Wabunge 400 wa kazi gani kwa nchi masikini Kama Tanzania?

Naishauri SERIKALI WAKATI wa mapitio ya kubadilisha KATIBA fanyeni mpango wabunge wapungue 400 nakitu wengi mno... MFANO mkoa Kama dar uwe na mbunge MMOja tu ilikuokoamatimizi ya FEDHA za walipakodi...mbunge MMOja mkuu wa mkoa na madiwani tu wanatosha KUENDESHA eneo husika...mchawi KUIMALISHA vituo vya police basiii

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mm kwa maoni yangu Wabunge wapunguzwe maana kazi ya mbunge kwa sasa sioni hata maana yake km ni kusikiliza kero zetu hawazisikilizi ww km mkazi wa eneo fulani ni mashahidi tangu mbunge ateuliwe alisha wahi hata kurudi kwenu kusikiliza matatizo yenu ni wachache sana wanafanya hivo wamebaki kupiga makofi bungeni na kutunga sheria mbovu zisizo na tija kwa taifa.
 
Wapo KISIASA ZAIDI hawana TIJA kwa TAIFA hebu Fikiria WABUNGE wa VITI MAALUMU wana KAZI gani BUNGENI na Nje ya BUNGE? NCHI YA AJABU KABISA
Hebu Fikiria Wabunge Fake 19 Serikali inawalipa MISHAHARA kisa KUIKOMOA CHADEMA

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Mkuu, bora wabunge viti maalum watakaoingizwa kwa weledi wao kuliko hawa wa kuwakilisha eti moshi mjini na moshi vijijini watu wawili tofaut. Gairo na kilosa wawili tofauti. Iringa mjini na vijijini wawili tofaut. Arumeru east na west wawili tofaut na nk. Hii ni hasara. Wanaenda kutengeza/ kuzalisha nini bungeni?
 
Polisi ni muhimu sana katika jamii, kitu cha muhimu ni kuwalipa mishara mizuri kwa wakati unaopaswa. Hiyo mishara ya ma DC na RC ingetumika kuongeza polisi tena wenye usafiri hata kama ni pikipiki.
 
kujadili jambo kwa kutumia furaha sana au uchungu sana hutoa matokeo yasiyofaa.

leo hii tunaona wabunge 600 hawafai, sababu si robo wala 1/8 wanatoka upinzani, ni sababu hakuna kabisa mbunge kutoka upinzani. inawezekana kabisa tungekuwa na wabunge 300 wa upinzani story zingekuwa tofauti.

ukimuuliza mfuasi wa ccm, nayeye atakwambia kama kuna uwezekano waongezwe wafikie 900.

kama taifa sasa tumefikia hatua ya kujadili mambo kwa itikadi za vyama, wala si maslahi ya nchi tena.
 
Polisi ni muhimu sana katika jamii, kitu cha muhimu ni kuwalipa mishara mizuri kwa wakati unaopaswa. Hiyo mishara ya ma DC na RC ingetumika kuongeza polisi tena wenye usafiri hata kama ni pikipiki.
Kweli kabisa polisi ni muhimu shida wanavyotumika sio kwa tija maana polisi Tanzania utaalamu na intelijensia yao ni kuzuia mikutano na maandamano ya kisiasa lakini sio kutimiza lile lengo la msingi kumlinda raia na mali zake mfano kwenye matukio ya wizi na ujambazi Wana maneno mengi na rushwa tu ila hakuna wanachokifanya
 
Tatizo sio polisi. Ni viongozi wa polisi. Wale viongozi wa juu wa polisi hawazidi 10 Ndio wamefanya nchi ikawa hivi wakishirikiana na vyombo vyingine vya dola.
 
Back
Top Bottom