IS NATIONAL, COHESIVE & SELF-SUSTAINING


  I am NOT for this idea of ANYTHING TRIBAL in Tanzania, not even the idea for owning media house fanning and deliberately championing religious propaganda that seeks to tear us apart as a nation.

  Sure, let all religious institutions, keen and capable, own media houses if they may, but never again shall we afford them a rather diluting democratic space or the luxury of peddling hostile and divisive thinking in our midst once the envisaged Katiba Mpya (Si Viraka) comes into force.

  A clean departure from otherwise the known Godly teachings for good relationship between Man, God and fellow Men and the sustained national co-existence agenda MUST be checked before any of our numbers gets an air-ticket to The Hague at some points in time in future.

  Indeed, let's think about the the costs of rolling back the monumental gains that 'we happy-go-lucky' Tanzanians of today landed after Mwlimu Nyerere and many others had painfully invested enomous amouts of resources to make what we see to day a reality.

  No doubt, what we today live in Tanzania, though persistently being deformed by greedy elements in CCM government, never just fell down that way like Mane mane, and the benefits that we've loong been reaping from in there is simply like no that we'd stand to enjoy with what a reverse to the 120 separate tribal unities would bring to this nation.
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..utamaduni haushii kwenye lugha peke yake.

  ..mambo kama mapishi,mavazi,ufundi,sanaa, etc etc ni sehemu ya utamaduni.

  ..kuhusu lugha zetu za asili, binafsi naipenda sana lugha ya kabila langu. ndiyo lugha ya kwanza kuisikia toka kinywani mwa mama yangu mzazi. sioni tatizo kusikikia lugha hiyo ktk radio au kuisoma ktk gazeti.

  ..kukianzishwa radio au magazeti yanayotumia lugha za makabila, bila shaka vyombo hivyo vitakuwa local, sasa tatizo liko wapi?

  ..siamini kama utaifa na uzalendo unaweza kujengwa kwa kukandamiza mila na tamaduni za jamii zetu.

  ..kuzienzi lugha zetu za makabila haimaanishi kwamba tunakipuuza au kukipunguzia nguvu Kiswahili.
   
 19. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #19
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hapana, haliwezi kuwa bomu. Ila kama hatukujirudi mapema tutaftka pahala tukajikuta hakuna pa kwenda. Naafiki kiswahili ndiyo ya taifa hakuna ubishi. Lugha na tamaduni za makabila yetu ndiyo zinatakiwa kukuzwa tena kwa bidii sana. Hapa ndiyo malezi mazuri ya kabila zetu yanakubalika katika jamii yetu ya watanzania! Hofu ya nini? Tuliteleza hapo nyuma sasa umuhimu wake unaonekana wazi kabisa tujirudi! Watu tumeacha mila zetu tukawa tuppo tupo tu tumewafunza watoto wetu kiswahili na tukanda mbele zaidi tukawfunza kifaransa nakadhalika. Sasa wanauliza sasa tamaduni yetu ya tulikotoka vipi mzee? Hatuna jibu na hatukuona umuhimu wake! Hivi mpaka tuambiwe na wageni ndiyo tuzinduke? Tuanze kuzienzi lugha za makabila yetu!
   
 20. C

  Chal Senior Member

  #20
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naamini kabisa ipo haja ya kulinda utamaduni wetu hasa katika kipindi hiki cha uvamizi wa tamaduni za kigeni. Ila kutumia lugha za asili kama nyenzo ya kulinda utamaduni yaweya pia kuwa nyenzo ya kutugawa watanyania .
   
Loading...