Wabunge 50 Tanganyika 20 Zanzibar inakuwaje mgao huu??

mrelbattawy

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
564
112
Nimejaribu kupitia Rasimu nimeona hili la wabunge wa Jamuhuri ya Muungano watakuwa 70, Tanganyika itatoa 50 na Zanzibar 20 ukiacha wale wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha watu wenye ulemavu na wengine mmoja mmoja kuwakilisha m'me na m'ke katika majimbo ya uchaguzi.,

Ivi warioba na tume yake hapa kweli walitenda haki? mana ukiisoma Rasimu inazungumza wazi wazi ni shirikisho la nchi 2., inakuwaje nchi moja 50 nyengine 20??

Mbona hawa Tanganyika wanataka kuendelea kutuburuza tena kwene bunge? Ivi burundi nchi ndogo lakini inawakilisha wabunge sawa na nchi kubwa kwenye muungano wa afrika., inakuwaje Muungano huu wa Tanzania?

Nimeskia Kenya na Unganda wamevutiwa na Muungano huu uliotoka kwenye rasimu wa Tanzania wanataka kujiunga lakin sasa itakuwaje kwa mgao huu wa wabunge??
 
Kama nitapiga kura ya hapana kwa rasimu hii basi ni kwa hicho kipengele.

Rasimu inapendekeza shirikisho la nchi mbili huru kwa hiyo ni lazima kuwe na uwiano katika mambo yahusuyo muungano.

Hiyo ratio ya 50:20 imetumia kanuni gani?
 
Na Je kuchangia kwenye pato la serikali ya Muungano napo wanaangalia 50:50, ama wanaangalia population 50:20. Ni nini wanachoangalia ama watachoangalia?
 
Fumbua macho mkuu, hyo inawezekana vip? Tanganyika iwe sawa na zanzbr hata hvyo z azbr imepewa weng ukilingalisha na uwakilish wake ilitakiwa mpate wabunge 5! Tatizo lako unateswa na udini!
 
Kama nitapiga kura ya hapana kwa rasimu hii basi ni kwa hicho kipengele.

Rasimu inapendekeza shirikisho la nchi mbili huru kwa hiyo ni lazima kuwe na uwiano katika mambo yahusuyo muungano.

Hiyo ratio ya 50:20 imetumia kanuni gani?

hapo unapotoka zaidi, unajua population ya tanganyika vs ya zanzibar iko kwa ratio ipi? hata hao tuu watakuwa wamependelewa! ilitakiwa kama ni 70:7 to be fair, fuatilia us na nchi nyingine populn ina impact gani!
 
Miye hapana yangu itapatikana kwa kutokuwekwa mahakama ya Qadhi kwenye katiba.

hapo unapotoka zaidi, unajua population ya tanganyika vs ya zanzibar iko kwa ratio ipi? hata hao tuu watakuwa wamependelewa! ilitakiwa kama ni 70:7 to be fair, fuatilia us na nchi nyingine populn ina impact gani!

Hiyo ratio inaweza kutumika kama kuna mgao wa chakula cha msaada kwa waathirka wa njaa! Hapo nitakubaliana na wewe.

Linapokuja swala maamuzi, katiba inataka simple majority kwa hiyo ZNZ kuingia katika uwiano wa namna hiyo ni kutengeneza mgogor mwingine wa kikatiba ambao utakuja kuundiwa tume baada ya miaka michache ijayo.
 
Fumbua macho mkuu, hyo inawezekana vip? Tanganyika iwe sawa na zanzbr hata hvyo z azbr imepewa weng ukilingalisha na uwakilish wake ilitakiwa mpate wabunge 5! Tatizo lako unateswa na udini!

Una akili sn, zanzibar haifikii ht wilaya kondoa wanataka usawa. Je pato la Taifa watakubali kuchangia 50:50?
 
kama contribution ya pato ni 50% ni it ok!
haiwezekani wazenj hawana uwezo huo,hii mambo ya serikali tatu yanakwenda kuua muungano sasa hivi.kumbe ndo maana kambarage alikua amegoma kabisa...ratio ya wabunge wa muungano pia ni issue kubwa.
 
...

