Wabunge 46 na mawaziri 13 wahamasisha wananchi kutaka JK ajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge 46 na mawaziri 13 wahamasisha wananchi kutaka JK ajiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nurujamii, Aug 9, 2009.

 1. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wanaharakati wapinga kauli za wabunge kuhusu JK

  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete

  Wanaharakati wa Haki za Binadamu, Elimu na Mazingira (Thren), wamepinga baadhi ya kauli zilizotolewa na wabunge kwa kumtaka Rais Jakaya Kikwete ajiuzulu kwa kile walichoeleza kuwa ni kushindwa kwa Serikali kutekeleza maazimio ya Bunge.

  Pingamizi hilo lilitolewa jana na wanamazingira 217 kutoka mikoa ya Dodoma, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Mara, Kigoma, Kilimanjaro, Unguja, Mbeya, Rukwa, Morogoro, Ruvuma, Kagera, Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Tanga, Mtwara na Tabora ambao wamesema kauli hizo zinalengo la kuvuruga amani ya nchi.

  Wanaharakati hao wamewataja wabunge 46 na mawaziri 13 ambao walisema wamekuwa wakizunguka maeneo mbalimbali nchini kuwahamasisha wananchi waunge mkono ajenda yao ya kumtaka Rais ajiuzulu.

  Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya kuhifadhi misitu na mazingira (Mreca), Mchungaji William Mwamalanga, alionya kuwa mpango huo ni matokeo ya uhasama, ufisadi, uzushi, udini, fitna na majungu yaliyojikita ndani ya chama tawala, ili kudhohofisha Serikali na vyombo vyake.

  Mchungaji Mwamalanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa mtandao wa Thren, alisema kimsingi wanaotakiwa kujiuzulu ni wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wameshindwa kutumia vikao na miiko ya uongozi kuwafukuza mafisadi papa ndani ya chama chao ambao alisema wameanza kutoa vitisho kwa wazalendo wanaojaribu kuzuia kasi yao ya ufisadi.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Maumivi ya kichwa huanza pole pole!!
   
 3. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Huyu Mchungaji naye haelewi mambo ndani ya chama. Wabunge ndani ya CCM hawawezi kumfanya Mwenyekiti wao ajiuzuru, lakini wakiwa wabunge wanaweza kutumia nguvu yao ya mhimili wa bunge kufanya hivyo.

  Ikiwa ni kweli wabunge wanafanya hivyo, kimsingi wanafanya vema. Kuna ombwe la uongozi katika nchi.
   
 4. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,441
  Trophy Points: 280
  haiwezekani!!!!!!!, kwanini rais wetu
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  ehee! yamefika hapa!
   
 6. M

  Mvutakamba Member

  #6
  Aug 9, 2009
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa ni wabunge na mawaziri wa CCM ? Kuna nini hasa kuna endelea ?
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280


  Yaani msanii huyu haoni ushahidi chungu nzima unaothibitisha kwamba Kikwete Urais umemshinda na atakuwa ameifanyia Tanzania msaada mkubwa kujiuzulu sasa ili kupisha uchaguzi mpya badala ya kusubiri 2010 na wala hastahili kupewa tena uongozi wowote ule ndani ya chama au serikali.
   
 8. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  mie naona kikwete ni weak sana kuliko watu walivyo mtegemea.
   
 9. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kikwete ni Rais safi Tanzania haijawahi kupata na huenda haitampata tena kama huyu atakapomaliza muda wake. Maisha bora kwa kila mtanzania hayatawezekana hivi hivi, hili Kikwete analijua na ili yawezekane mpaka msingi uliopo ubomolewe na ujengwe mwingine mpya. Hili si jambo rahisi ni kama kubomoa Dar es Salaam ya leo na kijenga siku moja.

  Kizuizi ni nini? Vikwazo vilivyopo kutokana na siasa chafu ya "UONGO NA KIFICHO" ambayo ilihubiriwa kipindi cha Mkapa badala ya "UWAZI NA UKWELI" Hii imezuia kwa kasi mpya ya maisha bora kwa kila mtanzania. Kila mwenye upeo wa kufikiri ataona hivi kuwa maisha bora hayataweza kudhihirishwa ikiwa kumekuwa katika msingi wetu wa nchi UONGO NA KIFICHO uliozaa UFISADI Kikwete anaopambana nao. Sasa kipindi cha kwanza cha mchezo Kikwete anafanya kazi za Rais wawili YEYE mwenyewe SAFI na Mkapa Fisadi; yaani kufanya UWAZI NA UKWELI WA KWELI na kisha ndipo MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA. Kwa kweli Kikwete TUTAMKUMBUKA KWA KURUDISHA UWAZI NA UKWELI na hata Rais aliyemng'atua waziri mkuu tena shoga yake kabisa.

  Kama ni rafiki mnafiki yeye ameweza kutomkumbatia, Je kuna walakini hapa kweli? Sijui lakini hizi ni tafiti na fikra zangu.

  Kwa Kikwete nina IMANI naye kabisa kama RAIS ALIYETUKUKA anayesikiliza hoja na kujibu hoja. Anayeheshimu fikra sahihi za watu wake. Anayechukulia kila jambo kwa uzito BUT slowly kujiridhisha na siyo MPAYUKAJI. Tutampata wapi Rais kama huyu KIPINDI KIJACHO? Ee Mungu TUSAIDIE!!! Linalosemekana ni umbeya YEYE amelichunguza na kulirihidhisha kwa umma wa watanzania na kuwaonesha kuwa sisi siyo WADANGANYKA bali WAZALENDO WATANZANIA. Kwa kifupi Kikwete ameongoza kipindi kigumu kuliko hata cha Nyerere kwa kuwa wakoloni waliopo hatuwezi kuwafukuza, ni stakeholders wa nchi hii. One can imagine. Tuwe wakweli katika FIKRA watanzania. Hata kama ni changes we can not change overnight. Imagine mafisadi wamekuwa kwenye sytem tangu wakati wa mwalimu na ni zaidi ya miaka 30 na ndio tunaona hivi sasa. To restore the trust and harmony it will take sometime, quite sometime; probably more than 30years. Kwa kuwa ni kweli tunajua ni rahisi kubomoa kama walivyofanya mafisadi BUT kujenga it will and may take quite sometime.

  No matter what we need to start to change and a change we can believe in is KIKWETE na hili kwa Kikwete nina imani naye. Ni Rais pekee aliyeweza kuibadilisha siasa ya Tanzania ya kuwaogopa watu kama Mkapa ambao hata Mo Abraham wameweka wazi si Rais bora bali alikuwa BORA RAIS na hata yeye sasa ndio anajua, na anatamani hata akifa afe kifo kama cha Balali. Ama kwa hakika asiona hili basi na atuachie uraia wetu. Ni rais aliyefanya hatimaye watanzania tukaweza kujadili wazi wazi mambo muhimu yanaikabili nchi. Angeweza kama amiri jeshi mkuu kuzuia kama Mkapa alivyofanya BUT hakufanya hivyo!!
   
 10. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Waswahili husema ukiona moshi wafukuta, ujuwe moto waja...
   
 11. GreatConqueror

  GreatConqueror Member

  #11
  Aug 9, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Huu ni upuuzi MTUPU hivi kweli yupo waziri yeyote anayeweza kufanya/kufikiria hili? Labda mawaziri kivuli. Hawa wachungaji tuwenao makini sana siku hizi maana anaweza kuwa anatafuta umaarufu ili siku moja aanzishe 'DECI' yake.. au nia ni kujipendekeza kwa RAIS!?
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Jinsi mambo yanavyoenda naanza kuhisi karibu tutaiona njia. CCM hawana namna ya kuongoza muda mrefu ujao bila ya kujaribu kufanya mabadiliko ya dhati.Na pengine inaweza kufanya wakakigawa chama chao katika makundi tofauti tofauti. Yes, panapofuka moshi, huwa pana moto!!
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  JK kwaniini asi step down??imetosha....he is not fit...for second term...
   
 14. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimemtetea sana JK hapa ukumbini lakini sasa naona habebeki.

  Ukweli nafurahi kuona demokrasia inavyokuwa kwa mijadala motomoto ndani na nje ya bunge. Lakini bado JK kama rais na amiri jeshi mkuu anapaswa kujua kwamba kuna mambo ya kufanyiwa mijadala na mambo yasiyohitaji mjadala hata dakika moja bali kushughulikiwa kwa haraka na kwa ukali.

  Mfano masuala kama ya Kiwira na Richmond hayahitajidi mjadala wa miaka miwili.... these are not issues for discussion but to be dealt with strongly and promptly!
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Aug 9, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kwa hili, Tanzania tunakabiliwa na wakati mgumu sana. Wakati ni kweli kuwa Kikwete ameshindwa kuongoza nchi, vile vile si kweli kuwa kampeini hizo za kichinichini zina nia njema kwa nchi. Zingekuwa na nia njema basi zingefanyika hadharani bila woga wowote, nionanvyo mimi ni kuwa kampeini hizi kama ni kweli zipo basi zinaendeshwa na watu waliobanwa na Kikwete huyohuyo kwenye misheni zao za kifisadi.
   
 16. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakuna utamaduni wa kujiuzulu Rais katika Tanzania kwa hiyo basi ,Jk aendele tu afuate nyayo za Brown wa kule UK, atumia mbinu za kiujanja ujanja jahazi lifike au liende mrama tugawane mbao .
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapo hakuna mkoa hata mmoja uliotoa hayo madai,hizo ni mbinu za kutaka kuonyesha kuwa CCM inakubaliwa katika mikoa hiyo wakati sio kweli ,hao wabunge 46 na wengine ni uwongo na siasa za propaganda ,ukiangalia kwa makini hizo sehemu zilizotajwa na mkoa wao wa Unguja zote ni sehemu ambazo Chama Cha CCM kimekuwa kinaporomoka kwa kasi sana ,sasa hizi ni hila za wizi ambazo zinachomekewa ili pindipo watakapoiba kura waunganishe na hisia zao kuwa mikoa hiyo ilimpa sapoti Mwenyekiti wa CCM.

  Anaposemwa Jakaya mjue inasemwa CCM ,hivyo kuweni makini sana.Hawa CCM dalili za kufa kwao zimekuwa zikiwapa tabu sana siku hizi.
   
 18. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Wala haihitaji College Degree kuona kuwa Nchi inaendeshwa kama Danguro!!..Kila kitu kimekuwa hovyo,kila kiongozi anatamka lake,hakuna collective leadership tena......Wale tuliowachagua wengi wao wametugeuka na kila mtu anajali tumbo lake...na wale walioteuliwa kumsaidia kazi Mkuu...Leo wanamgeuka Mkuu wazi wazi,wamemuona Mkuu kapoteza sifa za Uongozi.Ule Mvuto aliokuwa nao 2005 haupo tena.....Hao Wabunge wanaozungumzwa kumkana Rais Wao ni wajanja wachache wanaofikiri watakubalika kwa wananchi kwa kumkana Mkuu wa Serikali yao!!
   
 19. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Who the BLEEP is TREN and Mchungaji Mwamalanga? Mbona story imekaa kizushi sana? Lakini zaidi ya hayo naamini KICHUGUU amezungumzia jambo muhimu, kama ni kweli kuna viongozi wanaotaka kushinikiza JK ajiuzulu wafanye hivyo kwa uwazi, wasiogope watashangaa kuona wananchi wengi watawaunga mkono.
  Naamini watanzania tumechoka... muda umefika wa kubadilika.....let's give another person to lead us and deifnitely not CCM! They had 40 odd years to prove their while but they have failed miserably....
   
 20. O

  Omega.Omega Member

  #20
  Aug 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni ndoto tu.
   
Loading...