Wabunge hawa wa CHADEMA ni janga kubwa

Nov 28, 2012
28
0


Wabunge hawa wa Chadema ni Janga La Taifa, tuhakikishe mwaka 2015 hawarudi bungeni kutuwakilisha because wame prove failure katika majimbo yao.....ni jambo la kusikiktisha sana kuona John Mnyika Mbunge wa Ubungo anaemaliza muda wake amefeli kabisa ku address na ku solve tatizo la Maji katika jimbo lake....yaani inasikitisha sana katika dunia hii kuona mbunge ambaye anashindwa kujua matatizo ya jimbo lake lakini yuko mstari wa mbele katika kuhakikisha anapangwa na Chama katika safari za kufungua matawi ya Chadema huko Marekani na Ulaya.....Sasa John Myika Hizo Safar Za Kufungua Matawi zina Tija Gani kwa Wakazi Wa Ubungo...huo ni upuuzi na udhaifu wa hali juu....na kwa taarifa yako mwaka 2015 haurudi bungune coz ww ni janga kwa sisi wakazi wa Ubungo....ume prove failure na kuanzia tarehe 1.1.2013 nitaanzisha petition ya kukusanya sahihi za wakazi wa Ubungo ya kukosa imani na wewe.......nawaasa wananchi wenzangu tuamke hawa CHADEMA hawana lolote ni wanafiki wakubwa na wanatutumia kama ngazi ya kujinufaisha wao wenyewe na familia zao...


Wabunge wafuatao nao ni Janga la Taifa

1. Halima Mdee

2.Peter Msigwa

3.Joseph Mbilinyi

4.David Silinde

5.Freeman Mbowe


NATABIRI KIFO CHA CHADEMA KABLA YA MWAKA 2015......
 

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,778
2,000
Tafadhali,,naomba tusome tuh na tumwache ivo ivo,,

ugonjwa anaougua huyu hauna tiba wala kinga,nasisitiza aachwe kama alivo,hakuna wa kuweza kumponya zaid ya maulana mwenyewe..


Hii chini ni dedication yake..,,

"kiii chaa kimempandeje jeelii,,baaada ya kuvuta mine,,nelii,,watu wanasema karogwa na jiranii,,kumbe mibangi imempanda kichwanii,,kichaa kimempandajee,,jeliii,,,""
 

UPIU

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
602
0
Bwana Kimbunga Siyo kweli mkuu, wabunge wa CDM hawatofautiani na wa CCM, wote ni walewale tusichague Chama bali mtu.
 
Last edited by a moderator:

DARKMAN

Senior Member
Aug 23, 2012
122
0
kwani mnyika ndie anayekusanya kodi? waulize wanaokusanya kodi kwanini ubungo maji hamna? mambo mengine ni bora uyaongee hapa JF kwa ID za kujificha ila ukithubutu kuongea mtaani huku kwetu ubungo utapigwa mawe,
yaani badala ya kuwauliza wabunge wako akina keenja waliokuwa wanakusanya kodi kwa miaka 50 bila kuleta maji ubungo uje umuulize mnyika
 

marembo

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
202
170
Yeye ndiya anayekufa temna hafiki 2015. Huyu mlevi tu wa siasa na hajui kuwa siku zake yeye na mafisadi wao ziko ukingoni. Mtu mzima na akili zake ameaga watoto anaenda kazini na kujikita JF na kutoa utumbo na ***** huu. Kwa taarifa yake wabunge hawa wanarudi na wengine wengi kuingia kuziba nafasi za magamba ambao wamekaa kubadilisha sura za viongozi ambao hawaleti tija yoyote ktk maisha ya mtanzania. Uwezo wa kufikiri wa bw Kimbunga kama walivyo wengi wa magamba ni matokeo ya kuchezea elimu kwani wengi hata kama wamefika sekondari ni hizi za kata zisizokuwa na walimu. Pole sana wananchi wa leo hawataki propaganda
 

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,807
2,000
CDM ina wabunge wawili tuu hapa Dar ambao ni majembe! utakuwa umevurugwa uliuchotakiwa kusema ni kwamba wabunge wa CCM dar na TZ kwa ujumla ni janga la kitaifa.Meya wa Dar alisema kuna wabunge wa CCM wanatumia makalio kufikilia.
 

