Wabunge Dr. Slaa na Dr. Tarab wafanyiwa umafia!

Nudgu yangu Ibrah,Binafsi naamini kuwa vyombo vya dola vipo kwa ajili ya kulinda umma na mali zake.sasa kwa ajili ili mradi tayari lipo mikononi mwa vyombo vya usalama kama alitabaiinisha mtendewa kwenye mahojiano na ITV,tusiwe waganga wa kienyeji kutabiri bali yeye binafsi mh.DR.slaa anaviamini vyombo vya dola vitafanya kazi yake kwa uadilifu na umakini mkubwa na taarifa sahihi ya kilichotokea wananchi tutapatiwa kupitia vyombo husika.

yalikuja mambo ya uchawi bunge yakakuzwa kweli kweli taarifa ya mkemia mkuu ikiwa unga wa mahindi eehheeeh!!!!!

Naamini serikali ya ccm inasimamia vyema utawala wa sheria hivyo tusubiri taratibu na hatua zinazochukuliwa na zitakazo chukuliwa na taasisi husika za serikali.
 
Ka ukumbi kamejaa. Duu, kweli kuna issue siku zote zinauzika kiurahisi. Ndiyo uzuri na ubaya wa hizi habari katika jamii.

Ma vifaa ya kipepelezi na kugundua vifaa vya kipepelezi kwa nchi za Eastern Europe na zaidi ni kwa mama yao Russia, ni vingi sana na vipo tu madukani. Nafikiri wao kwa sasa yaani KGB na ndugu zao FBI/CIA/MI6/ nk watakuwa na vya kisasa zaidi na hasa vya kuogopa ni vile vinavyorusha mawimbi ya chini sana (kama jeshi la Marekani) na kiboko ni vile vinavyobadili mawimbi yake katika range kubwa sana.

Alichokisema Mtanzania juu ya kukutania PARK au jangwani kuongea ni jambo muhimu sana. Pia unapoongea unaziba mdomo maana kuna vyombo vinaweza hata kujua unaongea ninikwa kusoma mdomo wako. Pia park kwa sababu ziko mjini, kuna antena zinazoweza kunasa sauti zenu hata kama mko mita 50.

Mazungumzo ndani ya nyumba ni hatari sana. Warusi ndiyo baba lao kwa kunasa sauti kupitia nyumba zilizojengwa kwa Cement concrete. Kuna mkutano jamaa walishawahi kufanya na ilibidi kuanzia mwanzo hadi mwisho wawe wanaandika kwenye karatasi kwa kuogopa vifaa hivyo. Pia East German walikuwa wakali wa kusana kupitia mabomba ya maji. Wanakusikiliza kila kitu. Nafikiri kuna umuhimu wa watu kama Slaa na informer wake wawe wanatumia CODES au maneno ambayo ni wao tu watajua maana yake. Vinginevyo umekaangwa.
Olaah, namuona Dr. Slaa mwenyewe in this house. Dr, tumegee yaliyosibu, twakusubiri.
 
Invisible nimekupata

Naomba uweke clip ya ITV hapa.Ila tumekuwa tuliilaumu serikali ya Rais kikwete kuwa ni serikali ya kisaniii na viongozi wake ni wasanii wa kutupa.Ndiyo inawezekana, ila usaniii wa namna hii sijawahi kuona na kama ukiendelea kutukuzwa tunaleleke akubaya.

Kwanini kila mara ZOTE wanaotafutwa ni watu wa kutoka sehemu moja tu.Dr. Slaa hana uwezo wowote wa kuitisha serikali.Period!

Serikali ina mkono mrefu na ikitaka hata kujua aliyemwambia Mengi habari ambazo hazithibitishwa mpaka leo itampata.Kumekuwa na maneno ya kutunga tunga yasiyo na maana yoyote.

Kwa uzeofu wangu kama wallitaka kumtape Slaa hawakutakiwa hata kuweka hicho kifaa ndani.Hii ni danganya toto ya Slaa mpaka hapo atakapotoa ushahidi ni nani alimambia na ithibike
 
Last edited:
Unachosema gembe ni kweli yaani kwa dunia hi ya sasa ilivyoendelea watu watumie njia butu kama hizo kumnasa mtu ?
 
