Wabunge hawa wanaongoza kukaa kimya bungeni tangu walipochaguliwa 2010,ona listi hii

Wana JF heshima,
Nimejaribu kupitia wavuti ya bunge letu kutaka kujua mambo kadhaa yanayoendelea bungeni.Lakini nikakutana na profile ya wabunge ambao tangu wachaguliwe bungeni hawajawahi kuuliza swali,wala hata swali la nyongeza na pia hata kutoa michango.Baadhi yao katika hao wameishia kutoa michango kidogo tu.

Nimeamua kuwaletea wabunge hawa muone wenyewe. Katika orodha hii nimewa exclude mawaziri ambao wengi wao na niseme karibia wote hawajachangia.

Kama unayemwona kwenye listi ni mbunge wako una maoni gani kwake?

Wabunge wanaoongoza kukaa kimya bungeni toka 2010 walipochaguliwa
NaJina la MbungeChamaMaswali aliyoulizaNyongeza ya MaswaliMichango aliyotoa
1ABEID ALI BAHATICCM005
2ABDALLAH MARGARETH ANNACCM008
3AYOUB HASHIM JAKUCCM110
4CHAMBIRI WEREMA KISYERICCM004
5HAMAD OTHMAN ASSACUF007
6HASSAN BUKHELI SHAWANACCM003
7ISHENGOMA GABRIEL CHRISTINECCM008
8KAPUYA ATHUMAN JUMACCM001
9KHAMIS ALI KHERICCM000
10KHATIB SEIF MUHAMMADCCM000
11KOMU MAULID VALERIANACHADEMA001
12EDWARD NGOYAI LOWASSACCM001
13SHIBUDA JOHN MAGALECHADEMA008
14ZAKIA MEGHJICCM005
15MUSSA HASSAN MUSSACCM004
16ABDULLA JUMA ABDULLACCM004
17SAID SULEMAN SAIDCUF004
18SAID KASSIM MWANAKHAMISCCM000
19
20
SEIF IDDI ALI
LAMECK AYIRO
CCM
CCM
0
1
0
0
0
2



Asanteni wakuu
Mbona kama wote (except watatu) ni waislam?ama ni majina tu?kuwa makini wasikuite mdini,cha muhimu kuwe na ukweli kwenye data hizi...
 
Mleta hoja unaongeza majina?Maana nimeona umeongezea hapo wakristo wawili,niliedit mara ya kwanza ulipoongeza mmoja,sasa umeongeza tena na mimi itabidi niseme wote ni waislam kasoro wanne!
Sikusema ukatafute majina ya wakristo uongezee,cha muhimu ni validity ya data zako_Otherwise it is very interesting...
 
Hivi mkuu Narubongo yule mbunge wa Rorya Mh. Ayiro amewahi kunena ama kuandika chochote akiwa ndani ya Bunge lao Tukufu?

Hili siyo Bunge Tukufu, ni Bunge Tukutu. Kitu kitukufu hakina tabia kama za wabunge wanao zomea na wenye kuwa na ushabiki wa kijinga kama wanavyofanya magamba. Kitu kitukufu hakiwezi kuwa na wazinzi na wanao jisifia wanajua kutukana, wauawaji kwa wanao wapinga kisiasa!
 
Umekosea mkuu, Tenasana; Kiwia Higness anauliza maswali kila leo na kuchangia, pialisu naleticia inaonekanahuangalii sana bunge hivyo unatoa taarifa ambazo hazina utafiti.

Pia elewa kuchangia unaweza omba ukakataliwa juu ya muda au wanaangalia ratio ya vyama, jinsia, na wale wenye taaluma na kufanyakazi eneo hilo. Piamuda wa bunge ni mdogo sana hivyo wengi huchangia kimaandishi zaidi kuliko kuongea.

Sio sifa kuchangia inategemea taifa linapata nini hapo.

Hu ni upuuzi kulinganisha kwa style hii.

Wakina dewji, Rostam na wale CCM damu sawa ndio uwaweke hapa maana wataconflict inerest zao wakichangia.
20 Mwanamrisho Abama

21 Raya Ibrahim

22 Naomi Kaihula

23 Christina Lissu

24 Leticia Mageni

25 Conjesta Leos

26 Rose Kamili

27 Highness Kiwia

28 Israel Natse

29 Mustafa Boay

30 Prof Kulikoyela
 
jf now dayz kama magazeti ya udaku yaani aakh? Hivi mbunge akiwa vuvuzela bungeni halafu si mfuatiliaji wa mambo ya kimaendeleo jimboni kwake anafaida gani? Halafu mbona wa dini 'a' tu? Wale wengine vipi? Ni kweli hawapo wenye sifa hizo kweli? Mbona siku hizi kushambuliana kwa sampuli hii {dini} kumeshika kasi sana? Msingi wake ni upi?
watanzania;kumbukeni taifa hili halikuasisiwa ktk misingi ya ubaguzi wa kidini, ukabila wa umaeneo. Sisi sote ni ndugu!
 
mizambwa inauma sana hizo picha

kumbuka tuna miaka 50 baada ya uhuru


Duble Chris; Yaani wakati mijadala mbalimbali inaendelea Wabunge wetu waheshimiwa tuliowachagua kwa kura nyingi na nderemo na vifijo; wao wanasinzia Bungeni.

Je, hiyo michango au maswali watauliza saa ngapi ikiwa hawajui kinachoendelea. Na Mwaka wa uchaguzi ukifika sisi wananchi tunaolalamika bado tutawachagua hawa hawa.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Last edited by a moderator:
Duble Chris; Yaani wakati mijadala mbalimbali inaendelea Wabunge wetu waheshimiwa tuliowachagua kwa kura nyingi na nderemo na vifijo; wao wanasinzia Bungeni.

Je, hiyo michango au maswali watauliza saa ngapi ikiwa hawajui kinachoendelea. Na Mwaka wa uchaguzi ukifika sisi wananchi tunaolalamika bado tutawachagua hawa hawa.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
we have no way out !!

linalo nisikitisha siku zote ni kuunga mkono hoja kwa 100% ili hali halisi wanaorodhesha matatizo lukuki sasa najiuliza hizo 100% za nini ikiwa hoja inakuwa na mapungufu mengi tu

kwa nini wasiunge kwa 59%, 81%, 44% etc na mtu akiunga kwa 100% maana yake efficiency ni 100% there is no energy lost kitu ambacho si rahisi hata kidogo

lakini yote haya sisi tumeyataka ndiyo maana tunasomeshea watoto wetu kwenye vijumba vya nyasi karne ya 21

PICHA HIZO ZIMENITIA UCHUNGU SANA BORA KAMA SI ZA TANZANIA
 
mimi nilikuwa nimeshasahau kama juma kapuya ni mbunge.kweli magamba wana kila aina ya vihoja
 
ongeza nyingine inaitwa Dr.Festus Limbu,hii jamaa kimya sana mjengoni,jimboni nako pia kilaza,imejenga kwao tu kidogo,haitembelei wapiga kura wake mpaka wakati wa kampeni,inankera sana mimi nnapoiona kwenye screen imebunda kama levi wakati naona hali ya magu mbaya sana..nikomee hapo,ila kama ipo humu ijistukie,doctor mzima huna cha kuongea kuhusu jimbo lako!!!
 
Getrude Lwakatare amewahi kuchangia kitu chochote?

i just wanted to mention her. Huyu mama tangu ateuliwe na Rais na mpaka aliponogewa na kuchukua viti maalum mwenzenu sijamsikia akinyanyua mdomo bungeni zaidi ya kupiga kura ya "Ndiyooooooooo".
 
i just wanted to mention her. Huyu mama tangu ateuliwe na Rais na mpaka aliponogewa na kuchukua viti maalum mwenzenu sijamsikia akinyanyua mdomo bungeni zaidi ya kupiga kura ya "Ndiyooooooooo".
hapa unamuongezra hasira za kutaka JF ifutwe mapema zaidi ndiyo ulio kuwa mchango ake kwenye bunge lililo pita
 
Back
Top Bottom