Wabunge CCM waichoka serikali ya Rais Kikwete; Anna Abdallah, Kilango waishambulia bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge CCM waichoka serikali ya Rais Kikwete; Anna Abdallah, Kilango waishambulia bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 27, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  • Anna Abdallah, Kilango waishambulia bungeni

  na Tamali Vullu, Dodoma

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  WABUNGE wa Chama cha Mapinduzi (CCM) juzi na jana waliicharukia serikali na watendaji wake kutokana na ufisadi unaodaiwa kufanywa katika sekta ya kilimo, huku wakulima nchini wakiendelea kukandamizwa.

  Wakichangia hotuba ya bajeti ya makadirio ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, baadhi ya wabunge wa CCM walitaka utendaji kazi unaofanywa na serikali ubadilike haraka, ili wananchi waweze kupata maendeleo.

  Katika mjadala huo wa juzi jioni, wabunge hao walisema kinachoiangusha serikali ya CCM ni watendaji wake kutokana na kuibua miradi ambayo haitekelezeki.

  Mjadala huo ambao ulitekwa na wabunge hao wa CCM, ulivuta hisia za wabunge wengine kutokana na hoja zilizotolewa na wachangiaji kulenga katika utatuzi wa matatizo ya wakulima nchini.

  Wa kwanza kuchangia mjadala huo alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Abdallah (CCM), ambaye aliwasha moto kwa kuhoji mambo mbalimbali yanayokwaza kilimo cha korosho, ikiwemo mbolea inayopatikana kwa njia za magendo kutokana serikali kuacha kuwasaidia wakulima.

  Alisema hakuna pembejeo za zao hilo kwa mikoa yote inayolima korosho, suala ambalo limesababisha mfuko mmoja wa mbolea aina ya ‘sulphur’ kuuzwa sh 50,000.

  “Bodi ya Korosho ilimaliza muda wake tangu mwaka 2005, ni nani anayesimamia suala la korosho? Korosho inasimamiwa na nani? Nani mmemuachia mambo ya korosho?” alihoji mbunge huyo.

  Alihoji kama utendaji huo wa wizara unazingatia mazingira ya utawala bora ambao umekuwa ukihubiriwa na viongozi wa juu wa kitaifa.


  Mbunge huyo alisema kutokana na kumaliza muda wake, amekuwa akisikia wajumbe wa bodi hiyo huitwa kujadili mambo yanayojitokeza, wakati uhalali wao umepitwa na wakati.

  “Nasikia hata baadhi ya wajumbe wa bodi mkiwaita wanakataa, tunataka mtuambie hizi fedha za Bodi ya Korosho na zile mnazotenga mnazipeleka wapi? Mnafanya hivi kwa fedha za korosho?

  “Wabunge wote 11 wa Mtwara hatujui. Hicho kikao cha RCC ni wadau gani waliitwa? Mlipata wapi ruhusa ya kufanya hivyo?” alihoji.

  Aliomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aitwe akague matumizi ya fedha hizo kutokana na kuwepo kwa uwezekano kuwa zilitumiwa vibaya.

  “Hivi ni serikali hii ya CCM? Naomba kupatiwa majibu mazuri vinginevyo hapa hapatatosha. Siungi mkono hoja na nasikitika kwa mara ya kwanza naipinga serikali yangu,” alisema Mama Anna Abdallah.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, alisema adui mkubwa wa CCM ni watendaji wao kutokana na kuleta mipango isiyotekelezeka.

  Alisema ni kwa nini watendaji ndani ya wizara hiyo hawaleti mabadiliko na kusema kuwa njaa haina adabu, wasishangae siku moja kuona wananchi wamekwenda bungeni.
  “Mnataka kutuua? Mbona hamfanyi mabadiliko katika sekta hii. Hatutaki porojo. Tanzania ni nchi ambayo hata Mungu anaishangaa kwani ikinyesha mvua ni janga, ukame ni janga.
  “Hivi hata kuiga mnashindwa? Rais alipokwenda Malaysia nilimuona anaomba Business Card, hivi hao wataalamu anaokwenda nao wanafanya nini? Si bora wasiende?” alihoji mbunge huyo.

  Alisema hata mabwawa yaliyojengwa enzi ya uongozi
  wa Mwalimu Nyerere, serikali imeshindwa hata kuyafufua.

  Lusinde alisema kulima si suala la mchezo, kwani mazao yanapatikana kwa tabu na kuhoji iwapo wabunge wataamua kuanzisha shamba lao kama wataweza kuliendeleza.

  “Tuanzishe shamba la Bunge kama hatujaliacha. Kulima si mchezo na mazao yanapatikana kwa taabu, lazima tuwaenzi wakulima kwa kuwapatia bei nzuri,” alisema.

