Wabunge CCM kumpigia makofi kitwanga kipindi anajibu swali ina maana gani

WHITE HOUSE

Member
May 8, 2016
22
20
Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga kabla hajafukuzwa uwaziri alikua akipigiwa makofi na wabunge wa CCM ndani ya bunge wakati akijibu swali aliloulizwa huku akiwa amelewa,
Najiuliza maswali mengi sana kuhusu waziri Huyu kupigiwa makofi wakati inaonekana hakuwa anajibu swali kiufasaha,
Je wabunge wa CCM walijua ni kwanini walikua wanapiga makofi?
Je wabunge wa ccm walikua makini kweli kujua Kitwanga alichokua akijibu?
Je hawa wabunge walilielewa swali aliloulizwa Kitwanga kabla hawajapiga makofi juu yake?
Kama wabunge walimpigia makofi baadae ilionekana usahili wa alichojibu hakikuoneka kulingana na swali lenyewe na IKULU iko Dar lakini ikamuona hayuko sawa kuanzia kimwili mpaka kiakili, inakuaje wabunge wako karibu na Kitwanga kwenye viti wakashindwa Pata utimamu wa akili na kumpigia mlevi huku haoneshi uhalisia wa kimwili na majibu ya swali husika,,???
 
mkuu hata mimi nilijiuliza sana hili swala.

hii inaonyesha mule ndani haongalii hoja kinachoangaliwa ni wa chama gani anaongea
Hapa nakuunga mkono, bunge liko sooo divided, kila mtu anamsapoti mwenzake hata kama kaongea pumba!! Kiukweli sikuamgalia reaction ya wabunge wa sisiemu ila kama walipiga makofi, hiyo kali!! Kuna uwezekano ni wale BABES sasa safari hii wa sisiemu!!
 
hakuna cha ajabu hapo.si tunashuhudia hata mbunge wa ccm akitoa lugha ya matusi anashangiliwa? wao kila kitu ni "mbele kwa mbele".iwe ulevi,mipasho hapa kazi tu.
 
Inaonyesha ESPIRIT DE CORD, we came together we will leave together!! Team cohesiveness no matter what!!

Asilimia kubwa wanachukua muda kwenye salamu na kimtukuza bwana mkubwa kama vile malaika mkuu. Ni aibu sana waziri mzima muda uliopewa nusu nzima unaimaliza kwenye salamu alafu hotuba yako inaishia katikati.
 
Wanasema mazoea hujenga tabia, mtu haelewi nini? Kinazungumzwa Bali kazoea kupiga makofi kila mbunge wa chama tawala akisimama kuongea.
 
Kuna wabunge wapo kwa ajiri ya wananchi wao, wengine wapo kwa ajiri ya masilahi binafsi na masirahi ya chama. Kuna wengine hupeleka maswali ili tu wananchi wa jimbo lake wajue kuwa mbunge wetu shida zetu anazifuatilia wakati majibu wakati mwingine anakuwa nayo!
Kuna wabunge mizigo wengi sana bungeni akiwemo mbunge wa jimboni kwangu nilikozaliwa
 
Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga kabla hajafukuzwa uwaziri alikua akipigiwa makofi na wabunge wa CCM ndani ya bunge wakati akijibu swali aliloulizwa huku akiwa amelewa,
Najiuliza maswali mengi sana kuhusu waziri Huyu kupigiwa makofi wakati inaonekana hakuwa anajibu swali kiufasaha,
Je wabunge wa CCM walijua ni kwanini walikua wanapiga makofi?
Je wabunge wa ccm walikua makini kweli kujua Kitwanga alichokua akijibu?
Je hawa wabunge walilielewa swali aliloulizwa Kitwanga kabla hawajapiga makofi juu yake?
Kama wabunge walimpigia makofi baadae ilionekana usahili wa alichojibu hakikuoneka kulingana na swali lenyewe na IKULU iko Dar lakini ikamuona hayuko sawa kuanzia kimwili mpaka kiakili, inakuaje wabunge wako karibu na Kitwanga kwenye viti wakashindwa Pata utimamu wa akili na kumpigia mlevi huku haoneshi uhalisia wa kimwili na majibu ya swali husika,,???
Wabunge Wa ccm huwa hawafikirii sana , wao huwa wanasubiri kuunga mkono hoja, na kujipendekeza kwa mawaziri...... Hakuna jipya nategemea kwao
 
Back
Top Bottom