Wabunge CCM wamuunga mkono Mbatia

Olaigwanani lang

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
541
175
Wabunge kadhaa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameunga mkonohoja ya Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), kuhusuudhaifu uliopo katika sekta ya elimu.

Miongoni mwa wabunge hao ni wanaomiliki na kuendesha shule binafsi zachekechea, msingi, sekondari na vyuo katika maeneo tofauti nchini.

Hata hivyo, wabunge hao, wakizungumza kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki,hawakutaka majina yao yatajwe gazetini.

Mmoja wa wabunge kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa Viktoria, alisema hoja ya Mbatiakuhusu udhaifu huo ina mashiko na kwamba jitihada mahususi zinapaswakuchukuliwa ili kuinusuru sekta hiyo nchini.

“Mimi ninaungana na Mbatia kwa asilimia mia moja, lakini ni vigumu kuyasemahaya bungeni kutokana na misimamo ya kichama,” alisema.

Mbunge mwingine kutoka nyanda za juu kusini, alisema maboresho ya sekta yaelimu nchini, yatafanikiwa ikiwa kutafanyika mageuzi ya kiuongozi katika Wizaraya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake.

Mbunge huyo alitoa mfano kuwa, katika kikao cha wabunge wa CCM kilichoongozwana Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta wiki iliyopita, Waziri wa Elimu naMafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alidhihirisha kushindwa wajibu wake.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo, Dk. Kawambwa, aliulizwa kuhusu sababu ya kuwapomgawanyo usiolingana kwa fedha za ukarabati wa shule za sekondari ambapo mkoawa Kilimanjaro umependelewa, alijibu hajui.

“Aliulizwe kwenye kamati ya wabunge wa CCM, kwa nini Kilimanjaro ilipewa shulenyingi za kukarabatiwa wakati maeneo kama Kongwa kwa Naibu Spika (Job Ndugai)na Mchinga inayowakilishwa bungeni na Said Mtanda wana shule mbili kila mahali,akasema hajui,” alisema.

Mbunge huyo, akiwa miongoni mwa baadhi waliohojiwa na kuwa na fikra kama hiyo,alisema si sahihi kwa serikali ama chama tawala (CCM), kupuuzia ama kupindishaukweli kuhusu hoja za msingi zinazowasilishwa na upinzani bungeni.

Mbatia, akizungumzia hoja hiyo, alisema kitendo cha wabunge wa CCM kupingamapendekezo mema aliyoyawasilisha kuhusu udhaifu unaoikabili sekta ya elimu,kinaashiria kutoitakia mema nchi na raia wake.


CHANZO:NIPASHE
 
Sasa kama alikuwa hajui walitaka awadangaye? Waziri mwenye dhamana amekuwa mkweli kwamba hajui. Hapa alimaanisha kuwa hakuwauliza maafisa wake waliochagua hizo shule. Kwa kawaida alitakiwa awe amewasiliana na wakurugenzi wa Idara ya Elimu ya Sekondari na yule wa Mipango pamoja Elimu TAMISEMI. Kwa kuwa hakuwa amefanya ndiyo maana alikuwa makweli kwamba hajui. Hao wabunge ni wanafiki waliopitiliza. Wanasema kwa ajili ya Chama? Kwani wako bungeni kwa ajili ya chama kwanza au wananchi wao kwanza? Waseme kwanza walipokwenda ukumbi wa Msekwa wakati wa party caucas waliambiwa nini?
 
Back
Top Bottom