  Alisema wizara hiyo ndiyo ambayo wabunge wanapaswa kuitolea macho, kuliko Wizara ya Nishati na Madini na kuongeza kuwa katika suala la umeme ni ubinafsi wa wabunge kuogopa nyama kuoza kwenye mafriji.
  “Tunakuwa kama tumelogwa? Tutakataa kupitisha bajeti zote, potelea mbali tusirudi kwenye uchaguzi. Hawa wataalamu wanafanya kazi gani, wanaleta vitu ambavyo havitekelezeki!” alishangaa.

  Pamoja na hayo, mbunge huyo alihoji inakuwaje wakati wa uchaguzi maboksi ya kupiga kura yanaweza kufika katika kila kijiji, lakini linapokuja suala la wakulima kupelekewa mbolea linafika kwenye vijiji vichache.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), alisema mfumo uliowekwa na serikali wa kugawa pembejeo za kilimo kwa wakulima kwa njia ya vocha ni moja ya njia za kuwapelekea watu biashara za kuwanufaisha.
  “Mimi na serikali hapa ndiyo tunapishana, hamuwezi kutoa kitu kizuri namna hii halafu baadaye mshindwe kufuatilia. Hapa mmewapa watu biashara za kujinufaisha kupitia pembejeo za kilimo,” alisema Kilango.

  Akizungumzia serikali kuwazuia wakulima kuuza mazao nje ya nchi, alisema si haki kuwakataza wananchi kuuza mazao yao.
  Kilango alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali ndiyo ina jukumu la kuwajibika kwa wananchi wake, lakini serikali ya CCM haifanyi hivyo.

  “Nimesikitishwa na hatua ya waziri ya kufunga mipaka ya kuuza mazao ya chakula eti kuepuka taifa kukumbwa na baa la njaa, hapa sijafurahishwa hata kidogo na sijapapenda kabisa.

  “Anafunga milango kwa wakulima kuuza mazao yao, halafu juzi kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, waziri amezikaribisha nchi zinazokabiliwa na njaa zije zizungumze na serikali ili iziuzie mazao ya chakula.

  “Hivi ni lini mmeingia kwenye biashara, hicho chakula
  mmekilima ninyi? Tafuteni utaratibu mwingine na si kuwakandamiza wakulima wasiuze chakula nje, hili nalikataa kabisa.

  “Hili nalikataa kwa sababu serikali haijafuata Katiba, kwa nini yenyewe iuze nje halafu wakulima iwafungie milango? Waacheni wauze ili na wao wanunue VX. Bei yenu mnayotaka kununulia kwa wakulima iko nchini, hivyo wakulima hamuwatendei haki, nikiunga mkono hoja hii nitakuwa mtu wa ajabu,” alisema Kilango.

  Akiendelea kuzungumza, Kilango alisema wananchi wa Same wamejitolea kujenga kiwanda cha kusindika tangawizi, lakini akashangazwa na hatua ya serikali kutowaunga mkono.
  “Kule Tanga machungwa na matunda mengine yanaoza, wananchi wa Same wamejitolea kujenga kiwanda chao wao wenyewe lakini jambo la kushangaza ni kwa serikali kushindwa kuwaongezea nguvu.

  “Hata wanaojitahidi mnakataa kuwasaidia, Katiba inasema serikali itawajibika kwa wananchi wake. Mnaona uzito gani kuwasaidia wananchi waliojitahidi? Nakushukuru Waziri Mkuu ulituchangia sh milioni 10, nashukuru sana,” alisema.
  Aliitaka serikali kujenga barabara ili wakulima wa tangawizi waweze kutoa mazao yao shambani na kupeleka kwenye kiwanda hicho kwa ajili ya kusindikwa.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Kessy Mohammed, akizungumzia utaratibu wa vocha za ruzuku kwa wakulima, alisema utaratibu huo umegubikwa na ufisadi na kuufananisha na EPA nyingine kwa madai kuwa wao kama wabunge wa Rukwa hawazitaki kwa vile usimamizi wake ni mbaya.

  “Hizi vocha za ruzuku ni balaa, ni EPA nyingine. Tumeshasema sana kuwa hazifai, kule kwetu mpaka maiti wameandikwa,” alisema.

  Aidha, alisema walishakataa matrekta ya Power Tiller, lakini anamshangaa Waziri Maghembe kuweka picha ya Rais akiwa ameipanda na kusema kuwa kitendo hicho ni cha udhalilishaji.

  “Tulishakataa Power Tiller, lakini katika kitabu cha waziri ameweka picha ya Rais akiwa ameipanda. Huu ni udhalilishaji. Kwanza atueleze hii kampuni ya Power Tiller ni ya nani?” alisema.

  Kessy alihoji kampuni inayouza matrekta madogo aina ya Power Tillers na kutaka apewe maelezo ya mmiliki wake, kwa madai kuwa uwezo wa vitendea kazi hivyo ni mdogo na haviwezi kuhimili ardhi ngumu.