HUGO CHAVES

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
2,045
1,500
umetumwa au unatumika kwa manufaa ya aliyekutuma .kukaa kimya ni busara pia .hawa watu uliotaja hapo juu kazi zao na mchango wao kwa jamii unaonekana tofauti na wabunge wengine wanasinzia bungeni wakiamka wanapiga makofi ndio oooo.muulize hoja gani imesomwa anasema ndio.............hajui ila anapitisha siku posho yake apate na aonekane alikuwepo pale .
 

Mpitagwa

JF-Expert Member
Feb 10, 2012
2,340
2,000
Kama namuona alivyokuwa ametoa mishipa wakati wa kuandika huu uzi na anaonekana kuwa uwezo wake wa kufikiri umeishia hapo. Tumpo pole na kumuomba aanze kusoma japo majukumu ya mbunge ni yapi na baadaye aje asome majukumu ya mbunge wa upinzani ni yapi. Halafu anajifanya ametembelea majimbo yote 5 wakati aliyoyasema ni hisia zake za jimbo moja tu la ubungo. Hata jimbo la kawe hajaliongelea, sembuse Mbozi Mashariki na Hai. Jenga tabia ya kusoma ndoo tiba b
 

Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,520
1,225
Nakusamehe kwa kuandika jambo ambalo wala moyo wako hauamini kuwa ni kweli,siku nyingine usipende kufurahisha watu wanaokutuma bila kutafakari utakuja umia.
 

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
225
Bwana Kimbunga Nakushukuru sana kwa maoni yako, nakushauri uanze kwanza kukusanya saini za watanzania siku ya uhuru tarehe 9 Disemba 2012 tunaposheherekea miaka 51 ya Uhuru bila ya maji katika majimbo mbalimbali nchini (Ubungo likiwa na afadhali kuliko majimbo mengi nchini na hata baadhi ya majimbo la Dar es salaam).

Kuhusu kazi nilizofanya katika kipindi cha miaka miwili niliyokuwa mbunge unaweza kuzisoma tu hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...su-kazi-za-maendeleo-jimboni-ubungo-amua.html , lakini kama ni mwananchi wa Ubungo ulipaswa kuwepo wakati nafanya ziara jimboni na DAWASA, DAWASCO kushughulikia matatizo ya maji na hatimaye ziara na Waziri wa Maji Prof. Maghembe kuzindua miradi ya maji. Nikodekeze tu kwamba pamoja na kazi hizo tulizofanikisha bado naendelea kuwatumikia, juzi nimewasilisha hoja binafsi ya maji Dar es salaam kwa halmshauri ya jiji, nasubiri mkutano wa baraza la madiwani ijadiliwe kuongeza msukumo wa hatua za haraka. Kumbuka, mkutano uliopita wa bunge niliwasilisha lakini ratiba ilibana haikujadiliwa, fuatilia mkutano ujao wa Bunge mwezi Februari utaona kitakachotokea.

Umeandika maneno yasiyokuwa ya ukweli kwamba toka nichaguliwe kazi yangu imekuwa kwenda Ulaya na Marekani kufungua matawi ya CHADEMA; kwa taarifa yako sijawahi kwenda kufungua tawi lolote Ulaya na Marekani miaka miwili ambayo nimekuwa mbunge (Lakini nitakwenda). Kwa sasa nikifanya ziara za kichama ni jimboni Ubungo, unaweza kufuatilia hapa ya karibuni: JOHN MNYIKA: Ziara ndani ya Jimbo iliyofanyika Desemba 1, 2012: Kimara na Saranga au vijijini katika mikoa mbalimbali nchini. Kama wabunge uliotutaja ni janga la taifa, nitajie wabunge ambao sio janga la taifa.

