Wabunge hawa wasipoteze muda kugombea tena!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,409
AINA YA WABUNGE AMBAO SI VYEMA WAKAPOTEZA FEDHA KUGOMBEA TENA..

Ni ukweli usiopingika kuwa Mbunge ana kazi kubwa 3 ( Kutunga sheria, kusimamia Serikali na kuwakilisha Jimbo) na pia anawajibika kwenye mambo yake binafsi, Chama chake cha siasa, Serikalini na kwa wapiga kura wake ( Jimbo)..

Lakini kama ulikua miongoni mwa wabunge waiofanya maujanja hayo hapo chini, aisee wajiandae vizuri mno maana khaa....

1. Uliishi nje ya Jimbo
haswa Dar. Aidha huna makazi ya kueleweka jimboni au hutumii ofisi ya mbunge jimboni. Unakuja "ziara" jimboni kama mtalii.

2. Uliongelea zao lisilolimwa jimboni mwako. Mfano jimboni wanalima michikichi wewe ukaongelea Korosho. Nchi yetu kilimo ndio mwajiri mkuu. Usipoongelea kilimo cha jimboni kwako unakuwa umewaathiri wapiga kura wengi mno jimboni mwako.

3. Ulikagua miradi nje ya jimbo badala ya jimboni mwako. Mfano ulikagua masoko ya mjini Dar ukaacha kukagua masoko jimboni mwako. Ukadhani kwa kukaguwa masoko ya Dar jimboni watakuelewa.

4. Toka uchaguliwe hujuwahi kufanya ziara jimboni hadi 2020 ndio ukajifanya unawatembelea kujua shida zao. Wapiga kura hawajui toka walipokuchagua umerefuka, umenenepa au umekonda. Wanakuona Twitter na YouTube kana kwamba wewe unaishi Ubeljiji.

5. Badala ya kuwasilisha mahitaji ya wanajimbo ulipoteza muda kudai au kuongelea katiba, tume, dikteta, takwimu za Corona, n.k.

6. Badala ya kufanya ziara jimboni ulijigharamia kwenda nje kutukana nchi, kudai misaada izuiwe, watoto wapate mimba, n.k. aidha uliona ni kipaumbele kuzuru Nairobi kumtembelea mgonjwa ukasahau wagonjwa walioko jimboni mwako.

7. Bungeni hukuwahi kutoa hoja yenye maslahi ya Jimbo badala yake ulishiriki kutoroka vikao vya bunge, kutukana na utovu hadi ukafukuzwa, n.k. Yaani wanajimbo hawakunufaika na uwepo wako bungeni.

8. Ulitumia muda mrefu wa ubunge wako vituo vya polisi, mahakamani au jela badala ya jimboni. Tena kwa kesi zisizo na maslahi kwa jimbo.

9. Ulitumia muda mwingi kupigania maslahi ya Chama au kiongozi wa chama badala ya maslahi ya waliokuchagua kuwa mbunge.

10. Ulipinga miradi au juhudi ambazo wapiga kura walikuwa na maslahi nazo. Mfano ulipinga ufufuaji shirika la reli ambalo wapiga kura wananufaika.

11. Ulishiriki mambo ya kijinga. Kwa mfano ulishiriki kufanya vurugu ambazo hakukuwa na maslahi yoyote ya wana jimbo.

12. Ulitoa kipaumbele kwa hoja ambazo hukutumwa na wana Jimbo. Mfano ulitumia nguvu na muda mwingi kudai Bunge live kana kwamba ndio shida kuu ya wanajimbo.

13. Ulisahau ubunge unatokana na jimbo wewe ukajigeuza kuwa mbunge wa Taifa. Unadaka kila hoja hata isiyohusu jimbo lako. Unaongelea majimbo yote!

Haya ni baadhi ya matendo ambayo kama ulishiriki Bora ukipata mafao kawekeze kwenye biashara kuliko kugombea tena. Utajuta!

From KADA WA CCM, je unafikiri hizi sifa ni za wabunge gani wanalengwa?
 
Umesahau moja mkuu....Kama alikuwa anapiga kofi meza mwanzo wa bunge mpaka hivi linavunjwa kusifia kila kitu hata kama hakina maslahi kwa nchi na jimbo lake. Kiufupi ni wale team praise.
 
Back
Top Bottom