  Pamoja na hayo alisema huu ni mwaka wa neema kwa wakilima wa mahindi, lakini Waziri Maghembe anaonekana kutowaonea huruma wakulima hao kutokana na kuwafungia mipaka ya kuuza mazao yao.
  “Hivi hii ni kasi mpya na bora? Hii ni balaa. Hivi serikali inakwenda wapi? Mnafunga mipaka kwa wakulima halafu mnasema Kilimo Kwanza, mimi nasema ni Kilimo Mwisho.
  “Yale mahindi yakioza waziri utayanunua au kulipa fidia? Unawalazimisha wakulima wayaweke hadi Januari, nakwambia yakioza utayanunua.

  “Na sintokubali kuiunga mkono hoja wala kutoa shilingi kwa kuwa mtanishinda kwa kura. Hiki si kilimo kwanza bali kilimo mwisho, wakulima wananyanyaswa hawana sehemu za kuuzia mazao yao wala kuyahifadhi, serikali hii ni balaa tupu,” alisema na kumtaka Waziri Maghembe kutangaza bei ya mahindi.

  Naye Mbunge wa Viti Maalum, Zainab Vullu, alisema suala la kilimo limekuwa likipewa misamiati mingi toka ‘kilimo cha kufa na kupona’ hadi ‘kilimo kwanza’, lakini hakuna mafanikio yanayoonekana kutokana na bajeti yake kupungua mwaka hadi mwaka.
  Aliishauri serikali kulitumia bonde lenye hekta 2,000 lililoko wilayani Bagamoyo, kwa ajili ya kuzalisha chakula, kwani mpaka sasa ni hekta 100 ndizo zinazotumika.
  “Kwa nini tulie njaa Tanzania? Kwa nini hatutumii wataalamu wetu. Katika bonde lile zikitumika hekta zote tunaweza kuondokana na tatizo la njaa nchini,” alisema.
  Alisema mpaka sasa wakulima wa korosho hawajapata mbolea ya kunyunyizia (sulphur) na kumtaka waziri kumweleza wakulima hao wataipata lini mbolea hiyo.

  Akizungumzia zao la nazi, alisema waziri huyo hakulizungumzia mahala popote na kuhoji iwapo zao hilo halitambuliki na kwamba halipo tena.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Kwela, Ignas Malocha (CCM), alisema kitendo cha serikali kuwazuia wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi ni cha uonevu.
  Alisema kitendo hicho hujenga chuki na wakulima na kuhoji iwapo serikali inataka wakulima nao kuandamana.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Du nchi hii kazi ipo!mimi nilichopenda ni hapo tu kwenye kuuza mazao nje ya nchi!ukienda Tarekea kuna foleni ya malori yanapeleka mahindi Kenya!wao wanasema wamezuia!kumbe ndio wanawatajirisha askari na maofisa wa mpakani!
   
 3. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hapa CCM umeamka ila bado Mawaziri hawaelewi
   
 4. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Hawa wachache wanye uchungu na nchi hii lazima wafukuzwe tu!Wataonekana hawana nidham na wanakivua nguo chama,ukiwa humo hautakiwi kukisema chama vibaya hata kama kinakwenda kinyume!
   
 5. W

  We know next JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nilisha sema ktk thread yangu jana, kuwa utendaji wa baadhi ya watumishi serikalini, kwa kweli inatia kinyaa. Ona sasa mambo ya Kilimo hayo.... TUMECHOKA, Rais chukua hatua kabla wananchi hawajachukua hatua.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ni kawaida au niseme mara nyingi mtoto anapofanya kosa basi mzazi wake hujulishwa ili achukuwe hatua haraka za kumrekebisha. Sasa hivi baraza mawaziri wetu na watendaji wengi serikalini wanafanya watakavyo kwa sababu hakuna wa kuwakemea! Siku chache zilizopita Mizengo Pinda amedhihirisha hilo pale aliposhindwa kuchukua hatua yoyote dhidi ya Jairo kwa madai kuwa liko nje wa mamlaka yake na hivyo alikuwa anawasiliana na Rais. less than 24 hours later Katibu mkuu kiongozi anamsimamisha kazi Jairo na kusema 'hili liko ndani ya uwezo wangu'.

  Niliuliza umuhimu wa kuwa na Waziri mkuu kwenye thread nyingine na sasa nauliza tena, kama Katibu mkuu kiongozi ana uwezo kimamlaka na ki-uthubutu katika utekelezaji kwa nini tunapoteza kodi kumuweka Waziri Mkuu? Kule Bungeni Pinda amefanya kazi moja tu ya kuwanyamazisha wabunge wa ccm-kupita kifimbo (chief whip) lakini wabunge wa ccm wamegundua hii tabia ya 'ndiyoooo' inawamaliza kisiasa na sasa wanaanza kwenda kinyume (japo wamechelewa).

  Hivi Sokoine angekuwepo sasa nini kingetokea?
   
Loading...