JJ
 
Last edited by a moderator:

sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
2,000
Tumwacheniiii Big Show katoa angalizo..
Nadhan tuilaumu serikali watu kama hawa ni zao la ARV fake!
 

JGK

New Member
Dec 17, 2011
4
20
Kijana naona unaanzisha thread kwa manufaa binafsi na unajikuta unadhalilisha uwezo wa upeo wako. Hao unao ona wanafaa wameshindwa kuli address hilo tatizo toka tupate uhuru mpaka jimbo linachukuliwa na Mnyika. Huwezi kusema yeye ka prove failure ndani ya miaka michache tangu aingie madarakani. Mpe nafasi kwani naye ni binadamu si Mungu wa kunena na likatokea.
 

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
0
Kamanda Mnyika wala usipoteze muda kumjibu huyo jamaa, uwezo wake wa akili ni mdogo sana, anatumwa kuandika chochote, wamejaa hapa Lumumba(ofisi ya CCM) kuja kuchukua posho kwa kila topic au post watakayo andika humu JF.
 

tumpale

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
200
0
Du, huyu ndugu ni poyoyo kwelikweli, majukumu ya mbunge sio kuleta maji hayo ni majukumu ya serikali kupitia kodi zetu. kama hujui jambo usiogope kuuliza.hivi myika anaweza kulingana kwa uwezo na prof maji marefu au unatania tu.

chukua maji marefu, azani, zungu, mtemvu, kwambwa, Ghasia, Wassira na wengine kwa pamoja ukichanganya akili na uwezo wao hawamfikii john myika mbunge wa ubungo. hebu kili uwezo wa mnyika na wenzake, ukitaka kuthibitisha kamuulize pinda atakueleza.

lakini kuweka kumbukumbu sahihi katika bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania hakuna mbunge anayeitwa john msigwa
 

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,322
2,000
siyo kweli mkuu, wabunge wa CDM hawatofautiani na wa CCM, wote ni walewale tusichague Chama bali mtu.
wengine uelewa wetu ni mdogo hebu tupe mwanga zaidi, kwa hiyo mkuu unashauri kuchagua watu kama Mtemvu, Zungu na Iddi Azzan hivi?
 

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,285
2,000
Kila siku Mnyika na Mdee kuhusu maji...........hivi hawa wanaoanzisha hizi thread wanataka kutuambia Jimbo la Mtera wapiga kura wana maji kweli? Hata huyo Prof Maghemebe mwenyewe jimbo lake watu wanakunywa na kuoga vumbi na yeye ni waziri wa maji
 

JoyPeace

Member
Oct 18, 2012
66
0
mfu mwingine anayetembea !!!!

Akija Kichaa na kuchukua nguo zako mlangoni ukiwa bafuni! nawe ukamkibiza ukiwa uchi, WEWE ndo Kichaa na yeye ataonekana fit!!:crazy: Nashauri msipoteza kumjibu huyo mtakuwa vichaa pia!!
 

UPIU

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
602
0
[FONT=trebuchet

ms]wengine uelewa wetu ni mdogo hebu tupe mwanga zaidi, kwa hiyo mkuu
unashauri kuchagua watu kama Mtemvu, Zungu na Iddi Azzan
hivi?[/FONT]

ki ukweli mimi si mkazi wa maeneo ya wabunge uliowataja mimi niko
ubungo, tulimchagua Mnyika tukitegemea mabadiliko ya kweli, lakini anachofanya ni kumtusi Rais bungeni, je sisi tulimtuma hayo? Anafikiri wabunge wengine hawajui kutumia maneno ya kebehi dhidi ya Rais? Anatudhalirisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom