Wabunge CCM wamtaka Rais Kikwete Dodoma; wasema wamechoshwa na mawairi wanaolala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge CCM wamtaka Rais Kikwete Dodoma; wasema wamechoshwa na mawairi wanaolala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 5, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Friday, 05 August 2011 08:31 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  WASEMA WAMECHOSHWA NA MAWAZIRI ‘ WANAOLALA’ ,PINDA ANUSURU BAJETI YA UCHUKUZI

  Mussa Juma, Dodoma

  BAADA ya kuitoa jasho Serikali katika mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, wabunge wa CCM sasa wanataka kukutana haraka iwezekavyo na Rais Jakaya Kikwete ili waweze kuweka wazi jinsi walivyopoteza imani na baadhi ya mawaziri na watendaji wengine serikalini.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao cha kamati ya wabunge wa CCM ambacho kilifanyika jana mchana, wabunge hao walieleza wazi kutoridhishwa na utendaji wa Serikali.

  Kikao hicho pamoja na mambo mengine kililenga kuwabembeleza wabunge wa CCM kupitisha bajeti ya Wizara ya Uchukuzi.

  Katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mmoja wa wabunge hao aliliambia Mwananchi kuwa wabunge waliozungumza walionesha kupoteza imani na baadhi ya watendaji wa Serikali hasa mawaziri ambao baadhi “wamekuwa wakilala bungeni”.

  Kwa mujibu wa habari hizo, mbunge wa Longido, Lekule Lazier ndiye aliibuka hoja ya kumuomba Waziri Mkuu, kumweleza Rais Kikwete kuwa wanamuomba afike Dodoma wazungumze kwa maelezo kwamba mambo sio shwari kwa wasaidizi wake.

  Hoja hiyo ya Lekule iliongezwa nguvu na hoja la Naibu Spika, Job Ndugai ambaye alionyesha wasiwasi kuhusu uadilifu wa baadhi ya watendaji serikalini, kutokana na tabia yao ya kuvujisha siri za Serikali kwa wabunge wa upinzani.

  Katika kikao hicho, ilielezwa kuwa wabunge hao, waliombwa kusaidia Serikali kupitisha bajeti hiyo kwani kutofanya hivyo ni kuwaongezea nguvu wapinzani bungeni.

  Wabunge ambao walizungumzia hoja hiyo ni pamoja na mbunge mkongwe, Anna Abdalah, ambaye amekuwa mtetezi mkubwa wa CCM ndani na nje ya Bunge.

  Abdalah pamoja na wabunge wengine, waliwasihi wabunge wenzao hasa vijana kuwa wavumilivu kwa Serikali ya CCM ambayo inajitahidi kufanya kazi kubwa ya kusaidia, lakini ukata bado ni tatizo.

  Habari toka katika kikao hicho, zinaeleza jitihada za Naibu Waziri wa Ajira na Kazi, Makongoro Mahanga kutaka kumtetea, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi kuhusiana na tuhuma za kuuza kinyemela Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) katika kikao hicho zilikwama.

  “Mheshimiwa Makongoro, aliinuka na kuzungumza kamtetea Dk Masubiri bila mafanikio,”alieleza mtoa habari huyo.

  Kikao hicho cha wabunge wa CCM, kilitanguliwa na kikao kingine cha juzi usiku cha baadhi ya wabunge wa CCM ambao walichangia bajeti na kusisitiza kuwa hawataipisha.

  Mmoja wa wabunge hao wa CCM alifafanua kuwa, walishangazwa kuitwa kwa Waziri Mkuu, muda mfupi baada ya Bunge kuahirishwa na kuahidiwa kuwa Serikali itatoa fedha zaidi kwa bajeti hiyo.

  “Sasa kama kulikuwa na fedha zaidi ni kwanini walituletea bajeti ndogo kiasi kile na hizo Sh95 bilioni zilipatikana wapi harakaharaka…hili tunadhani ni tatizo la watendaji wetu wa serikali,”alisema Mbunge huyo.

  Alisema kwa mazingira hayo, wamebaini kuwepo kwa upungufu mwingi katika utendaji wa Serikali na kwamba hali hiyo inatokana na uzembe wa baadhi ya mawaziri na watendaji wengine.

