Wabunge CCM waagizwa kuitetea bajeti kufa na kupona | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge CCM waagizwa kuitetea bajeti kufa na kupona

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CHASHA FARMING, Jun 12, 2011.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  Jun 12, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Ally Mkoreha, Dodoma
  WAKATI mjadala kuhusu bajeti ya serikali katika mwaka wa fedha wa 2011/12, ukitarajiwa kuwa mkali ndani ya Bunge, kufuatia hatua ya awali ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kupinga bajeti hiyo kwa maelezo kuwa haikutoa unafuu wa maisha ya wananchi wa kawaida, wabunge wa CCM wamesema wamejipanga kuitetea kikamilifu.

  Habari zilisema wabunge wa chama hicho kinachoongoza serikali, walikutana juzi katika kikao cha kamati yao ambayo Mwenyekiti wake ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Katika mkutano huo wabunge hao waliweka mikakati jinsi ya kutetea bajeti hiyo, iliyowasilishwa bungeni Jumatano iliyopita na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo.

  Katika hotuba yake, Mkulo alisema bajeti hiyo imelenga kuwapunguzia wananchi, makali ya maisha na kwamba, ndiyo maana serikali imeondoa tozo mbalimbali za mafuta na kufuta kodi kwenye pembejeo za kilimo.
  Alisema kupanda kwa bei ya mafuta, ni moja ya mambo yaliyosababisha ugumu wa maisha miongoni mwa wananchi.

  Hata hivyo siku moja baada ya kuwasilishwa kwa bajeti hiyo, kambi ya upinzani kupitia kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, iliibuka na kuiponda kuwa ni bajeti hewa haikulenga kuwasaidia walalahoi kama ilivyoelezwa na serikali.

  Hatua hiyo ilisababisha Waziri Mkulo kuibuka mjini hapa na kuwaeleza waandishi wa habari kuwa, Zitto amepotosha umma kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

  Hali hiyo inaashiria kuwapo kwa mvutano kati ya wabunge wa CCM na wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inayoongozwa na Chadema katika mjadala kuhusu bajeti itakayojadiliwa kuanzia Juni 1 5 hadi 21, mwaka huu.

  Wakizungumza na Mwananchi jana kwa masharti ya kutotajwa, baadhi ya wabunge wa CCM walithibitisha habari kuhusu kuwapo kwa kikao cha kamati yao na kwamba, kilikuwa na lengo la kuweka msimamo wa pamoja kuhusu kutetea bajeti.

  "Ni kweli jana (juzi) tulikuwa na kikao cha Kamati ya Wabunge wote wa CCM, kuweka msimamo wa pamoja kutetea bajeti yetu. Tumejipanga vilivyo kuwakabili wapinzani wetu na tuna uhakika kwa kuwashinda katika mjadala huo kwa sababu bajeti yetu ni safi na wao wanaikubali ingawa kwa tabia yao, wanaipinga,” alisema mmoja wa wabunge hao.

  Lakini akizungumzia majigambo hayo ya wabunge wa CCM, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alisema: Wabunge wa CCM watashinda kwa kupiga meza na kuzomea, ni mabingwa katika hayo lakini siyo


  SOURCE MWANANCHI [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna haja kubwa kwa wabunge wa upinzani kutoa pingamizi kali kwa mchakato mzima wa kupitisha bajeti kwani unalifanya bunge hilo kuwa "rubber stamp;" hii inatokana na ukweli kwamba kulingana na ratiba ya kikao cha bunge linaloendelea hivi sasa, kuanzia kesho bunge linaanza kujadili hotuba ya bajeti; baada ya mjadala huo wabunge wanatarajiwa kupitisha makisio yaliyo hainishwa kwenye hotuba hiyo; baada ya hapo utawasirishwa muswada wakuidhinisha kuanza kutumika kwa bajeti hiyo {appropriatin bill). Muswada huo ukishapitishwa, kwa hali yeyote hile zoezi hilo la bajeti litakuwa limehitimishwa. Hata hivyo wabunge wataendelea kukaa huko Dodoma kwa miezi mingine miwili na nusu eti kujadili makisio ya wizara moja moja, zoezi ambalo halina mantiki yeyote isipokuwa ni kupoteza tu fedha za umma, kwani bunge hilo likisha pitisha bajeti katika ujumla wake haliwezi tena kufanya marekebisho yeyote katika makadirio ya wizara kwakuwa makisio ya wizara hizo yamejumlishwa katika makisio ya jumla ambalo bunge litakuwa tayari limeyapitisha. Kutokana na hali hiyo kuna haja kubwa ya kuhairisha kuridhia hotuba ya bajeti hadi baada ya kujadili madirio ya wizara moja moja.
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kitaeleweka vizuri 2015, maana hawakuchaguliwa na kamati ya bunge ya CCM bali umma. Sasa ole wao wasichambue kwa manufaa ya umma, waendelee kupitisha tu. Watakiona cha mtema kuni.:hatari:
   
