Wabunge fanyeni haya kuondoa tatizo la ajira

Vawulence

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
1,928
2,101
Miaka ya karibuni hapa nchini kumekuwa na tatizo kubwa sana la ajira kwa vijana hasa wasomi.

Pamoja na tatizo hili wabunge wa pande zote wamekuwa wakiitupia tu lawama serikali bila kutoa suluhisho.

Leo napenda niwashauri wabunge kuwa ni kwanini
1. Wasipeleke bungeni muswada wa mabadiliko ya umri wa kustaafu ili wazee waachie nafasi kwa vijana? Kwa kuanzia umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria iwe miaka 55 walau.

2. Wabunge waishauri serikali ianzishe miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji kwa vijana kwa ubia na serikali. Kuna mamilioni ya heka zinazofaa kwa kikimo. Pia hii inaweza kufanyika kwa ufugaji.

3. Wabunge wafanye namna wizara ya Elimu iweze kuandaa mitaala itakayowaandaa vijana kwenye fani mbalimbali wanapohitimu. Shule isiwe sehemu tu ya kukariri. Wanaweza kufanya tafiti kwenye seminari za Katoliki waone vijana wanavyoandaliwa kujitegemea. Inaweza kuwa kufundishwa ufundi mbalimbali, muziki, kilimo n.k....
 
Nilishawahi kuleta wazo hapa ili nchi iendelee watu hawatakiwi kufanya kazi muda mrefu hivyo kama ilivyo sasa...
Kuanzia chuo, serikali ipeleke fresh candidates toka form6 wale cream wakachote elimu ya kisasa nje ya nchi warudi na elimu nzuri waje kuwa ndio Lecturers wafundishe what happens in real world sio kuja kukaririshana ma theories.

Kuwe na kazi za mikataba serikalini 3-5 years...Mitatu ya mwanzo lazma mtu aoneshe uwezo mkubwa na ufanisi katika kufikia malengo kisha ataongezwa miwili ya mwisho, akizengua tu baada ya mitatu ya kwanza out. Anaachia kiti wanaingia fresh and skilled candidates graduates wa chuo ambao wako more current na corporate trends management yote inabadilika.

Wale wanaotoka wanaweza kurudi vyuo wapewe mkataba as part timers wakapige brush vijana juu ya nini kinahitajika kazini maana watakuwa tayari na experience ya elimu kwa vitendo. Ama wanaweza kujiajiri tu na kufanya vitu vyenye tija kulingana na taaluma zao, kwa wale wa science wanaweza kwenda viwandani kusimamia processing pia kwa muda kabla ya kujiajiri.

Faida yake kuu watu watakuwa very active hamna kuzembea na kuzoea ofisi kiasi cha kuanzisha mianya ya ufisadi na wizi. Kazi ya serikalini isiwe sehemu ya kupumzikia kama ilivyozoeleka.
 
Umenena vyema mkuu. Serikali inapaswa kuelewa kuwa mikataba inaleta ufanisi kuluko ajira za kudumu.
 
pia waachie fao la kujitoa naamini ajira zitapatikana kwa wingi kwani naamini mtu akishapiga kazi miaka yake 5 au kumi itamtosheleza kupat pesa za kujiajiri mwenyewe..na nafasi aloacha atajiriwa mtu mwingine..
 
Vijana tunawaombeni viongozi wote wa vyama vya upinzani mlioko bungeni na nje ya bunge tunaomba mtuombee ajira za walimu toka serikalini kwani miaka yote ajira zetu zilikuwa ni za moja kwa moja toka serikalini , nyie ndio watu pekee mnaoweza kutupazia sauti sisi wanyoge tulioko uraiani.
Tunaombeni tupazien sauti popote mlipo na hapo ndipo mtakuwa mmeonyesha ushirikiano katika kipindi hiki kigumu kwetu sisi walimu tarajali.
 
Hii nchi haitahiji tena walimu washakuwa wengi hasa wa art.... Selikali haina pa kuwapeleka
 
Vijana tunawaombeni viongozi wote wa vyama vya upinzani mlioko bungeni na nje ya bunge tunaomba mtuombee ajira za walimu toka serikalini kwani miaka yote ajira zetu zilikuwa ni za moja kwa moja toka serikalini , nyie ndio watu pekee mnaoweza kutupazia sauti sisi wanyoge tulioko uraiani.
Tunaombeni tupazien sauti popote mlipo na hapo ndipo mtakuwa mmeonyesha ushirikiano katika kipindi hiki kigumu kwetu sisi walimu tarajali.

sasa mwalimu unaandika hivi? kiswahili kibovu

kuna vijana unataka umuajiri, kaanza kukosea kwenye cover letter tu

be competent and get ready for any job out there

huyo mbowe yuko KIA na wema sepetu saa hizi
 
Acha lugha chafu kijana kama nime kosea si ungenirekebisha tu alafu acha kujifanya mjuaji wakati hujui kitu.
 
sasa mwalimu unaandika hivi? kiswahili kibovu

kuna vijana unataka umuajiri, kaanza kukosea kwenye cover letter tu

be competent and get ready for any job out there

huyo mbowe yuko KIA na wema sepetu saa hizi
UNAJIFANYA UNAJUA WAKATI HUJUI KITU.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom