Wabunge 400 wa kazi gani kwa nchi masikini Kama Tanzania?

Two dimension array

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,593
2,380
Anaongea Bishop Mpemba.

Kodi nyingi tunazo kusanya zinaishia kuwalipa mishahara first class citizen!

Wabunge 400, DC 120, RC 30+ , Wakurugenzi na MaDAC . Tunaitaji kuwa na watu wachache kwenye uwalikishi wa mawazo ya wananchi na kuimarisha Jeshi la Polisi!

Kwa kweli ni hasara kwa Taifa hatuna haja ya kuwa na wabunge wengi wanalipwa mishahara mikubwa ajabu na hawazalishi.

Masikini na mnyonge ndo mnaangaika kuwakamua Kodi na tozo mbalimbali huku wafanyakazi wa umma wakiwaa na maisha magumu kwa miaka 7 bila kuongezewa mishahara

 
Hakuna kitu kinachonikera kuwa na viongozi kama maRC na maDc, turekebishe sheria huku Wabunge wa viti maalum huku wakuteuliwa dah acha tutafute katiba nzuri ya kuondoa uozo huu, ila iwe yenye manufaa na tija kwa mwananchi wa kawaida
 
Private sector, PAYE inapigwa kwenye Gross, kwakuwa bunge sio serikali na ndio maana miposho na mishahara ni tofauti na ya serikalini, iingizwe tu kwenye PAYE.

Fikiria, 400 X 11,000,000 X 0.3 X 12 = 15,840,000,000

Kwa mwaka tungekuwa tunapata angalau hiyo tsh 15.84bn kutoka kwenye kodi wakatwazo wabunge, na wala wasizipeleke kwenye kapu kuu, wazilete vijijini, kila mwaka wapeleke 1bn kwa vijiji 15, angalau baada ya 5yrs, vijiji 75 vitafikiwa na huduma fulani au kunyanyua chochote kile, iwe shule au kilimo, mikopo ya masharti nafuuu n.k.

Kwa hii miaka ya CCM madarakani, chukulia kwa miaka 30 X 15 = 450 vijiji vingekuwa vimenufaika na hiyo 1bn, ni mfano, inaweza kuwa hata mgao wa 50m kwa kila kijiji ambapo vijiji 300 vitanufaika na hiyo pesa kila mwaka, sijui tunavyo vingapi ila hata kama mzunguko ukiwa wa kila baada miaka 3 kwa kijiji sio mbaya.
 
Wabunge ni kundi la kunyonya wananchi.Wanatunga sheria za hovyo na wanapiga pesa zetu bila hata la maana wanalofanya.mishahara ya kufulu mtu kwenda mjengoni kulala lala analipwa 12'000'000 kwa mwezi,wakati mwalimu wa tz mwenye masters anayefanya kazi ngumu analipwa 450,000takehome.Mbunge mmoja wa std 7 anakula mshahara wa walimu 26 wenye shahada.

TUNATAKA KATIBA MPYA.
 
Hao hao tunaowalipa pesa nyingi bado wanatutubgia sheria za hovyo na kuuza rasimali zetu
Ndo vyanzo vipya vya mapato boss, kwa nafasi ya nchi yetu kiuchumi, hatupaswi kuwa hata mwananchi mmoja anayekuwa exempted na kodi ya msingi, kuanzia raia namb moja, maana kwa hapa tulipo sisi ni WENYE MAHITAJI MAALUMU yaani, sasa hizo privilege za ku-enjoy majukumu ya kuisogeza nchi kwenda kwenye ndoto yetu tunaziweka iliiweje? Kuiga walioendelea tayari?

China walifanya kazi kwa filimbi kufikia walipo, Ulaya waliteka nchi nyingine na kuiba rasilimali na watumwa ili kuwa pale walipo, Amerika walifanya biashara vitani kuwa pale walipo, SISI tunafanya nini kutoka hapa tulipo? Tunaiga maisha ya mbele bila kujua tulipo?
 
... halafu bila aibu kabisa wanataka waongezwe mishahara na marupurupu! 😅

👊 :cool:✌️💥
1626813236216.png
 
Hayo yote yanaweza kubadilishwa kwa upatikanaji wa katiba mpya, Je, Tuendelee kudai katiba mpya au Tukaushie ili dawa iendelee kuingia vizuri
 
Back
Top Bottom