  “Sasa wametuomba tupitishe hii bajeti sisi kama wabunge wa CCM tumekubali, lakini kwa kutoa angalizo kuwa lazima sasa watendaji wa Serikali wafanye kazi kwa uadilifu na kutokiangamiza chama,”alisema Mbunge huyo.

  Bajeti yapita
  Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi ilipitishwa jana baada ya kuwepo mjadala mkali huku wabunge wa CCM na wale wa upinzani bila kujali itikadi zao kutamka wazi kuwa hawaungi mkono bajeti hiyo.

  Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu aliwachekesha wabunge wakati akihitimisha hoja hiyo alipotamka kwa sauti "Mheshimiwa Spika" mathalani ya ile inayotolewa na mpambe wa Bunge pindi vinapoanza au kufungwa vikao vya Bunge.

  Alipoona wamecheka sana akarudia ''Mheshimiwa mwenyekiti", wakacheka zaidi na ndipo alipohitimisha hoja yake kwa kutamka vyema kwa kuanza na "Mheshimiwa Spika''

  Awali akiwasilisha bajeti hiyo aliliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha Sh 237.5 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na mipango mbalimbali ya wizara hiyo.

  Pinda amwokoa Nundu
  Mapema jana asubuhi, Pinda aliwasilisha taarifa ya Serikali ya kuongezea wizara hiyo kiasi cha Sh95 bilioni ili iweze kuendeleza miradi ya Reli ya Kati, kufufua shirika la Taifa la Ndege (ATCL) na ununuzi wa Meli.

  Pinda alitoa taarifa hiyo ya Serikali jana , baada ya Spika Anne Makinda kutoa ufafanuzi kuwa, Waziri Mkuu anaweza kutumia kipindi cha maswali na majibu kutoa taarifa ya Serikali kwa dakika zisizozidi 15 na baadaye kipindi cha maswali kuendelea.

  Akisoma taarifa hiyo, Waziri Mkuu alisema baada ya kusikiliza maoni ya wabunge, juzi jioni Serikali ilikutana na kuona kuna haja ya kuoingezea fedha wizara hiyo.

  “Yaliyojitokeza yalionesha uzito..michango ilikuwa ni mizuri na ninawashukuru, Rais Kikwete aliamua kuunda wizara hii pamoja na wizara ya ujenzi kutoka wizara ya miundombinu kutokana na uzito wa wizara hizi,”alisema.

  Alisema sekta ya uchukuzi inahitaji mitaji mikubwa ili kufanikisha miradi ya Reli, Ndege na mingineyo hivyo ina mahitaji makubwa, lakini pia bajeti haitoshelezi.

  “Jana Serikali ilikutana kutazama uwezekano wa kuongeza bajeti.. sasa tumeridhia na tumekubali zitaongezewa Sh95 bilioni ambazo zinaweza kutumika katika kusaidia Reli ya Kati, ATCL na ununuzi wa Meli katika maziwa Tanganyika, Nyasa na Ziwa Victoria,”alisema Pinda.

  Juzi idadi kubwa ya wabunge, walitamka wazi kuwa kama wizara hiyo, isipoongezewa fedha hawatapitisha bajeti hiyo, huku wakitaka Reli ya Kati na ATCL kupewa kipaumbele.

  Vigogo wa UDA kuchunguzwa
  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imewaagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuanza uchunguzi juu ya kuuzwa kwa UDA.

  Pinda alisema uchunguzi huo utafanyika sambamba na ule utakaofanywa na Kamati Ndogo ya Bunge ya Miundombinu na kwamba Serikali itatoa ushirikiano ili kazi hiyo iweze kukamilika haraka.

  “Baada ya uchunguzi kukamilika Serikali itachukuwa hatua za kisheria kwa wahusika wote,”alisema Pinda.

  Juzi wabunge walishauri kukamatwa mara moja kwa watuhumiwa wote sakata hilo wakiwamo, Meya wa Jiji, Dk Didas Masaburi, aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya UDA, Idd Simba na Mbunge wa Urambo Magharibi, Juma Kapuya kwa madai kwamba ni wahusika wakuu wa kuuza mali za shirika hilo kwa Kampuni ya Simon Group Ltd ambayo inaaminika mwanahisa mmoja wao ni mtoto wa kigogo nchini.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wameanza kuona hatari ya kutokurudi bungeni mwaka 2015,hali ni mbaya kwa magamba.peoplez power
   
 3. T

  Technology JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Makongoro alikua anamtetea kitu gani Mayor was DSM? hebu fafanua kidogo mtao mada
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mkuu unanichosha na habari zako za magazeti

  copy and paste

  Uwe unafanya analysis kidogo
   
 5. M

  Michelle Hilton Senior Member

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  A reform
   
 6. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  haina mashiko mada yako! CCM tunawajua kwa kunusuru bajeti, lakini hawana pa kutokea 2015!
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  What kind of Analytical research should be done? Would U like me just spread the rumor? I'm transparent I cannot say something just to please your analytical mind!!!

  It is an Article and Jamii Forum is a Free Place to express your View and not alwyas giving bogus analytical research; ending up the issue being not true... make this Place a BUGUS FORUM like the old ones which ha failed!!!
   
 8. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  We do not need the analytical research, gaash you got me wrong
  You need to come up with the analysis of the article as great thinker no copy and paste
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  R U Serious I did not see on the Article? Ndio matatizo ya sisi Watanzania tunataka kila kitu kiwe Mezani, as long as is food you eat and forget to know about how that plate was on that table...
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  That's why we R in the FORUM everyone of US view this Article in a different prospective... and that's why JF is rich with people of different characters and views... Not just to bring what other's wanted to see and please such as U... and I stand by my way No one can take away my freedom of expressions... I'm FREE BROTHER/SISTER!!!
   
 11. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ukiwa na raw data ndio unaweza kufanya analyisis hii inaeleweka.
   
 12. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  Haikufaa rangi itaweza chokaa?!
   
 13. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ina maana jamani kumbe issue ni ukata kwenye serikali? Guys we are being fooled so that budget sails through but the matter of fact there is no cash to implement them! CDM must get this and counter it professionally.
   
 14. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukishakuwa na watendaji (makatibu wakuu) kama akina Omari Chambo, Jairo unategemea nini? Hawana vision, hawapo creative wanasubiri 10% ndipo waiaprove miradi, wawekezaji obviously watakimbia!
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Rais Kikwete alikuwa Dodoma only a week ago kuongoza vikao vya cc, kwa nini hawakumuona?
   
 16. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Sipati picha siku Si Si Em ikiondoka madarakani,
  Nadhani Tanzania itakuwa na wakiimbizi wengi sana wa kisiasa nje ya nchi.
   
 17. T

  Testimony Senior Member

  #17
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kitu kimoja kilicho wazi sasa kwa wabunge wa ccm na wengineo ni kuwa party partisan haitawarudisha bungeni. wasipofanya wattegemewacho kufanya na wapiga kura zao, wawe wa ccm au kwingineko hawatarudi bungeni asilani. hii itaboresha uimara wa taasisi iitwayo bunge na labda, inshallah, itainusuru nchi na nguvu nyingi wajionazo kuwa nazo watawala!
   
 18. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Yeah hao wakimbizi wa kisiasa watadhani pesa zilizoko Mabenki nje ya Nchi yataendelea kuwatukuza... waambie waanze kuuliza Jamaa za Mobutu, Sanni Abacha, Hosni Mubarak, Ben Ali wanaishije sasa?

  Majumba na Pesa zote zimeshikiliwa... Waaache sasa hivi wacheze hizo ngoma za Mduara, kudhalilisha Mwananchi wa Tanganyika...
  Hizo nchi zenyewe zitawaomba waondoke ila Saud Arabia na South Africa zitawapokea...

  Saud Arabia itawaambia hakuna masihara hapa ni DINI 101, kwahiyo UFISADI 0 wamuulize Ben Ali na Idd Amin family hakuna mchezo huko

  South Africa watawaambia wakae ndani tu hawaruhusiwi kuzurura... wamuulize Rais Tapeli wa Haiti - Jean Bertand Aristide
   
 19. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Issue kubwa zinoisibu bajeti yetu ni makusanyo hafifu ya TRA, na vipau mbele vya mashaka katika matumizi ya serikali.
   
 20. D

  DONALD MGANGA Member

  #20
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Navyomjua Ndugu JK na hoja hii atafunja Baraza la Mawaziri na Mzee white hair atarudi kwa style ya aina yake maana miaka mitano ndo imepita toka ajivue gamba bila kosa na hapo ndipo mtaona kila kitu kwenye machoya watu. Rudi Lowassa uokoe jahazi mkuu amalize vizuri.
   
Loading...