Wabunge badilikeni, kuweni na msimamo wa kifikra kabla ya kuamua na kupitisha mambo makubwa ya Nchi

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
5,159
5,399
Umuofia kwenu.

Bunge la Tanzania limesheni watu wa sampuli zote. Wenye vyeti aina zote uvijuavyo duniani. Ndiyo ni bunge lenye full package.

Hili ndiyo bunge ambalo ukichukua ramani ya mipango yao ukaitumia nchi nyingine unapata matokeo chanya.

Wakati wa kupitisha TOZO wabunge hawa walishangilia mno kuisifia serikari lakini baada ya maumivu ya TOZO kuwa makali serikali ikaja na sailing ya kunyoa TOZO kiduku ili kuleta unafuu wakasimama kushangilia utadhani ni watu wawili tofauti.

Wabunge badilikeni mnatia aibu kwa raia wenu kuweni na msimamo wa kifkra kabla ya kuamua na kupitisha mambo makubwa ya nchi.
 
Katiba ingelikuwa inaruhusu mgombea binafsi basi kidogo Serekali ingepata challenge kutoka bungeni lakini leo hii wabunge wote ni kutok ccm unadhan nan atanyanyua mdom wake kutetea wananchi unatak 2025 akatwe? Aisipitishwe na chama kugombea? Hata kama ni wewe ungeufyata kimya ili kulinda ugali wako.
 
Mbunge pekee anayejielewa kwa sasa awapo bungeni ni Mh. Mpina tu. Hata ile dhambi yake akiwa waziri mwandamizi ya kupima samaki kwa rula na ukatili wa kuchoma hovyo nyavu za wavuvi inaweza kusameheka kwa sasa.
 
Kuna mh Aida Kenan kama sijakosea huyu mbunge sio mnafiki hua anasema, anashauri, sema wabunge wetu hawajui wapo hapo kwa ajili ya nani, na kingine wananchi tunapochagua viongozi tunangozwa na mihemko ya uchama bila kuangalia athari za siku za mbele.
 
Back
Top Bottom