Wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya wamefurahi Kanumba kufa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya wamefurahi Kanumba kufa?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Kamura, Apr 12, 2012.

 1. K

  Kamura JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimesikitishwa na kauli zilizotolewa na wabunge Halima Mdee (CHADEMA) na Esther Bulaya (CCM) kusema kwamba wanataka KUMNASUA Elizabeth Machael (Lulu) anayetuhumiwa kusababisha kifo cha Kanumba. Kama wabunge walitakiwa kutumia busara kwa kuacha upelelezi huru na kutoingilia uhuru wa Mahakama.
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Masaburi at Work. Peleka Jukwaa la Umbeya au U-turn
   
 3. K

  Kamura JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuwa makini haiwezekani wabunge wakatoa kauli ya kijinga kama hiyo eti KUMNASUA na kesi.
   
 4. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ninavyofahamu mimi Mh. Halima Mdee ni mwanasheria. Kuhusu sakata la LULU (Elizabeth), pamoja na yote yanayozungumzwa bado anahitaji usimamizi wa kisheria ni haki yake. Tunaamini Mh. Mdee ama Mh. Bulaya hawawezi pindisha sheria kama Lulu atakutwa na kosa la mauaji kwa kukusudia.

  Pia kama itadhihirika kuwa anaumri wa miaka 17 (ingawa najua alishajitangaza na kusheherekea miaka18), atahitaji usimamizi na ushauri kama mtoto maana anaweza kuathirika vibaya sana na pressure ya jambo hili.

  Tunaamini akipata usimamizi na usaidizi wa kisheria, na kama atahukumiwa kwa kisa la mauaji, basi itakuwa haki imetendeka. Tusipende kukimbilia kuhukumu, bali nakubaliana bado kunautata mkubwa kwenye tukio hili la kusikitisha ssana.
   
 5. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Halima wewe tunakuheshimu sana, achana na hili tukio. Lulu ameharibika siku nyingi sana tena akiwa under 18, picha za uchi kwa mitandao n.k. hamkusema kitu, sasa matokeo ya kuharibika kwake mnataka mseme, acha dada yangu maana inataka kuwa kama mwehu kuongelea athari za kuharibika kwake bila kuongelea kuharibika kwenyewe.

  Unakumbuka alikana kuwa hana uhusiano na Kanumba, Je imekuwaje tena? ni muongo hivyo kila analosema hatuwezi kuamini kirahisi. Under 18 kapata wapi driving license? ni muongo huyo dada yangu atakuchafua bure. Kituoni aliandikisha ana miaka 18, kwani hajui hata umri wake? Mama yake akaleta cheti ana miaka 16 na siku 360 hadi leo hapo tena inaonesha ni muongo.

  So please achane naye, ashughulike na waongo waongo wenzake sio wewe.
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tatizo lako ni Kufikiria kwa Makalio ambayo hayajatawazwa watu watarajie nini kutoka kwako? Fikra pumba zenye harufu ya Chooni?

  Ungeweka Maneno ya Wabunge, Ungeweka ni kwa namna gani wataathiri mwenendo wa Kesi na Ungetuambia ni kwa nini Lulu hastahili watetezi.

  La Sivyo Katawaze ili fikra zako zitakaswe
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Acheni Vyombo vinavyohusika vifanye Uchunguzi huru. Well simpendi Lulu kwa Matendo yake katika Jamii lakini hilo lisiwe sababu ya nyie ku conclude kwamba Lulu Kamuua Kanumba. Hakuna ajuaye siri ya Kifo cha Kanumba zaidi ya Lulu na Kanumba Mwenyewe. Kanumba hayupo tumpe nafasi Lulu aelezee kilichotokea na Vyombo husika vipime kauli yake na kutoa Maamuzi kulingana na Utetezi wake
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Sikujua kama mtuhumiwa wa mauaji hana haki ya kutetewa.................!
   