 4. emmathy

  emmathy Senior Member

  #4
  Jun 12, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Je wabunge wanajadili hotuba wakiwa upande wa serikali au upande wa wananchi? Nadhani kuna haja yakuona uendeshaji wetu wamabunge badala yakuwa mawazo yajumla basi mawazo mbadala kwa mtu mmoja mmoja yapewe kipaumbele ili kuliokoa Taifa. Mjadala wabajeti uzingatie wananchi na si mwelekeo wa kivyama. Ipo siku nasisi wananchi tutakataa wawakilishi , halafu tujadili bajeti zetu kupitia vikao vyetu vijijini.
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Upuuzi wao waufanye huko huko bungeni na huko kwenye kamati yao! Wakija kwetu watajua kilichomtoa kanga manyoya. Niwakumbushe tu kwamba mawaziri wao walishawahi kutuletea ujinga kama huo wakaishia kuzomewa!
   
 6. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hii ndio kawaida yao....Hoja imepita NDIYOOOO!!!!!!!!!!!!!!! yaani hoja ikitoka kwa mbunge wa CCM hata iwe ya k****ge wao ni NDIYO
   
 7. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wachakachue wasichakachue by the time being wakija huku kwetu sasa ivi ni mawe mawe tu kudadadadeki nshachoka mie!!
   
 8. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kama wamejiandaa kutetea bajeti ya serikali bila kujali kama ina manufaa kwa taifa au laa ni upuuzi....Pia inadhihirisha ni jinsi gani hawako bungeni kwa maslahi ya wananchi,kwa mantiki hii hawana uhalali wa kuitwa wawakilishi wetu!Nasikitika mno kuwa kwenye jimbo linaloongozwa na mbunge toka ccm..!
   
 9. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hawa wabunge ni mzigo kwa taifa kama si umbumbumbu wanajipanga kuteteya uozo cdm ninawashauli wakitumia uwingi wao mkimaliza vikao anzeni opalesheni kuwashitaki kwa wapiga kura mijini-vijijini

  Kuwaeleza watz uozo wa wabunge wa ccm

  ccm acheni kufuata mkumbo hayo yakupiga makofi kwa kira jambo bira kuangalia madhara ya baadaye ndo yaliyotufikisha hapa hamtazalauliwa kwa kukubali ushauli wa upande wa pili kama unamanufa kwetu sisi hatuangalii rangi yapaka tunataka paka anae kamata panya msipo badilika ninaimani 2015 mliowengi hamtaingia tena mjengoni
   
 10. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hiyo inayoitwa bajeti itayompunguzia makali mwananchi imejaa aibu tupu, na kwa hili nashawishika kusema kweli CCm imefika mwisho wa kufikiri.
   
 11. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Wabongo kuandika tunajitahidi. Utekelezaji ndio F
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Baada ya kupitia hoja mbali mbali za vyama vya upinzani kuhusu bajeti, nimeona kuwa hawataki kuusema ukweli kwa wananchi kuhusiana na bajeti, basi hata kuugusia tu hawataki? Na hali wanaujuwa fika.

  Kuhusu vipaumbele vya Serikali kwenye bajeti wamekuwa wakilalamikia kuwa kiasi kikubwa cha fedha hakijatengwa kwa maendeleo. Hilo ni kweli kabisa. Jee, kwa nini? Mbona hawasemi kwa nini? kinawashinda nini kusema kwa nini na huo ndio ukweli na wanauficha kwa makusudi kabisa?

  Ukweli ni kwamba, Serikali siku nyingi sana ilishajitowa katika kuwekeza kwenye maendeleo kila inapowezekana, na imejikita katika kuelekeza "policy" wapi pawekweze kimaendeleo na sekta binafsi. Na hicho ndio sahihi. Serikali inawekeza pale tu ambapo haina budi kuwekeza.

  Sera za Serikali kuwa na mali ya Umma na kuendelea kuwekeza kwa wingi kwenye kujenga viwanda, mashule, vinu vya umeme, na mengineyo mengi, ilisha pitwa na wakati na sasa ni jukumu la wananchi na wenye mitaji kuwekeza kwenye maendeleo. Na hiyo ndio fursa kuu ya wananchi wanaotaka na wenye muono wa kujiendeleza.

  Kwa hayo, hakuna msingi wa kuelekeza fedha nyingi katika kuwekeza kwenye maendeleo bali fedha nyingi ni lazima ziende kwenye utawala kwani huko ndipo zinapohitajika zaidi. Kwa mfano tumeona wawekezaji wakija kuwekeza kwenye sekta ya umeme kwa fedha zao, Sasa kwa nini iwepo bajeti yake Serikalini wakati ni fedha za wawekezaji?

  Wanasiasa muwe wa kweli kwa haya na yanayofanana nayo.
   
