Katika hali isiyo ya kawaida, hofu ya wabunge wa CCM katika mchakato wa uundwaji wa katiba mpya imetokana na kuogopa aina ya wajumbe watakaoingia kwenye tume ambayo Rais ataiunda. Soma sehemu hii: "Hoja nyingine iliyojengwa na wajumbe ni kwamba kama wataruhusu mabadiliko ya Katiba yafanyike, utafika wakati tume atakakayoiunda Rais itakuwa na wajumbe wenye utata kama akina Dk. Slaa (Wilbrod Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA) na Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Profesa Mwesigwa Baregu. Kwa hiyo lili kuepusha mambo yasiyofaa katika mchakato mzima wa Katiba, lazima waanze kuwa macho kuanzia sasa badala ya kukaa kimya na kusubiri mambo yaharibike."My take: Wabunge wa CCM wanaona ni bora kupambana na Mwenyekiti wao (Rais) kuliko kuruhusu akina Dr. Slaa kwenye mchakato.Source: Mtanzania ya leo Ukurasa wa 2.