Sifa kubwa ya Ufalme unaofitinika ni kufanya mambo yanasababisha kuanguka kwa ufalme huo bila kujua. Hii inanikumbusha kisa cha Mfalme Nero wa Rumi (Roma) wakati Ukristo uliposhika kasi huko Italia. Baada ya kuwatafutia kila sababu ya kuwaangamiza na kuona kuwa haimsaidii bali unaendlea kwa kasi, aliamua kuuchoma moto Mji wa Roma na kuwasikingizia Wakristo kuwa ndiyo waliofanya kitendo hicho cha aibu. Lakini hatimaye Wananchi wakaamua kumgeuka na kumkimbiza kama mwizi na hatimaye kummaliza na hiyo ndiyo people power.

Nachokiona hapa ni kuwa lazima kuan watu ndani ya Serikali wanampinga JK kwa nguvu zote na wanafanya vitendo vya aibu ili kumuaibisha na kumdhalilisha JK mbele ya Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa, JK akiwaonea aibu basi ajue ni kwa hasara ya ufalme (utawala) wake mwenyewe. Lazima awatafute na kuwawajibisha watu hao waliofanya vitendo vya kuudhalilisha utawala wake na kuipaka nchi matope.

Kwa maoni yangu nadhani JK atajipa kazi kubwa sana kuanza kuwatafuta wanaohujumu mbinu chafu za serikali yake. Kwa sababu kazi wanayofanya ni takatifu kwa umma, haweza kushinda hiyo vita. Ningemshauri aachane na upuuzi wa mafisadi aungane na umma. Umma una nguvu zaidi ya kumlinda kuliko mafisadi!
 
Mimi siku zote vyombo vya dora iwa nakuwa sina imani navyo hata kidogo kutokana na kushughulikia maswala kadha wa kadha hapo watakacho fanya ni kupindisha ukweli.Sijui ngoja tuwasubili watakavyo tudanganya.
 
Yaliyojiri Dododma jana usiku ni kweli kabisa.

Kilichotokea ni kama kilivyoelezwa ila wasiwasi mkubwa ni je? kama wameweza kupenya na kuweka vifaa hivyo afya ya Dr.Slaa na mwenzake ikoje?

Hiki ni chumba cha hotel ambacho Dr.Slaa tangu aingie bungeni mwaka 1995 amekuwa akiishi na pamekuwa kama nyumbani mwake kila kipindi cha bunge na hata mwenye hoteli huwa hampi mtu chumba hicho hata kama Slaa hayupo kwa heshima ya mteja wake .

Kwanini ameamua kuishi hapo muda wote , unaweza kutumia saikolojia rahisi ili kuweza kungamua.

Jana usiku kwenye taarifa ya habari ya TBC1 ya saa sita usiku walirusha habari hiyo na waliwasiliana moja kwa moja na mwandishi wao aliyeko Dodoma jina anaitwa Prudence Constantine, na pia taarifa za habari za leo asubuhi wamerusha hao hao TBC1.

Kuna mambo mengi hapa kwani inawezekana kabisa kuwa lengo walitaka kujua kunachoendelea, ila wasiwasi zaidi ni juu ya hali za afya yake.

Kuna mmoja wa viongozi wa kisiasa mkoani Rukwa Wilaya ya Sumbawanga mbunge alipotofautiana naye alisuka mpango wa kumkamatisha na viungo vya ALBINO na suala hili liliripotiwa Polisi Sumbawanga ila mpaka leo hakuna hatua wala taarifa juu ya jambo hili, hivyo kaeni chonjo.
 
Unachosema gembe ni kweli yaani kwa dunia hi ya sasa ilivyoendelea watu watumie njia butu kama hizo kumnasa mtu ?

Shy, aliekwambia tza ni ma-expert ktk tasnia ya intelejensia ni nani? Tupo nyuma kwelikweli ktk fani hii technologically!!!
 
Kama wanatumia njia kama hizo waelewekeje?

Kwa jinsi TEchnolojia ya mawasiliano ilivyo kwa sasa.Kama unataka kujua Dr. Slaa anawasiliana na nani ni rahisi sana..Very easy!

Hiyo ni zuga tu.Hakuna kitu
 
Napenda kutoa maagizo sababu maagizo ndiyo yanayofaa siku zote.Enzi za Mwalimu watu walikuwa wakipewa maagizo na kuyatekeleza ila kwa saasa watu wengi wameuwa wakifanya wanavyotaka wao bila kutekeleza maagizo.

Inawezekana ni tabia yako au ya mwingine kutopenda Maagizo.


Ndiyo ni tabia yangu kutopenda maagizo yako. Ukiwa na maagizo jiagize wewe mwenyewe halafu uyatekeleze. Hii tabia ya kuwapa maagizo watu wengine inanikumbusha sana viongozi wa CCM. Ni wepesi sana kutoa maagizo ya kila namna ili mtu mwingine afanye kitu.

Zamani watu wa namna hii ambao walikuwa wanaketi kwenye viti vyao vya endi na kutoa maagizo kwa watu wengine huko wao wenyewe hawafanyi lolote walipewa jina moja la kitaalamu. Sikumbuki walikuwa wanaitwaje.

Haya nasonga mbele (nimejiagiza).

LOL

Invisible nimekusoma Mkuu,Nilitumia jina lako makusudi ili kuweka mambo sawa sababu wachangiaji waliokuwa wakifuatilia mtiriko kutoka kwako hadi kwa Mzee Mwanakijiji walikuw akienda nje kidogo ya jambo lenyewe!

Unhealthy and unnecessary.
 
Kwa jinsi TEchnolojia ya mawasiliano ilivyo kwa sasa.Kama unataka kujua Dr. Slaa anawasiliana na nani ni rahisi sana..Very easy!

Hiyo ni zuga tu.Hakuna kitu
Utajuaje? alafu naona hoja zako zimejaa jazba na kutokuelewa....ni kutumia akili ndogo tu sio lazima uwe cheti cha darasa la 7 kuelewa.....kwa hiyo unasema Dr slaa kazuga nini? kajiwekea ving'amuzi hivyo?
 
Namwona Dr.Slaa hapa.
Mheshimiwa tunaomba ufafanuzi kidogo ni nini kinaendelea mpaka sana.Tupo nyuma yako mpiganaji wetu.
 
Kwa vile Dk Slaa anaonekana muda hu yumo humu ndani ya JF(anaonekana yupo online) ni vema akatupa japo kiduchu ni nini kilijiri ndani ya chumba chake pale Hotel 56...Mkuu Dk Slaa tunakuomba ututegulie kitendawili hiki maana wewe ndo unajua nini kilitokea...Maana kilichopo sasa ni kwamba kila mtu anaongea chochote anachokijua katika kuchangia habari hii...Tueleze mkuu maana hapa ni JF 'where we dare to talk openly'
 
Kwa vile Dk Slaa anaonekana muda hu yumo humu ndani ya JF(anaonekana yupo online) ni vema akatupa japo kiduchu ni nini kilijiri ndani ya chumba chake pale Hotel 56...Mkuu Dk Slaa tunakuomba ututegulie kitendawili hiki maana wewe ndo unajua nini kilitokea...Maana kilichopo sasa ni kwamba kila mtu anaongea chochote anachokijua katika kuchangia habari hii...Tueleze mkuu maana hapa ni JF 'where we dare to talk openly'
Mkuu Balantanda,

Uwezekano wa Dr.Slaa kusoma haraka kuanzia mwanzo mpaka tulikofikia sijui kama ni mkubwa kiwango hicho. Wewe waweza kusoma kwakuwa ulianza kusoma kabla yake lakini naye anahitaji muda aone wapi tumeenda visivyo na kutupa ukweli wa habari yenyewe.

Karibu Mhe. Slaa
 
Kwa jinsi TEchnolojia ya mawasiliano ilivyo kwa sasa.Kama unataka kujua Dr. Slaa anawasiliana na nani ni rahisi sana..Very easy!

Hiyo ni zuga tu.Hakuna kitu

Hivi unakumbuka Kombe alivyouawa? Wasn't very smart....or was it?
 
Tatizo humu ndani kuna watu wa kila aina kwani wengine ni watetezi wa uovu na wengine ni watetezi wa ukweli, sasa anapojitokeza mtu na kusema kuwa eti Dr.Slaa kazuga mimi simuelewi hata kidogo, hivi Dr.Slaa anahitaji kujitafutioa umaarufu ambao anajua wazi kuwa wabaya wake wanaweza kuchunguza na kumuumbua hadharani?

Tanzania bila Ufisadi -INAWEZEKANA.
 
Mkuu Balantanda,

Uwezekano wa Dr.Slaa kusoma haraka kuanzia mwanzo mpaka tulikofikia sijui kama ni mkubwa kiwango hicho. Wewe waweza kusoma kwakuwa ulianza kusoma kabla yake lakini naye anahitaji muda aone wapi tumeenda visivyo na kutupa ukweli wa habari yenyewe.

Karibu Mhe. Slaa
nimebakiwa na masaa 6 namsubiri atufafanulie......karibu Dr
 
Mkuu Balantanda,

Uwezekano wa Dr.Slaa kusoma haraka kuanzia mwanzo mpaka tulikofikia sijui kama ni mkubwa kiwango hicho. Wewe waweza kusoma kwakuwa ulianza kusoma kabla yake lakini naye anahitaji muda aone wapi tumeenda visivyo na kutupa ukweli wa habari yenyewe.

Karibu Mhe. Slaa

Nimekusoma mkuu..Hata hivyo nadhani kwa muda aliokoaa tayari keshajua ni nini chazungumzwa humu(hahitaji kusoma kila kitu)...Hata hivyo kinachohitajika ni yeye Dk kutujuza nini kimetokea jana maana kilichopo ni kwamba baadhi ya wachangiaji wameshaanza kujibizana wenyewe kwa wenyewe,sasa kwa nini iwe hivi ilhali mhusika mkuu wa sakata hili(anayejua kila kitu kuhusiana na taarifa hii) yumo humu,so ni vizuri atueleze nini kiltokea hiyo jana ili tujue nini cha kuchangia(baada ya kupata taarifa toka kwake)...Karibu Dk.Slaa
 
Hii inashangaza watu wenye akili kuweza kuzugwa kwa maneno.

a. Watu waliokuta vifaa hivyo ni watu wawili (mpaka sasa). Nao ni Dr. Slaa na Dr. Taarab. Hawa ni Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuna watu wanataka kufanya hili kuwa ni la Dr. Slaa, kwamba baada au kabla ya kuweka kifaa hicho kwenye chumba chake alienda pia kwenye chumba cha Dr. Tarab. Kwenye hoteli hiyo wapo wabunge wanne (wawili wengine wa CCM). Ha wawili waliangalia hawakukuta kwenye vyumba vyao.


b. Kufanya hili suala ni "Dr. Slaa" ni kutotendea haki uwezo wa mwanadamu kuona,kufikiri, kuamua na kutenda. Hili suala linahusu wabunge wawili ambao kuna watu wameweza kuingia hadi vyumbani mwao na humo vyumbani hadi kuweza kuinua kitanda (walikuwa na kitu kinaitwa muda). Kwamba hilo linawezekana inatosha kushtua.


c. Hoteli hiyo siyo hoteli uchwara au iko "uswahilini" kiasi kwamba mtu anaweza kuingia na kufanya lolote kwenye chumba cha Mbunge. Mtu anaweza kusema "Dr. Slaa anatuzuga" kwa faida ya nani? Watu wanaosema hivyo hawajui uzito wa tishio ambalo Dr. Slaa amelileta kwa watu wengi. NI mpuuzaji wa ukweli yule anayedhania Dr. Slaa katika impact ya taifa ni sawa na one Chitalilo! Hivyo si mkweli yule anayedhani kuwa Dr. Slaa siyo target ya uovu. Mtu anayefikiri hivyo ni naive.

d. Kuna watu wachache sana wanaoweza kuingia hoteli yoyote ambayo analala mbunge au waziri aidha kupata ruhusa ya kuingia hadi chumbani au na wao kupanga chumba hapo hapo na wakitumia funguo malaya kuweza kuingia humo na kufanya watakavyo. What if, tumeamka asubuhi hii na kusikia kuwa Dr. Slaa kafanyiziwa unyama chumbani kwake? Nina uhakika kuna watu watasema hapana "Dr. Slaa alikuwa anajaribu kutuzuga mambo yakaenda kombo"!


f. Kuna watu ati wanata kujua ni nani alimtonya Dr. Slaa kuhusu vifaa hivyo. Ati wakijua ndiyo wataamini! HIvi wanatuchukuliaje sisi. Anayetaka kujua ni nani alimuambia Dr. Slaa kuhusu bugs hizo niandikie PM nitakudokeza na wewe usimwambie mtu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom