Wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya wamefurahi Kanumba kufa?

Lulu inatakiwa aingie jela akakae japo mwaka 1 ili ajue dunia inaendaje, asipopata tabu atajifunzaje?
 
Kanumba alikuwa malaya tu unacheza "maigizo" ya mapenzi na mahusiano halafu akashindwa kuwa "badass" poor him, kisheria lulu anahaki ya kutetewa.Bongo hamna wacheza filamu ,kuna watu "wanaigiza" kuigiza
 
Ninavyofahamu mimi Mh. Halima Mdee ni mwanasheria. Kuhusu sakata la LULU (Elizabeth), pamoja na yote yanayozungumzwa bado anahitaji usimamizi wa kisheria ni haki yake. Tunaamini Mh. Mdee ama Mh. Bulaya hawawezi pindisha sheria kama Lulu atakutwa na kosa la mauaji kwa kukusudia. Pia kama itadhihirika kuwa anaumri wa miaka 17 (ingawa najua alishajitangaza na kusheherekea miaka18), atahitaji usimamizi na ushauri kama mtoto maana anaweza kuathirika vibaya sana na pressure ya jambo hili. Tunaamini akipata usimamizi na usaidizi wa kisheria, na kama atahukumiwa kwa kisa la mauaji, basi itakuwa haki imetendeka. Tusipende kukimbilia kuhukumu, bali nakubaliana bado kunautata mkubwa kwenye tukio hili la kusikitisha ssana.

umefunga mjadala, na tuishie hapa
 
Halima wewe tunakuheshimu sana, achana na hili tukio. Lulu ameharibika siku nyingi sana tena akiwa under 18, picha za uchi kwa mitandao n.k. hamkusema kitu, sasa matokeo ya kuharibika kwake mnataka mseme, acha dada yangu maana inataka kuwa kama mwehu kuongelea athari za kuharibika kwake bila kuongelea kuharibika kwenyewe. Unakumbuka alikana kuwa hana uhusiano na Kanumba, Je imekuwaje tena? ni muongo hivyo kila analosema hatuwezi kuamini kirahisi. Under 18 kapata wapi driving license? ni muongo huyo dada yangu atakuchafua bure. Kituoni aliandikisha ana miaka 18, kwani hajui hata umri wake? mama yake akaleta cheti ana miaka 16 na siku 360 hadi leo hapo tena inaonesha ni muongo.

So please achane naye, ashughulike na waongo waongo wenzake sio wewe.

halima pokea hili.
 
Nimesikitishwa na kauli zilizotolewa na wabunge Halima Mdee (CHADEMA) na Esther Bulaya (CCM) kusema kwamba wanataka KUMNASUA Elizabeth Machael (Lulu) anayetuhumiwa kusababisha kifo cha Kanumba. Kama wabunge walitakiwa kutumia busara kwa kuacha upelelezi huru na kutoingilia uhuru wa Mahakama.

Marehemu alikuwa anambaka LULU, maana ni under 18 huenda ameanza kukabaka na kukafundisha tabia mbaya kakiwa umri wa 15 years!!!!!!
 
Lulu ana haki sawa na mshitakiwa mwingine mwenye kosa kama hilo na ana haki ya kutetewa na wakili au mawakili tusimuhukumu tuache sheria ifuate mkondo wake.
 
Nimesikitishwa na kauli zilizotolewa na wabunge Halima Mdee (CHADEMA) na Esther Bulaya (CCM) kusema kwamba wanataka KUMNASUA Elizabeth Machael (Lulu) anayetuhumiwa kusababisha kifo cha Kanumba. Kama wabunge walitakiwa kutumia busara kwa kuacha upelelezi huru na kutoingilia uhuru wa Mahakama.

waache wamtetee si kosa, bado sheria itafuata mkondo wake.
 
Mkuu Kuna Mashosti huko Mtaani Lulu alikuwa anawakimbiza Kweli kweli sasa wanafunga ili Maskini haka katoko Kasitendewe haki. Lulu alikuwa anawapiga bao katika kuchuna Mabuzi

mkuu hiyo sentesi ya mwisho unamaanisha nini.
 
Nimesikitishwa na kauli zilizotolewa na wabunge Halima Mdee (CHADEMA) na Esther Bulaya (CCM) kusema kwamba wanataka KUMNASUA Elizabeth Machael (Lulu) anayetuhumiwa kusababisha kifo cha Kanumba. Kama wabunge walitakiwa kutumia busara kwa kuacha upelelezi huru na kutoingilia uhuru wa Mahakama.

Jitahidi kulewa japo sheria zinavyofanya kazi . labda ungehoji kwa nini Lulu sio kuwanausa mabnti wengine? Lakini kutuhumiwa tu haina maana niMkosaji nahata kama niMkosaji bado hata wauwaji wana haki ya utetezi.
 
Nimesikitishwa na kauli zilizotolewa na wabunge Halima Mdee (CHADEMA) na Esther Bulaya (CCM) kusema kwamba wanataka KUMNASUA Elizabeth Machael (Lulu) anayetuhumiwa kusababisha kifo cha Kanumba. Kama wabunge walitakiwa kutumia busara kwa kuacha upelelezi huru na kutoingilia uhuru wa Mahakama.

Kama kuna maelezo umeacha katika taarifa hii unaweza kupotosha umma ilikuwaje mpaka wamefikia hitimisho hili? (conclusion hii?). Utakuwa umetuletea hitimisho badala ya taarifa muhimu katika hoja yao.

Inawezekana na wao wameona Lulu anahukumiwa na jamii hata kabla ya kesi hivyo wanaona watamsaidia sio kwa kupanga njama bali kuhakikisha haki inatetendeka.

Kumsaidia mtuhumiwa kwa haki sio kosa kisheria kwani haki inafuata mkondo wa sheria.
 
habari yenyewe ya mwanzisha mada ni nyepesi sana 'kuwa wanataka kumsaidia kisheria' lkn watu humu ndani wanatoa maamuzi utadhani usiku ule walikuwapo live ktk tukio na kuhitimisha kuwa binti alilifanya hilo kwa makusudi.

Hii si habari nyepesi haijafahamika kama Lulu anahatia au la, sasa hawa Wabeijing (Bulaya & Mdee) wanaposema wanataka kumnasua wanamaanisha nini?
 
mkuu hiyo sentesi ya mwisho unamaanisha nini.

Mkuu ni Ukweli Kwamba Lulu hakuwa na Sifa nzuri katika Jamii, ni kweli kwamba Lulu alikuwa na Wapinzania wengi katika Maisha aliyokuwa anayaendeleza ( Namaanisha Kuchuna Mabuzi). Angalia blogs mbali mbali zilivyoripoti tukio la kifo cha Kanumba it is as if walikuwepo wakati wa Tukio na kushuhudia Lulu akimsukuma Kanumba.

Mkuu kuna sura Nyingi sana katika wale wanaomhukumu huyu Binti

1. Kuna wale ambao walikuwa hawapendi Tabia ya Huyu binti kwa Ujumla hawa sasa wanaona huu ndio muda mwafaka wa Binti kufundishwa Tabia njema, kwao suala kwamba Lulu anahitaji Kutetewa Maana. Hawa hawana Wivu na Lulu

2. Kuna Mashostito ambao walikuwa na tabia zinazofanana na Lulu ila Katoko kalikuwa kanawapiga bao Sokoni sasa hawa wivu unawaongoza katika Kujadili sakata la kifo cha Kanumba

Nafikiri Umenipata yeh yeh
 
Tupo hapa Jf tuliowahi kubaka na kufanya uzinzi wa aina ya Kanumba tunabeba mawe kumrushia kanumba ili jamii ituone sisi ni wasafi.

Kama tukikamatwa leo tunaingia kwenye kashfa nzito.

Tuwe na roho ya subira kuhukumu waliokufa twende mbele kuirekebisha jamii yetu ili tusipate akina Lulu wengi. Kushughulika na Lulu huyu tunapoteza muda mwingi wa kushughulikia akina Lulu wanaozaliwa kila siku.

Bomba la maji likipasuka tunalaumu maji au tunaziba sehemu iliyopasuka?
 
Nimesikitishwa na kauli zilizotolewa na wabunge Halima Mdee (CHADEMA) na Esther Bulaya (CCM) kusema kwamba wanataka KUMNASUA Elizabeth Machael (Lulu) anayetuhumiwa kusababisha kifo cha Kanumba. Kama wabunge walitakiwa kutumia busara kwa kuacha upelelezi huru na kutoingilia uhuru wa Mahakama.
Kifupi wewe aidha hujui sheria au hujui kazi ya wakili na mwanasheria. Hata jambazi lina haki ya kuweka wakili na kutetewa.
 
Inakera Mkuu kuona Watu wanamalizia hasira zao kwa Haka Kabinti. Hivi ngoja Nikuulize. Kosa la Haka Kabinti ni Lipi hasa?

Mkuu ninashangaa sana watu wanamwaga venom ya ajabu kuhusu huyu mtoto..! Yaani imefikia anaeonekana kumtetea kidogo ni mhaini..! Wanasahau ule msemo wa "it takes 2 to tango".. Kama wameamua kuwa chuki dhidi ya Lulu (ambae obvious udogo wake wa miaka na a stardom status aliyokuwa nayo) na wanashindwa kuwachukia wanaume ambao walim-exploit Lulu..! Na wengine ni wakubwa kuliko hata umri wa baba yake..! Hata Kanumba (RIP) hakustahili kuwa na yeye achilia mbali ku-mistreat the way alivyom-mistreat.. Na chuki inapitiliza mpaka wanaona hastahili haki zake kama mtuhumiwa..! Sidhani kama toka alipokamatwa alisomewa haki zake kisheria.. na kama mwanasheria alikuwapo wakati wa kuhojiwa..! Sasa wanapojitokeza wanasheria kutaka kuhakikisha haki inatendeka bado wenye chuki wanaponda..
Acheni kuhukumu.. Au kama ni lazima kuhukumu basi tuanze na hao wanaume waliomfikisha Lulu hapo.. Kanumba (RIP) akiwa mmoja wapo.. Otherwise hamna moral authority ya kuweka chuki zenu hadharani dhidi ya Lulu..
 
Acheni Vyombo vinavyohusika vifanye Uchunguzi huru. Well simpendi Lulu kwa Matendo yake katika Jamii lakini hilo lisiwe sababu ya nyie ku conclude kwamba Lulu Kamuua Kanumba. Hakuna ajuaye siri ya Kifo cha Kanumba zaidi ya Lulu na Kanumba Mwenyewe. Kanumba hayupo tumpe nafasi Lulu aelezee kilichotokea na Vyombo husika vipime kauli yake na kutoa Maamuzi kulingana na Utetezi wake

Sina uhakika sana, je Kanumba angekuwepo mzima angemuonea huruma Lulu. Turudi katika utu. Inawezekana ilikuwa ajali. Waacheni wanaotaka kumsaidia kisheria wafanye hivyo. Na mahakama itachukua mkondo wake. tusifanye prejudice.
 
Mkuu Inawezekana huko Kanumba anasikitika na jinsi watu wanavyomtundika Lulu katika Msalaba ( Hatujui) na kama angekuwa na uwezo wa Kuzungumza Pengine angesema ambayo yangetushangaza wengi, May be yeye ndiye chanzo cha Ugomvi uliopelekea Kifo Chake (Hatujui)
 
Hii si habari nyepesi haijafahamika kama Lulu anahatia au la, sasa hawa Wabeijing (Bulaya & Mdee) wanaposema wanataka kumnasua wanamaanisha nini?

Kwani Kumnasua maana yake ni nini? Yaani katika Maelezo yao yoooote wewe Umeona "Kumnasua tu"?
 
Back
Top Bottom