 13. mwanapolo

  mwanapolo Senior Member

  #13
  Jun 12, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hoja yako inatia kinyaa kuisoma. Unasikia usingizi, nenda kalale
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Faiza Foxy,

  Tunalipa kodi ili serikali itufanyie kitu gani??? Pili unapozungumzia serikali imejikita katika policy unamaanisha nini hebu fafanua kwani policy inashirikisha shughuli za maendeleo sasa kama serikali imejitoa huko utaformulate vp policy au ndio unapayuka tu kwasababu ya unazi wa chama. Tatu umeme unaathari mpaka kwako wewe wasipowekeza katika umeme unataka wakawekeze wapi au ndio nyie washauri wa Kikwete mnaomshauri awekeze katika mkukuta policy ambazo they are unworkable pathetic and do not make any sense!!!!!

  Ni hayo tu kwa sasa naomba majibu.
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @FaizaFoxy
  1. Serikali siku nyingi sana ilishajitowa katika kuwekeza kwenye maendeleo - hili halina mjadala tunaliona waziwazi

  2. imejikita katika kuelekeza "policy" wapi pawekweze kimaendeleo na sekta binafsi - policy zipi?

  3. Serikali inawekeza pale tu ambapo haina budi kuwekeza - kama wapi ambapo haina budi kuwekeza? na matokeo ya uwekezaji huo wa lazima ni nini?

  4. Sera za Serikali kuwa na mali ya Umma na kuendelea kuwekeza kwa wingi kwenye kujenga viwanda, mashule, vinu vya umeme, na mengineyo mengi, ilisha pitwa na wakati - Na hii nayo iko kwenye hizo policies za serikali? Shule za kata zilijengwa kwa policy ipi? Na ilani ya ccm inasemaje?

  5. ni jukumu la wananchi na wenye mitaji kuwekeza kwenye maendeleo - tayari wananchi wanafanya hivyo, kupitia kodi.

  6. hakuna msingi wa kuelekeza fedha nyingi katika kuwekeza kwenye maendeleo bali fedha nyingi ni lazima ziende kwenye utawala kwani huko ndipo zinapohitajika zaidi - wanatawala kivipi? kwa kununua vitafunwa?

  7. tumeona wawekezaji wakija kuwekeza kwenye sekta ya umeme kwa fedha zao - hela zimetolewa na Federal Government (USA) kupitia mfuko wa Milenia.

  Mwisho naomba usome hii orodha hapa chini uniambie kama nazo ni policy. Kama sio policy naomba useme waziwazi hii orodha inaitwaje? Na ni nani anatakiwa kuitekeleza?

  1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36.Kulinda haki za walemavu - Makete
  37.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43.Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58.Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Eti kaka unangojea jibu toka kwa huyu mtu hapo juu ?
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani atakuwa anachuwa notes - Mt wa Lumumba!
   
 18. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Ni nadharia tu kufikiri kwamba nchi hazijihusishi (hazitakiwi kujihusisha) na masuala ya makampuni, viwanda n.k. Ukweli ni kwamba serikali zote duniani zinajihusisha directly au indirectly kwenye ujenzi wa sekta mbalimbali.
  Mfano,USA ilipoingilia kati mgogoro kati ya serikali ya china na google. Hapa ilikuwa ni kulinda maslahi ya wamarekani wanaofanya kazi google na hivyo kuchangia ktk uchumi.Pili, mabalozi wa USA hawaji kuuza sura huku, kama tulivyoona ktk sakata la kununua ndege za ATCL. Wana-lobby kwa ajili ya makampuni yao-ambayo sio ya serkali.Hii mifano 2 kutoka nchi ya kibepari inayoamini ktk free market itoshe kuonyesha kwamba kuna sekta ambazo serikali (iwe ya kijamaa au kibepari) lazima ziwekeze directly or indirectly. Mama clinton hajaja kuuza face, amekuja kufanya biashara na akirudi ataelezea mafanikio ya ziara yake
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Imekugusa pazuri, husemi kweli?
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280

  Unapolipa kodi, inatakiwa kodi iende panapostahiki, lakini isiende kujenga kiwanda cha Umma ambacho kinajulikana wazi kuwa kitakufa, kwani vilikuwepo na vimekufa.

  Serikali inatakiwa ijikite katika kuhakikisha vipa umbele vinavyotakiwa vinaweza kuwekezwa na wananchi na wenye mitaji, mfano: Kilimo kwanza, serikali inahakikisha inasimamimia vipi pembejeo zipatikane, ipi ni bora, wapi inapatikana na at the same time inatafuta na kuhamasisha wawekezaji katika hizo pembejeo. Tunaona kwa sasa waTanzania wanavyofaidika na kiwanda cha mbolea cha minjingu, lakini wakati kilipokuwa cha umma? Utajaza mwenyewe.
   
Loading...