Wabunge hawa wa CHADEMA ni janga kubwa

John Mnyika Kamanda, heshima yako kwanza, hii hoja ni nyepesi sana kwako, hukupaswa kumjibu huyu mfa maji, ulitakiwa kujua kuwa jf is the forums of "GREAT THINKERS " and "GREAT SINKERS"
 
Last edited by a moderator:
Kamanda Mnyika wala usipoteze muda kumjibu huyo jamaa, uwezo wake wa akili ni mdogo sana, anatumwa kuandika chochote, wamejaa hapa Lumumba(ofisi ya CCM) kuja kuchukua posho kwa kila topic au post watakayo andika humu JF.
Ni kweli mnyika kaza buti pesa za kinana za pembe za ndovu zinafanya kazi
 
We jamaa wa ajabu sana, yaani tatizo la maji la toka uhuru unataka litatuliwe kwa miaka miwili tu?

Waliopita kutokea CCM walileta nini hapo ubungo? Wewe unatokea jimbo gani kwanza?
 
attachment.php


CCM Great Thinker maji taka
 
ki ukweli mimi si mkazi wa maeneo ya wabunge uliowataja mimi niko
ubungo, tulimchagua Mnyika tukitegemea mabadiliko ya kweli, lakini anachofanya ni kumtusi Rais bungeni, je sisi tulimtuma hayo? Anafikiri wabunge wengine hawajui kutumia maneno ya kebehi dhidi ya Rais? Anatudhalirisha
Hebu tupe hayo matusi aliyomtusi Rais
 
Kamanda, heshima yako
kwanza, hii hoja ni nyepesi sana kwako, hukupaswa kumjibu huyu mfa maji,
ulitakiwa kujua kuwa jf is the forums of "GREAT THINKERS " and "GREAT
SINKERS"

kuwa mkweli Mnyika ana kipi cha kujisifia jimboni, ana fan base kubwa anashindwa hata kuhamasisha usafi wa Soko la Urafiki? Tunaitaji visionary leaders siyo wapiga domo!
 
Naunga mkono hoja huku ubungo hali ni mbaya kazi yao ni kupiga domo matendo hakuna
 
Wewe ndio janga tena huna sifa ya kuitwa mtanzania weye,fisadi uliyetumwa na magamba yenu kuandika utumbo JF.
 
nnachokiona sasa hivi, watu wanajaribu kuanzisha vitu vya kijinga jinga visivyo na mantiki wala msingi wowote ili kutoa au kupoteza focus ya watu kufanya mambo ya msingi. muda anaotumia Mnyika au kiongozi mwingi ne kujibu huu upuuzi angeutumia kwa mambo mengine ya msingi. Nadhani tungejikita zaidi kwenye kuangalia namna tunavyoweza kukabiliana na changamoto zinazolikabili taifa letu na kukwamisha maendeleo.

Kuna vitu visipopatiwa ufumbuzi madhubuti, hata chama gani kitawale (including cdm), hapatakua na mabadiliko tunayoyatarajia.

Miongoni wa hayo ni hili hapa..

".... these huge NGOs, coming to Africa in the name of solving poverty. And what ends up happening is that all those multinational corporations that are in the aid business, in essence they are in the poverty business. And like in any other business, if poverty is your business, more poverty is more business…. The World Bank recently made a study where they said something like sixty percent of all the aid money stays in the donor country, because it goes to all of these consultants and people and this and that. Sixty percent of the entire money stays in the country that pledged it in the first place. That is not aid! That is the business of poverty."

Tusihuruhu hoja zisizo na msingi na ushabiki usio na tija kuchukua muda mwingi wa kupata practical solutions za matatizo yetu..

Mimi sio mwana chama wa chama chochote cha siasa, ila nna KADI YA KUPIGIA KURA.
 
Mkuu umewasahau John Mnyika, Wenje, Kiwia. Hawa siku zao zinahesabika.
 
Nakushukuru sana kwa maoni yako, nakushauri uanze kwanza kukusanya saini za watanzania siku ya uhuru tarehe 9 Disemba 2012 tunaposheherekea miaka 51 ya Uhuru bila ya maji katika majimbo mbalimbali nchini (Ubungo likiwa na afadhali kuliko majimbo mengi nchini na hata baadhi ya majimbo la Dar es salaam).

Kuhusu kazi nilizofanya katika kipindi cha miaka miwili niliyokuwa mbunge unaweza kuzisoma tu hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...su-kazi-za-maendeleo-jimboni-ubungo-amua.html , lakini kama ni mwananchi wa Ubungo ulipaswa kuwepo wakati nafanya ziara jimboni na DAWASA, DAWASCO kushughulikia matatizo ya maji na hatimaye ziara na Waziri wa Maji Prof. Maghembe kuzindua miradi ya maji. Nikodekeze tu kwamba pamoja na kazi hizo tulizofanikisha bado naendelea kuwatumikia, juzi nimewasilisha hoja binafsi ya maji Dar es salaam kwa halmshauri ya jiji, nasubiri mkutano wa baraza la madiwani ijadiliwe kuongeza msukumo wa hatua za haraka. Kumbuka, mkutano uliopita wa bunge niliwasilisha lakini ratiba ilibana haikujadiliwa, fuatilia mkutano ujao wa Bunge mwezi Februari utaona kitakachotokea.

Umeandika maneno yasiyokuwa ya ukweli kwamba toka nichaguliwe kazi yangu imekuwa kwenda Ulaya na Marekani kufungua matawi ya CHADEMA; kwa taarifa yako sijawahi kwenda kufungua tawi lolote Ulaya na Marekani miaka miwili ambayo nimekuwa mbunge (Lakini nitakwenda). Kwa sasa nikifanya ziara za kichama ni jimboni Ubungo, unaweza kufuatilia hapa ya karibuni: JOHN MNYIKA: Ziara ndani ya Jimbo iliyofanyika Desemba 1, 2012: Kimara na Saranga au vijijini katika mikoa mbalimbali nchini. Kama wabunge uliotutaja ni janga la taifa, nitajie wabunge ambao sio janga la taifa.

JJ
achana na huyo mpuuzi mhe mbunge wangu, nakushukuru sana na mimi kwangu Kimara Butcher ninapata maji japo mara 2 kwa week na week nyingine zaidi, umetusaidia sana mheshimiwa,kwa sasa ile biashara ya maji kwenye magari mtaani kwetu imeisha. Hongera Kijana mwezangu big up nakuadmire sana
 
ukiona mtu anawataja wabunge wote wa cdm kuwa mabomu halafu hamtaji shibuda basi ujue yupo kwenye payroll ya nape iitwayo majitaka
 
Mkuu umewasahau John Mnyika, Wenje, Kiwia. Hawa siku zao zinahesabika.

tutajie wa ccm walichofanya hadi wabaki kwenye majimbo yao...unaona utapata attention kwa kuwatajataja wabunge wa cdm
 
I am sure 100% UMETUMMWA WEWE na wala hauko jimbo la ubunge.
Hizo posho mnazopewa na ccm ili kuja kuchafua watu mtandaoni zitaendelea kukuangamiza wewe na vizazi vyako na hii serikali ya majambazi wa rasilimali za umma.ACHA UTUMWA HUO, JIKOMBOE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom