Wabunge CHADEMA watimuliwa Bungeni wakipinga Mbunge CCM kuchana hotuba yao

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson amewatoa ndani ya ukumbi wa Bunge wabunge watatu wa Chadema walioibua zogo bungeni kuhusu uamuzi uliochukuliwa dhidi ya mbunge wa Kasulu Vijijini (CCM), Augustine Vuma aliyechana kitabu cha hotuba mbadala ya bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni mwaka 2019/2020.

Wabunge hao ni Esther Matiko (Tarime Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Dk Emmaculate Sware (Viti maalum), ambao walipinga uamuzi wa Dk Tulia kumtaka Vuma kuomba radhi kwa alichokuwa akizungumza wakati akichana kitabu hicho, si kitendo chake cha kuchana kitabu.

Dk Tulia alichukua uamuzi huo kwa maelezo kuwa taarifa iliyoombwa na mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka baada ya Vuma kuchana kitabu hicho, inazungumzia mbunge kutamka maneno yasiyoruhusiwa bungeni.

Vuma wakati akizungumza utekelezaji mzuri wa miradi ya Serikali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), alishika kitabu hicho cha upinzani na kusema kina maneno yasiyofaa na kinafaa kuchanwa kisha kukichana.

Tukio hilo limetokea leo jioni Jumanne Juni 18, 2019 wakati Vuma akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2019/2020 ya Sh33. 1 trilioni.

Mchangiaji wakati akizungumza amechana hotuba ya upinzani ndani ya Bunge nafikiri jambo hili ni dharau kubwa. Ni kutojielewa kwa mbunge na hajui kwa nini vitabu hivi amepewa. Achukuliwe hatua maana tumemuona kama kichaa fulani hivi ndani ya Bunge,” amesema Mwakajoka aliyetumia kanuni ya 64 ya Bunge kutoa taarifa hiyo.

Katika majibu yake Dk Tulia amesema, “Ameitaja kanuni ya 64 japokuwa ufafanuzi wake haukuwa haswa katika kifungu gani ambacho kimevunjwa, kanuni hii inazungumzia mambo yasiyoruhusiwa bungeni na ukiisoma fasili ya kwanza inazungumza kuhusu kutotumia lugha ya kuudhi au inayodhalilisha watu wengine.”

“Kwa mchango wa Vuma hoja iliyopo itakuwa si kuchana kitabu maana amezungumza wakati akichana kitabu. Vuma maneno ya kuhusu kukichana kitabu nitakupa fursa ya kuyafuta na jambo hili lisirudiwe tena.”

Baada ya kupewa fursa hiyo Vuma alifuta maneno hayo na kusisitiza, “ila ilikuwa ni kuonyesha namna gani ambavyo hotuba hii haina maslahi kwa umma.”

Kauli hiyo iliwanyanyua Heche na Matiko na kutaka mbunge huyo kuchukuliwa hatua zaidi.

“Waheshimiwa wabunge ndio maana huwa nasisitiza anapozungumza mmoja wetu kumsikiliza, Vuma ameonyesha kitendo ambacho mimi nimeshakitolea ufafanuzi, wakati amesema kitabu hiki kinapaswa kuchanwa. Vuma ameshaambiwa afute hayo maneno,” amesema Dk Tulia ambaye kabla hajamaliza wabunge wa upinzani walitaka achukue hatua zaidi.

“Naomba mtoke nje maana hatuelewani. Matiko na Heche namba mtoke nje. Matiko simama uende nje,” amesema Dk Tulia.

Dk Sware aliposimama na kutaka kutoa taarifa naye alitakiwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Wabunge hao hawakutoka hivi hivi kwani ililazimika kutolewa na askari wa Bunge waliolazimika kutumia nguvu kumtoa Heche ambaye alikuwa amegoma.
 
Kwa hatua hiyo aliyochukua Tulia, ni dhahiri amekomaa sasa ndio atachukua nafasi ya Ndugai rasmi bunge lijalo. Vinginevyo ili Ndugai alinde nafasi yake yeye inabidi ampige vibao vya kutosha Mbowe ndani ya bunge kuonyesha yeye ni mkatili zaidi. Sasa hivi ili upate au kulinda cheo ni lazima uwafanyie hujuma za wazi wapinzani.
 
Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amewatoa nje ya ukumbi wa Bunge wabunge wa Chadema, Esther Matiko (Tarime Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Dk Emmaculate Sware (Viti maalum) kutokana na wabunge hao kutoridhishwa na uamuzi wa Dk Tulia dhidi ya mbunge wa Kasulu Vijijini (CCM), Augustine Vuma aliyechana kitabu cha hotuba mbadala ya bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni mwaka 2019/2020 wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni
 
Hivi mapendekezo ya bajeti ya vyama vya siasa imelenga kukusanya kwa vyanzo vipi?nje na vilivyopo au wanavyo vilalamikia wengi
 
2020 watanzania lazima tuwe na ujasiri wa kumtizama shetani usoni na kumwambia NO, not anymore! kinyume na hapo hivi vituko vya bibi ngongoti vitakua ndio kawaida kuanzia 2020-2025.
hapo sasa changanya na roho ya korosho ya bwana yule.
 
Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amewatoa nje ya ukumbi wa Bunge wabunge wa Chadema, Esther Matiko (Tarime Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Dk Emmaculate Sware (Viti maalum) kutokana na wabunge hao kutoridhishwa na uamuzi wa Dk Tulia dhidi ya mbunge wa Kasulu Vijijini (CCM), Augustine Vuma aliyechana kitabu cha hotuba mbadala ya bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni mwaka 2019/2020 wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni
Inauma sana Mkuu
Tufike mahali kuna watu wanahitaji kuchapwa viboko mtaani
Nchi imeoza haielezeki
Huu ubabe wa ccm wanautoa wapi?
Sheria inasemaje kwenye hili Mkuu
Tz ya viwanda imegeuka Tz ya visasi
Ipo siku isiyo na jina mtaani kutakuwa hakutoshi
 
video ya kusapot thread,kwa sisi majaji kabla ya kazi tunatakiwa tusikilize pande zote ndipo tutoe hukumu
 
2020 watanzania lazima tuwe na ujasiri wa kumtizama shetani usoni na kumwambia NO, not anymore! kinyume na hapo hivi vituko vya bibi ngongoti vitakua ndio kawaida kuanzia 2020-2025.
hapo sasa changanya na roho ya korosho ya bwana yule.
Hili bongo muvi nimeacha lifuatilia kitambo, ila kama mjadala bado unaendelea nitatamani na mbunge wa upinzani aichane ile ya serikali halafu tuone sub woofer atafanya nini kama double standard itathibitika dhahiri...
 
Kama kuna mtu nchii hii hatakiwi kuwa kiongozi basi Ni huyu Tulia ackson ila ndo vile wafu hutembea njia moja muovu humkumbatia muovu mwenzie huyu mama hana kila sifa za kuwa kiongozi huwezi mlinganisha hata chembe na bosi wake huyu kazidi kwa roho mbaya Kama mapokezi yake anashindwa kukemea upuuzi huu na kuchukua hatua.
 
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson amewatoa ndani ya ukumbi wa Bunge wabunge watatu wa Chadema walioibua zogo bungeni kuhusu uamuzi uliochukuliwa dhidi ya mbunge wa Kasulu Vijijini (CCM), Augustine Vuma aliyechana kitabu cha hotuba mbadala ya bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni mwaka 2019/2020.

Wabunge hao ni Esther Matiko (Tarime Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Dk Emmaculate Sware (Viti maalum), ambao walipinga uamuzi wa Dk Tulia kumtaka Vuma kuomba radhi kwa alichokuwa akizungumza wakati akichana kitabu hicho, si kitendo chake cha kuchana kitabu.

Dk Tulia alichukua uamuzi huo kwa maelezo kuwa taarifa iliyoombwa na mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka baada ya Vuma kuchana kitabu hicho, inazungumzia mbunge kutamka maneno yasiyoruhusiwa bungeni.

Vuma wakati akizungumza utekelezaji mzuri wa miradi ya Serikali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), alishika kitabu hicho cha upinzani na kusema kina maneno yasiyofaa na kinafaa kuchanwa kisha kukichana.

Tukio hilo limetokea leo jioni Jumanne Juni 18, 2019 wakati Vuma akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2019/2020 ya Sh33. 1 trilioni.

Mchangiaji wakati akizungumza amechana hotuba ya upinzani ndani ya Bunge nafikiri jambo hili ni dharau kubwa. Ni kutojielewa kwa mbunge na hajui kwa nini vitabu hivi amepewa. Achukuliwe hatua maana tumemuona kama kichaa fulani hivi ndani ya Bunge,” amesema Mwakajoka aliyetumia kanuni ya 64 ya Bunge kutoa taarifa hiyo.

Katika majibu yake Dk Tulia amesema, “Ameitaja kanuni ya 64 japokuwa ufafanuzi wake haukuwa haswa katika kifungu gani ambacho kimevunjwa, kanuni hii inazungumzia mambo yasiyoruhusiwa bungeni na ukiisoma fasili ya kwanza inazungumza kuhusu kutotumia lugha ya kuudhi au inayodhalilisha watu wengine.”

“Kwa mchango wa Vuma hoja iliyopo itakuwa si kuchana kitabu maana amezungumza wakati akichana kitabu. Vuma maneno ya kuhusu kukichana kitabu nitakupa fursa ya kuyafuta na jambo hili lisirudiwe tena.”

Baada ya kupewa fursa hiyo Vuma alifuta maneno hayo na kusisitiza, “ila ilikuwa ni kuonyesha namna gani ambavyo hotuba hii haina maslahi kwa umma.”

Kauli hiyo iliwanyanyua Heche na Matiko na kutaka mbunge huyo kuchukuliwa hatua zaidi.

“Waheshimiwa wabunge ndio maana huwa nasisitiza anapozungumza mmoja wetu kumsikiliza, Vuma ameonyesha kitendo ambacho mimi nimeshakitolea ufafanuzi, wakati amesema kitabu hiki kinapaswa kuchanwa. Vuma ameshaambiwa afute hayo maneno,” amesema Dk Tulia ambaye kabla hajamaliza wabunge wa upinzani walitaka achukue hatua zaidi.

“Naomba mtoke nje maana hatuelewani. Matiko na Heche namba mtoke nje. Matiko simama uende nje,” amesema Dk Tulia.

Dk Sware aliposimama na kutaka kutoa taarifa naye alitakiwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Wabunge hao hawakutoka hivi hivi kwani ililazimika kutolewa na askari wa Bunge waliolazimika kutumia nguvu kumtoa Heche ambaye alikuwa amegoma.
Kigoma kuna wabunge washamba sana......sasa unachana kitabu cha hotuba kwani kimekusea nini?

Kama kweli ana hasira angeenda kumvaa aliyekiandika kama asingerudi na manundu huku analia.....chezea Silinde wewe!!
 
Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amewatoa nje ya ukumbi wa Bunge wabunge wa Chadema, Esther Matiko (Tarime Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Dk Emmaculate Sware (Viti maalum) kutokana na wabunge hao kutoridhishwa na uamuzi wa Dk Tulia dhidi ya mbunge wa Kasulu Vijijini (CCM), Augustine Vuma aliyechana kitabu cha hotuba mbadala ya bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni mwaka 2019/2020 wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni
Kwa niaba ya Wanyakyusa wote wa Tanzania Nachukua nafasi hii kuomba radhi sana jamii kwa yanayotendwa na Tulia Ackson bungeni na kwingineko
 
Sikuwahi kujua kama huyu bana mdogo Vuma ni mpumbavu kiasi hiki. Akina Serukamba hebu mfundisheni huyu bwana mdogo anawaabisha ninyi ambao mmeshaziona bajet za kambi ya upinzani kwa miaka zaidi ya kumi sasa na bado hamzichani licha ya kutokubaliana nazo
 
Back
Top Bottom