Wabunge CCM wataka Rais ahojiwe bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge CCM wataka Rais ahojiwe bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 7, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=2][​IMG]
  Rais wa Tanzania Mh Kikwete

  Na Mashaka Mgeta[/h]  7th July 2012


  Hali ya kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inatazamiwa kukumbwa na mtikisiko kutokana na kuwepo nia ya kumtaka Rais Jakaya Kikwete, ahojiwe bungeni.
  Taarifa za ndani zilizolifikia NIPASHE Jumamosi zinaeleza kuwa, hatua hiyo inatarajiwa kufanikishwa kupitia mabadiliko ya kanuni yatakayoamuru Rais wa nchi kuhojiwa na Bunge kupitia maswali ya papo kwa hapo, badala ya Waziri Mkuu kama ilivyo sasa.
  Wachunguzi wa mambo ya siasa wanaielezea hali hiyo kuwa huenda ikakumbwa na mtikisiko na malumbano ya kisheria kati ya makundi yanayounga mkono mfumo uliopo sasa na wale wanaomtaka Rais aulizwe maswali.

  Hadi kufikia sasa, imebainika kuwa hoja hiyo inatarajiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Ritta Enespher Kabati.
  Kabati amethibitisha azma hiyo lakini akapinga kwamba inatokana na shinikizo la kundi moja kati ya yanayopingana ndani ya CCM.
  “Mimi sina haja ya kupata shinikizo lolote, nina akili na uwezo wangu, ninatambua kwamba ninawatumikia wananchi wa Iringa hasa wanawake,” alisema katika mahojiano yake na NIPASHE Jumamosi.

  Kabati alisema nia ya kuwasilisha hoja hiyo inatokana na uchunguzi aliowahi kuufanya kwa nyakati tofauti na kubaini kwamba asili ya kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu ni Bunge la Uingereza ambapo Waziri Mkuu ana mamlaka ya kuwa Mtendaji Mkuu wa serikali, tofauti na ilivyo hapa nchini.

  “Ninavyouona mfumo huu, tunahitaji kufanya marekebisho ili badala ya Waziri Mkuu kuulizwa maswali ya papo kwa hapo, awe anakuja Rais wa nchi,” alisema.

  Kabati alisema mfumo uliopo sasa ambapo Waziri Mkuu anashindwa kutoa majawabu ya baadhi ya hoja za wabunge anazoulizwa, isipokuwa kuelekeza kwenye mamlaka ya Rais, kunatoa fursa ya kufanya mabadiliko hayo.

  “Kama unavyolifuatilia Bunge kuna wakati Waziri Mkuu anatoa majawabu yasiyowaridhisha wabunge, inafikia wakati anaonekana anadanganya na hata kufikia hatua ya kudhalilishwa kama ilivyowahi kutokea wakati Godless Lema alipokuwa Mbunge wa Arusha Mjini.
  Lema aliwahi kuliambia Bunge kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alilidanganya Bunge wakati akitoa majibu kuhusu mgogoro uliosababisha mauaji ya raia mjini Arusha, hali iliyosababisha kiti cha Spika kumpa siku saba kuthibitisha kabla ya kutolewa mwongozo.

  Hadi kufikia sasa, gazeti hili halijapata kumbukumbu zinazoonyesha kuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda ama wasaidizi wake walishatoa bungeni utetezi wa Lema kuhusu hoja hiyo.

  “Kwa hiyo ninaona kwamba kama Rais atakuwa anakuja kujibu maswali kila Alhamis, itasaidia kupunguza mkanganyiko na wakati mwingine kumfanya aonekane anadanganya,” Kabati alisema.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia NIPASHE Jumamosi, baadhi ya wabunge wa CCM wanaamini kuwa kukosekana kwa majibu ya uhakika na yale yanayotofautiana miongoni mwa mawaziri wa serikali hususani Waziri Mkuu, kunasababishwa na kukosekana kwa Rais kujibu hoja za wabunge kwa niaba ya serikali yake.

  Kabati alisema hivi sasa anaendelea na maandalizi ya hoja hiyo, akitarajia kuwashirikisha wanasheria na kutafuta kuungwa mkono na wabunge bila kujali tofauti za kiitikadi.
  Waziri wa Uchukuzi ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, Dk Harrison Mwakyembe, alisema hoja hiyo iliwahi kutolewa na Kabati, lakini kinachoonekana ni upungufu katika kuitafsiri Katiba ya nchi.

  Dk Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela(CCM) mkoani Mbeya, alisema kimsingi, Rais anagawana mamlaka ya utawala na Waziri Mkuu, ambapo pamoja na mambo mengine, (Waziri Mkuu) anakuwa Kiongozi wa shughuli za kiserikali.

  Pia Dk. Mwakyembe alisema mfumo unaotumika nchini upo kwa mujibu wa mfumo wa mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola ambayo Tanzania ni mwanachama wake.
  Kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, ibara za 52, 53 na 57 zinatoa uhalali wa Waziri Mkuu kuwa na mamlaka ya kiutendaji yenye hadhi sawa na Rais, hivyo kustahili jukumu la kuendelea kujibu maswali ya papo kwa hapo bungeni.

  Ikiwa hoja binafsi ya Kabati itawasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM na hatimaye bungeni, inatabiriwa na wachunguzi wa mambo ya siasa kwamba inaweza kuibua mjadala na kuzidisha mgawanyiko wa kifikra ndani ya chama hicho.

  KATIBA MPYA

  Wakati huo huo, Dk Mwakyembe alisema pamoja na mchakato wa kuandikwa Katiba Mpya, taifa linapaswa kurejea katika hali ya uwajibikaji utakaochochea tija kwa maendeleo ya nchi na ustawi wa wananchi.

  Alisema upatikanaji wa huduma muhimu za jamii kwa wananchi ni moja ya nyenzo muhimu zinazochochea nchi zilizoendelea, zikiwa na Katiba mbovu kuliko ya Tanzania, lakini zinakubalika pasipo kuwepo shinikizo la mabadiliko.
  “Kama watu wanapata huduma kama za afya, maji safi na salama, elimu bora na nyinginezo kupewa kipaumbele, hakuna raia atakefikiria kudai Katiba, kwa maana mfumo unaoistawisha jamii ukifanya kazi, matatizo yote yanaondoka,” alisema.

  Alitoa mfano kuwa Katiba ya Marekani inatoa fursa kwa raia kuwachagua wawakilishi wanaoshiriki kumchagua Rais wa taifa hilo kubwa kiuchumi na kijeshi, lakini hakuna vuguvugu la mabadiliko yake (Katiba) kwa vile mfumo endelevu wa upatikanaji huduma za jamii unawanufaisha raia wake.
  Hata hivyo, alisema nia nzuri ya Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba inapaswa kuungwa mkono na kuihamasisha jamii ishiriki kutoa maoni yao.

  Dk Mwakyembe alisema maoni yanayopaswa kutolewa kwenye tume hiyo hayahusiani na uelewa wa Katiba, bali wananchi wayaelekeza mahitaji yao yanayostahili kutatuliwa kwa mujibu wa Katiba.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  .. ni kupoteza muda na kodi za walala hoi, wanashindwa kumuhoji waziri mkuu wataweza kumhoji rais, posho zimewalevya au.. ? taratibu cha chama chetu haziruhusu hilo rais ana kofia mbili Mwenyekiti wa Chama na Rais hilo wasahau halafu Rais si wa tanganyika peke yao na hilo sisi Zanzibar hatuliafiki maana mkimsulubu Kiwete mengi tulinanayo Zanzibar na kuwepo katika pipe line yatakufa, hilo hatutoliruhusu KUMBUKENI TUNA KURA YA VETO SASA, kwanza tujue lengo lenu nini kuumuliza kuwa nini ahsemi kitu kuhusu mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar au..? kabla ya yote kwanza leteni MoU Zanzibar tukubaliane hadidu za rejea katika utaratibu huo.
   
 3. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ugonjwa mwengine huo unakuja kwa Kikwete ikiwa alikuwa ana anguka anguka sasa naona atazimia kabisa, maana Serekali anayo iongoza imejaa Mswa. sizani kuwa Kikwete atakuwa na hoja kuwajibu Watanzania kutokana na uchafu uliokisiri wa Serekali yake?.

  Tunapoambiwa Watanzania kuwa serekali yetu imepiga hatuwa kubwa ya maendeleo nikweli, lakini hatua hio ni kwa vigogo kusomesha watoto wao nje na kutibiwa nje na kujilimbikizia rasilimali kwa jasho la Watanzania, huku Watanzania walio wengi wakishindwa kupata mlo wa siku.
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  naona mnataka ahame nchi kabisa
   
 5. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,100
  Likes Received: 11,250
  Trophy Points: 280
  muda wa kuhojiwa ukifika atatafuta safari ya gafla.
   
 6. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  dah jamaa anavyoogopa maswali..hiyo itakuwa ngumu!! isitoshe hana uwezo wa kujibu hoja nzito anaweza kuwa kituko tu pale mjengoni kwa kuachia kicheko tu kwenye serious issue:israel:
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Waambie wakatoe maoni yao kwenye Tume ya katiba, waache kuwa vizembwekela.
   
 8. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Wamfukuze kabisa nani Anamhitaji Raisi asiyejari Wananchi....

  Nasikia Riz1 Kesha anza biashara ya Mabasi ya Abiria Mikoani huu Jamaa Mjanja Sana Kaanza na Mabasi Kumi
   
 9. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,177
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  maswali ya kuulizwa ayajue pamoja na mulizaji ajulikane siku kadhaa kabla.
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,834
  Trophy Points: 280
  Kwa mpango huu akienda wingereza harudi naona mnataka kumuua!

  Mtu dhaifu alaf mnataka kumbebesha mzigo ambao hunaweza kumfanya aparalize
   
 11. k

  kibugumo JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  mnataka azidishe ziara za nje ya nchi.Mwacheni jamani baba yetu hapendi maswali.
   
 12. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Yanaitwaje mabasi hayo mkuu tuyafanyie subbotage njiani humo au kwenye yard
   
 13. Third Eye

  Third Eye JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Huwa siipend ccm, but kwa hili Rita Kabati kabehave kama jembe haswaa, anataka kumsulubu Vasco wa watu
   
 14. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Mawazo yako peleka Baraza la Mchamba wima kule.
  Hoja hizi tuachie waTanganyika, na jaribu kuzoea kwenu.
   
Loading...