 9. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kumbukeni sio mara ya kwanza lulu anafikishwa kituoni, mara zingine fujo zake zinamkumba hata mama yake; hapo ndo mngekemea tabia hiyo, sasa kuna tukio kubwa tena la kisheria, wabunge makini ningetarajia wangeacha sheria ifute mkondo wake, acheni mambo ya gender gender kwenye suala kubwa kama la kuhusiwa mauaji, hata kama ni kwa bahati mbaya, mahakama itajua.
   
 10. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hata wakimtetea,we inakuhusu nin? Na isitoshe ni haki yake kutetewa,af pia unataka anyongwe af iweje?nyie ndo walewale ukisikia mwizi unatoka na tofali unamponda kichwa! Si vizuri kuhukumu,hakuna anaejua ukweli zaid yao,hata ivo no1 is perfect! Mungu pekee ndo atakaehukumu kwa haki! Wangejitokeza wote wa Chadema ungesemaje?au wote CCM?
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Just Because ni Lulu, Mtoto mwenye Tabia isiyopendeza basi ndio kisa eti Asitetewe. Lulu ana Haki ya Kikatiba kutetewa. Mbona yule Mzungu alimfanyisha Mapenzi Mbwa wake na Mwanamke wa Kibongo alitetewa. Why not Lulu? Hakuna ajuaye nini Kilipelekea Kanumba kupata Brain Concussion, yawezekana kabisa Mtoto wa Watu alikuwa anajitetea dhidi ya Vitendo viovu?. Kwani ni Mara ngapi Mmekosana na Mpenzi wako mkasukumana lakini bahati nzuri tu hakuna Aliyekufa. Come on guys
   
 12. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja na yote nado hicho kibinti kina haki ya kupata msaada wa kisheria,hatujui yaliyojiri chumbani wakiwa na Kanumba,na kama ilijulikana kabinti kameshaharibika,hata aliyekachukua naye hakujitambua! tuache sheria ichukue mkondo wake na haki itendeke!
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ni Vipi Wamezuia Sheria isichuke Mkondo wake? Mbona Lulu keshafikishwa Mahakamani tayari
   
 14. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mods ondoeni hizi... Maana mimi nimewasikiliza hawa wabunge wanachokisema kiko sawa.
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Kuna Mashosti huko Mtaani Lulu alikuwa anawakimbiza Kweli kweli sasa wanafunga ili Maskini haka katoko Kasitendewe haki. Lulu alikuwa anawapiga bao katika kuchuna Mabuzi
   
 16. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mmmh mbona maneno makali namna hiyo mkuu asubuhi yote hii...umeguswa kunako?
   
 17. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  habari yenyewe ya mwanzisha mada ni nyepesi sana 'kuwa wanataka kumsaidia kisheria' lkn watu humu ndani wanatoa maamuzi utadhani usiku ule walikuwapo live ktk tukio na kuhitimisha kuwa binti alilifanya hilo kwa makusudi.
   
 18. k

  kuzou JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kisheria wenye kesi za mauaji wote hupangiwa mawakili wa utetezi bure,mtuhumiwa ana haki ya kuongeza wake,kwa sasa hahitaji msaada wa kisheria kwa kua kesi haijaanza rasmi,itaanza mahakama kuu atakaposhtakiwa rasmi,tena anaweza asishtakiwe kbs.kumbuka dito alishtakiwa kwa mauaji isivyo rasmi kisutu,badae kuua bila kukusudia rasmi mahakama kuu na kupewa dhamana mawakili wanahitajika hapo. mie nafkiri mdee na huyo mwenzie wangeshughulika kutafuta wabakaji(wapenzi) wa huyo mtoto wawafungulie kesi tofauti.kisheria walikua wanambaka
   
 19. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #19
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Si tu kwa makusudi inawezekana wala hata Hakufanya Mtoto wa watu
   
 20. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Inakera Mkuu kuona Watu wanamalizia hasira zao kwa Haka Kabinti. Hivi ngoja Nikuulize. Kosa la Haka Kabinti ni Lipi hasa?
   
Loading...