Wabunge hawa wa CHADEMA ni mizigo isiyobebeka

Kilaza

JF-Expert Member
Feb 28, 2013
3,324
1,377
wakuu

Salaam

Kwanza nianze kwa kusema mimi ni mwanachama hai wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA tena inaweza kuwa nimejiunga siku nyingi kuliko wewe lakini ngoja lro niseme ukweli mtupu.

Kumekuwa na hili neno "mzigo" linalotumika sana kwenye siasa na niukweli usiopingika kuwa viongozi wa chama cha mapinduzi wengi (almost all) ni mizigo tena mizigo mikubwa sana lakini hata sisi wapinzani tuna mizigo yetu.

kwa upande wangu mimi na kwa chama changu cha CHADEMA mizigo hiyo ni

1) John Shibuda
Huyu kila mtu anajua alivyo tatizo ndani ya chama chetu na sijui ni kwanini tulikubali kupokea huu mzigo uliowashinda CCM .

Kitu anachokiweza ni mipasho na misemo yake bungeni hana la ziada
fani aliyobobea ni kuhama vyama na kuanzisha malumbano yasiyo na tija ndani ya vyama

2) Mh. prof. Kahigi
huyu mzee nadhani alishinda ubunge kwasababu ya tittle yake ya "uprof"ndicho kigezo alichotumia kuwahadaa wananchi wakampa ubunge lakini kujenga hoja hawezi kabisa nilitegemea angeleta michango muhimu kwenye kambi ya upinzani kama msomi lakini wapi.

3)Mh.machemli
huyu mimi sijawai hata kumuona akiongea bungeni japo mimi ni mfuatiliaji mzuri wa vikao vya bunge kwanza sidhani hata bungeni kama anaendaga muulize mwanachama yeyote wa CHADEMA kama alishawai kusikia kama kuna mtu anaitwa machemli wewe mwanachama wa CHADEMA unamjua huyu mtu japo kwa sura tu?

4)Mh. Opulukwa
Huu tena ni mzigo mwingine usiobebeka hata sihitaji kufafanua kila mtu analielewa hili.

5)mh. Kiwia Highness
Huyu labda kwa sababu ya ugonjwa wake kila mara analazwa nje ya nchi kidogo siwezi nikamuongelea lakini kama tunataka hili jimbo liendelee kubaki kwetu tumtute kamanda mwingine tusonge mbele

6) Mh. Selasini
Kiukweli huyu mzee hawezi chochote sio jimboni bungeni wala kwenye chama ni mzigo mkubwa tusipoangalia hili jimbo tutalikosa.

7) mustapha akonaay
CHADEMA bado inaushawishi kwenye jimbo la mbulu lakini tusipokuwa makini tukausimamisha mzigo huu jimbo tutalipoteza

8) Wabunge wote wa viti maalum

Kiukweli sijaona mbunge yeyote wa viti maalum chadema ambaye sio mzigo wote ni "empty set". Nilitegemea kuona wabunge wa viti maalum wenye kaliba ya Mdee wa bunge la tisa akiwa mbunge wa viti maalum lakini wapi hawa wote ni mizigo mitupu.

Hakuna kazi wanayofanya sio ndani ya bunge wala nje ya bunge wala kazi za chama. Nijuavyo mimi ubunge wa viti maalum ni kwaajili ya kuwajengea uwezo na platform ili wawe wabunge wa majimbo kabisa (mfano Mdee) lakini hawa hawana uelekeo wowote.

Embu jiulize CHADEMA ina wabunge zaidi ya ishirini wa viti maalum wewe unawajua wangapi ?wanafika watano ...!! yupi mwenye uwezo wa kuwa mbunge wa jimbo!

Nakishauri chama changu kuwapiga chini hii "MIZIGO" yote uchaguzi ujao.

NB: Nitajitolea fedha za fomu na kampeni kwa kijana yoyote atakayeonesha nia kwenye majimbo tajwa hapo juu.

kilaza
 
Ni ukweli kabisa hawa wabunge ni mzigo chadema tueni hii mizigo kama huyo kasulumbai sijui ni mmbunge wa wapi?
 
Muda umeisha,mwakani uchaguzi, hata kama wabadilike saivi, wamechelewa

Viti maalum si wote mizigo Kuna dada kupitia mkoa wa Morogoro aise yule ni makini sana na mwakani anagombea jimbo la Kilombero kwa Celina Kombani. Pia anacheo kwenye chama na alikuwa meneja campain wa chadema 2010
 
.... Hata Mbowe Watu Wa Hai Wanalalamika Sana.!

mbowe siwezi kumlaumu ...anamajukumu mengi sana hata hivyo bungeni tunaona impact yake kubwa sana kama kiongozi wa upinzani vilevile kazi anayoifanya ya kujenga chama ni kubwa sana.....licha ya yote hayo jimboni anajitahidi kutimiza majukumu yake
 
Kweli wewe ni kilaza!
Shibuda sawa , ila kuona wabunge wote wa viti maalumu ni mizigo inaonesha hujawahi kuhudhuria shughuli za field za chadema km vile kampeni za chaguzi ndogo n.k.
 
Chadema wote mizigo tu hakuna mwenye unafuu hata mmoja wote mbugila.
 
wewe labda Shibuda wengine wote ni safi sana,

Pia usitake Mungu awe kama Yesu au Yesu awe kama Mungu utakuwa unakosea sana, hata darasani huwezi kuwa kama X na X hawezi kuwa kama wewe.

Hata bungeni huwezi kumfanya Mh. Ridhiwani awe kama Lusinde. pls. hope nimeeleweka vyema.
 
Mkuu nimekupata na umesema ukweli ingawa kuna wabunge wachache wa viti maalum wamejaribu. kuna MHS Mbunge kutoka Mkoa wa Kagera anajitahidi na anapambana. Ingawa anatakiwa kuongeza kasi lkn siyo mzigo!
Hapa ninapenda kusema hivi: CDM inahitaji wabunge ambao ni results oriented nikiwa na maana kuwa Mbunge mmoja wa CDM inabidi awe bora mala dufu ya mbunge wa CCM ili kubalance equation! CDM ina wabunge wachache ukilinganisha na CCM, hivyo kutoka na uchache wake ni lazima mbunge mmoja wa CDM afanye kazi zaidi sana na cha muhimu ni matokeo ndo hapo chama kinaweza kuiga hatua kwa kasi. Ninajua wakati mwingine ni vigumu kupata watu wa namna hii ila tafdhari kwa wale ambao wameonyesha uzembe au hawana uwezo itabidi CDM ikae nao na bila aibu kuwambia sasa basi itabidi wapumzike. Wataendelea kuwa active ktk shughuli zingine. Hii ni muhimu sana kabisa. Sasa Prof Kahigi, amekuwa anafanya nini? Yeye ni Prof wa nini? Tunataka Mbunge wa kuhamasisha vijana na akubaliwe. Mfano ni huyu Mdee, she is one to be an axample. She is not there to show how cute is ila ni kupambana. CDM inataka wabunge ambao wata invest for the future!
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom