Wabunge 400 wa kazi gani kwa nchi masikini Kama Tanzania?

Inaumiza sana! Kazi anayoifanya mwalimu au nesi halafu ukija kulinganisha na kazi ya mbunge halafu ukaangalia tofauti ya mishahara yao, kwa binadamu halisi utahuzunika kwa dhati. Hapo haujafikiria wingi wa wabunge
 
kujadili jambo kwa kutumia furaha sana au uchungu sana hutoa matokeo yasiyofaa....
Hapana majimbo mengi yameongezwa kisiasa hayana tija wabunge wapo bungeni miaka nenda miaka rudi na matatizo ya wananchi majimboni mwao ni yale yake kwa miaka yote sasa wakazi gani?

Madiwani wanatosha kabisa kufikisha kero zao kwa wenyeviti wa halmashauri na mbunge mmoja akayasemea bungeni kwa ngazi ya wilaya na serikali ika fanyia kazi

Pesa nyingi sana zinahudumia wanasiasa wasio na faida wala tija huku wafanyakazi wenye tija wakilipwa fedha kiduchu, huu ni ujinga wakutupwa na sijui kwanini kila kiongozi anaye kuja hawazi kupunguza utitiri wa hawa watu bungeni wasio na tija kabisa wanacho waza ninkuongezea mzigo wa kodi wananchi ili hawa wanunge waendelee kulelewa ni ujinga kabisa.
 
Licha ya kuwa wengi sana sijona mchango wa maana au fikra mpya kuiletea maendeleo nchi.

Mbunge mtu mzima mchango wake ni kwa Nini Mbunge mwenzake wa kike, kwa nini amevaa suruali yenye kubana makalio

Wale wa viti maalum toka Zanzibar ni hawachangii chochote zaidi ya kuchukua posho
 
Back
Top Bottom