Ivi warioba na tume yake hapa kweli walitenda haki? mana ukiisoma Rasimu inazungumza wazi wazi ni shirikisho la nchi 2., inakuwaje nchi moja 50 nyengine 20??

...

Nimeandika kwenye threads nyingine kadhaa humu JF. Kuna option 2 ili kuwa na uwuiano wa haki kama ifuatavyo:-

Option I: Kwa kuzingatia population ratio ya nchi washirika: Kwa mujibu wa Sensa ya 2012 (ambayo pia wa-Tanganyika wengi hawakushiriki kwa sababu mbalimbali) inaonesha ration ya Tanganyika:Zanzibar ni roughly 43:1 au 98%:2%. Kwa maana hiyo, idadi ya wabunge 70 maana yake, kwa kuzingatia ratio, Tanganyika ina-deserve 98% x 70 = 68.6 (69) na Zanzibar ina-deserve 1.

Option II: Mgao uwe sawa kwa sawa: Kwa maana hiyo kila nchi inatakiwa kuwa na wabunge 35. Sawa, ila kama ndivyo, na gharama za muungano tubebe sawa kwa sawa. Kwa mfano, bajeti ya Wizara ya Ulinzi kwa 2013/14 ni T.Shs. tr. 1.2/=. Kwa maana hiyo, Zanzibar inatakiwa kuchangia T.Shs. bn. 600/= kwa mpango huo wa sawa kwa sawa. Ila nasikia bajeti ya Zanzibar kwa kipindi hicho hicho ni T.Shs. bn. 600/=; sijui inakuwaje hapo! Vivyo hivyo kwenye ajira, kila penye ajira 100; 98 wa-Tanganyika wanobaki wa-Zanzibari.

Polepole kitaeleweka tu na kelele zenu za "tuacheni tupuwe". Kimsingi, Warioba kawapendelea sana ninyi!
 
Hiyo ratio inaweza kutumika kama kuna mgao wa chakula cha msaada kwa waathirka wa njaa! Hapo nitakubaliana na wewe.

Linapokuja swala maamuzi, katiba inataka simple majority kwa hiyo ZNZ kuingia katika uwiano wa namna hiyo ni kutengeneza mgogor mwingine wa kikatiba ambao utakuja kuundiwa tume baada ya miaka michache ijayo.
kwamaana kila itakapohitajika ipigwe kura,wazenj watapoteza kwa ajili ya uchache bungeni,hawatakubali.
 
[h=2]Wabunge 50 Tanganyika 20 Zanzibar inakuwaje mgao huu??[/h]
Aisee mrelbattawy umegundua eeh! Hata mimi nimeshangaa Zanzibar kupewa idadi kubwa hivyo ya wabunge. Kama haki ingetendeka, ilitakiwa kila mbunge 1 Zanzibar kuwe na wabunge 33 wa Tanganyika. Ikumbukwe kwamba ratio ya population ya Tanganyika to Zanzibar ni 43,625,354 : 1,303,569, kwa hiyo kwa wabunge 50 wa Tanganyika, sana sana wangetoka wabunge 2 wa Zanzibar
 
haiwezekani wazenj hawana uwezo huo,hii mambo ya serikali tatu yanakwenda kuua muungano sasa hivi.kumbe ndo maana kambarage alikua amegoma kabisa...ratio ya wabunge wa muungano pia ni issue kubwa.

Muungano ni ule wenye manufaa kwa wananchi na unaofurahiwa kuwepo. Vinginevyo, hakuna haja ya muungano. Czech na slovakia wametengena wakati Scotland wana wafanya referendum kujitoa UK. Hivyo mambo ni kawaida kabisa.
 
hapo unapotoka zaidi, unajua population ya tanganyika vs ya zanzibar iko kwa ratio ipi? hata hao tuu watakuwa wamependelewa! ilitakiwa kama ni 70:7 to be fair, fuatilia us na nchi nyingine populn ina impact gani!

Ungesoma vizuri kwenye mada hapo juu ungetoka hilo gugu la usingizi., umeambiwa ruwanda na burundi ni nchi ndogo lakini kwenye muungano afrka wamechangia wabunge sawa na nchi kubwa., wabunge 9 kila nchi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom